Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21576 articles
Browse latest View live

Kanye West asema Wamarekani Waafrika 'walipendelea' kuwa watumwa

$
0
0


Msanii wa muziki wa rap nchini Marekani Kanye West,Haki miliki ya pichaPA
Image captionKanye West hivi majuzi alirekodi wimbo akitetea kumuunga mkono Donald Trump
Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amesema kuwa utumwa wa Wamarekani Waafrika uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliopita lilikuwa chaguo lao.
'Unaposikia kwamba utumwa ulifanyika kwa zaidi ya miaka 400.. miaka 400? ni kama walipendelea hilo kufanyika', alisema katika tovuti ya burudani ya TMZ.
Nyota huyo hivi karibuni aligonga vichwa vya habari kwa kumuunga mkono rais Donald Trump.
Watu weusi walilazimishwa kutoka Afrika na kuelekea Marekani katika karne za 17, 18 na 19 na kuuzwa kama watumwa.
Presentational white space
West baadaye alituma ujumbe wa Twitter na kusema kwamba hakueleweka vyema na kwamba alizungumza kuhusu miaka 400 kwa sababu 'fikra zetu' haziwezi kufungwa kwa miaka mingine 400.
Katika mahojiano na TMZ West alisema hivi sasa tunachagua kufanywa watumwa swala lililozua hisia kali kutoka kwa mfanyikazi mmoja mweusi katika kampuni hiyo.
Bwana Lathan alisema kuwa matamshi ya msanii huyo yalionekana kutolewa bila kufikiria.
"Una haki ya kuamini chochote unachotaka , lakini ujue kuna ukweli katika dunia ya sasa na athari zake kwa kila kitu ulichosema', aliongezea huku nyota huyo akisimama na kujikuna kidevu.
"Lazima tukabiliane na ukandamizaji uliotokana na mika 400 ya utumwa ambayo ulisema kuwa watu wetu walipendelea, bwana Lathan aliendelea akiongezea kwamba nimeshangazwa na ndugu yangu nimeumizwa kwa wewe kusema kitu ambacho sio cha kweli.
Katika mahojiano hayo ya TMZ West amemtaja bwana Trump kuwa rafiki yake na kusema kuwa rais huyo ni miongoni mwa watu wake anaowapenda sana.
Matamshi yake yalizua hisia kali katika mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wa twitter wakisema kuwa msanii huyo anafaa kusoma upya vitabu vya historia.
Presentational white space
Inajiri siku chache tu baada ya West kutoa wimbo ukimtetea rais Trump ambaye amesisitiza kuwa anapigania Wamarekani.
Wimbo huo uliozua utata Ye vs p The People ulizua hisia kali miongoni mwa wasanii akiwemo Snoop Dogg ambaye alionekana kukasirishwa na maneno ya wimbo huo.
"Like a gang truce, the first Blood to shake the Crip's hand," West raps, akitaja makubaliano kati ya magenge mawili ya mjini Los Angeles.
Mpwa wa Snoop Dogg msanii Daz Dillinger baadaye alichapisha ujumbe wa video akiwataka wanachama wa genge la Crip kumkabili Kanye iwapo watakutana naye mjini California.
Kanda hiyo ya video inachunguzwa na polisi kulingana na ripoti.
West amezua hisia kali kutokana na hatua yake ya kumuunga mkono Trump na wahafidhina kama vile Scott Adams na Candace Owens, ambaye amezungumza dhidi ya vuguvugu la Black Lives Matter.

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 02.05.2018

$
0
0


Wenger
Image captionWenger
Naibu mkufunzi wa Liverpool Zeljko Buvac anapigiwa upatu kumrithi mkufunzi wa Arsenal anayeondoka Arsene Wenger . (Pravda BL, via Mirror)
Arsenal huenda isimlipe mkufunzi wake mpya zaidi ya kitita cha £8.5m ambacho mkufunzi wake Arsene Wenger alikuwa akipata kwa mwaka (Daily Mail)
Eric Baily
Image captionBaily
Beki wa Manchester United Eric Bailly, 24, ana wasiwasi kuhusu hatma yake katika klabu hiyo baada ya kutochezeshwa na mkufunzi wa klabu hiyo Jose Mourinho. (Mirror)
Mabeki Matteo Darmian na Daley Blind, wote wakiwa na umri wa 28 wameambiwa kwamba wako huru kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Times)
Chelsea inamnyatia Anthony Martial,
Image captionChelsea inamnyatia Anthony Martial,
Chelsea inamnyatia Anthony Martial, 22, iwapo Manchester United haiwezi kumrai raia huyo wa Ufaransa kusalia katika klabu hiyo ya Old Trafford (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Roma Radja Nainggolan, 29, amepinga madai kwamba anahusishwa na uhamisho wa Chelsea na Manchester United kwa kuamua kusalia katika klabu hiyo ya Serie A. (Daily Mail)
Antonio ConteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Huenda wakufunzi wa Chelsea na Napoli Antonio Conte na Maurizio Sarri wakabadilishana vilabu.(mirror)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho amethibitisha kwamba kumekuwa na hamu ya mchezaji huyo kutoka nje huku klabu za Manchester United na Manchester City . (Manchester Evening News)
Mshambuliaji Andy Carroll, 29Haki miliki ya pichaEMPICS
Mshambuliaji Andy Carroll, 29, huenda asishirikishwe katika mechi muhimu ya West Ham dhidi ya Leicester siku ya Jumamosi baada ya mgogoro na meneja david Moyes katika mazoezi. (Guardian)
Ross McCormack atapata takriban £1m kama nyongeza ya marupuru iwapo Astona Villa watapandishwa daraja hadi katika ligi ya Premier, licha ya kutocheza mechi hata moja msimu huu. (Sky Sports)
Beki wa Brazil David Luiz, 31 huenda akaelekea Napoli iwapo Rafael Benitez atarudi katika uwanja wa San Paolo kuchukua mahala pake Maurizio Sarri
Beki wa Brazil David Luiz, 31 huenda akaelekea Napoli iwapo Rafael Benitez atarudi katika uwanja wa San Paolo kuchukua mahala pake Maurizio Sarri kama mkufunzi mwisho wa msimu huu. (Sun)
Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard ataweza kukabili shinikizo iwapo ataajiriwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Rangers , kulingana na mchezaji mwnza wa zamani Frank Lampard. (Talksport)
Kiungo wa kati Gerard Deulofeu, 24, amesema kuwa anaweza kuelekea Watfor kwa uhamisho wa kudumu baada ya kukiri kwamba hatma yake katika klabu ya Barcelona haijulikani.(Mundo Deportivo)

Madrid yatinga fainali ya tatu mfululizo UEFA

$
0
0


Karim Benzema (kulia) alifunga magoli yote mawili
Image captionKarim Benzema (kulia) alifunga magoli yote mawili
Mabingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu Real Madrid imefanikiwa kutinga hatua ya fainali muchuano ya Ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuindosha Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya magoli 4-3.
Wakiwa na faida ya magoli 2-1 ugenini, Real Madrid ilihitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kutinga fainali ya michuano hii mikubwa kwa upande wa vilabu barani Ulaya.
Joshua Kimmich alianza kufunga kwa mapema kipindi cha kwanza kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Madrid baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Marcelo.
Ulikuwa mchuano uliovutia wengi
Image captionUlikuwa mchuano uliovutia wengi
Makosa ya mlinda mlango wa Bayern Sven Ulreich yaliizawadia Madrid goli la pili lililopachikwa na Benzema kabla ya James Rodriguez kusawazisha.
Bayern walikua na nafasi ya kuondoka na ushindi lakini mikwaju ya Corentin Tolisso na Thomas Muller iliokolewa vyema na mlinda mlango Keylor Navas ambaye alikuwa katika kiwango kizuri.
Real itakumbana na Liverpool ama Roma katika fainali itakayopigwa mjini Kiev, Ukraine May 26.

'Sikutosheka kushiriki ngono mara 5 kwa siku'

$
0
0


Bi Barker
Image captionBi Barker
Shirika la wahisani la Relationship charity Relate limetoa wito kwa watu walio na uraibu wa ngono kupata usaidizi nchini Uingereza. Waathiriwa wawili wanazungumzia kuhusu athari za kuwa na pepo la ngono.
''Mara nyengine hata kushiriki ngono mara tano kwa siku haikutosha''.
Mama wa watoto 3 Rebecca Barker anasema kuwa tatizo hilo lilitawala maisha yake 2014 na kuvunja uhusiano wake
Alikuwa akitaka kushiriki ngono na mpenziwe mara kwa mara .
"Ilikuwa kitu cha kwanza kuja katika fikra zangu wakati nilipoamka , sikuweza kuitoa katika fikra zangu'' , alisema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 kutoka eneo la Tadcaster Kaskazini mwa Yorkshire.
"Nilihisi kana kwamba kila kitu kilikuwa kikinikumbusha kuhusu tendo la ngono. Nadhani ilitokana na shinikizo la mawazo . Nilihisi kwamba mwili wangu wote ulikuwa ukitamani kushiriki katika shughuli hiyo.
"Ilikuwa ikinigonga na dakika tano baadaye niliitaka kushiriki tena tendo la ngono.
Nilihisi upweke, nilisalia nyumbani kwa sababu nilihisi aibu, nilikuwa nikifikiria kufanya ngono kila wakati. Hata iwapo hakuna mtu ambaye angeweza kugundua kilichokuwa katika fikra zangu , nilihisi vibaya kuwa karibu na watu wengine.
Rebecca Barker wakati alipokuwa na tatizo la pepo wa ngono.Haki miliki ya pichaREBECCA BARKER
Image captionMs Barker alivunja uhusiano wak na mpenziwe na kubadilisha maisha yake ili kutibu pepo wa ngono.
Pepo la ngono la Bi Barker lilizua matatizo makubwa katika uhusiano wake, ijapokuwa mpenziwe alipendelea hali yake kwa mara ya kwanza lakini alishindwa kuidhibiti.
"Mara ya kwanza alikuwa akifurahia lakini mwisho mwisho hakuweza kuelewa na baada ya miezi michache alianza kuuliza maswali ni wapi hisia hizo zilikuwa zikitoka .
"Alinishutumu kwa kuwa na uhusiano wa nje- alidhani kwamba nilikuwa nikihisi kufanya makosa ndiposa nikataka kushiriki naye tendo la ngono.
  • Uhusiaono wake ulivunjika
Mnamo mwezi Novemba 2014, bi Barker "alitaka kupumzika kutoka katika uhusiano huo na alienda kuishi na mamake.
"Nilipoondoka nilimwambia mpenzi wangu kwamba nilihitaji kuimarika kitabia na hisia. Alinikubali kuondoka na uhusiano wetu ukaisha polepole''
"Nilikuwa chini ya uangalizi wa mtaalamu wa matatizo ya kiakili wakati huo-ambaye alikuwa akinimbia kwamba atabadilisha dawa zangu , lakini hakusema kwamba kulikuwa na makundi ya usaidizi.
Bi Barker alipatikana na shinikizo la kiakili 2012 baada ya kujifungua mwanawe wa tatu. Alisema kwamba alibadilisha kazi aliyokuwa akifanya , akakosana na mpenzi wake na kuhamia Ufaransa.
''Nilifanya mabadiliko katika maisha yangu ili kukabiliana na shinikizo hilo la mawazo na pepo huyo wa ngono na ni hatua hiyo ilionisaidia'', alisema.
Relate inaelezea uraibu wa ngono kuwa kushiriki ngono isioweza kudhibitika na shirika la afya duniani WHO linatarajiwa kuweka tatizo hilo miongoni mwa matatizo ya kingono katika orodha yake ya kitaifa ya magonjwa (ICD) mnamo mwezi Mei 2019.
Graham, ambaye jina lake limebadilishwa anasema kuwa tatizo lake la kuwa na pepo wa ngono lilimlazimu kulala nje na mamia ya makahaba na kumfanya kuwa na hatia kubwa.
Wakati unapokuwa na pepo huyo unakuwa ukifikiria kitendo hicho mara kwa mara kutoka wakati unapoamka hadi wakati unapoenda kulala. Haikuwa hali nzuri, wakati unapoamka alfajiri na kutumia dawa za kukabiliana na magonjwa ya zinaa .
Inakuharibia maisha yako.
Wanandoa wakishikana mikonoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBi Barker amesema kuwa ngono nio kilichokuwa kitu cha kwanza katika mafikira yake
  • Alikuwa na uhusiano na makahaba 3
Graham, ambaye yuko katika miaka yake ya 60 anakadiria kwamba alilipa mamia ya paundi kwa mwezi kwa miaka kadhaa ili kuimarisha uhusiano wake na baadhi ya makahaba
"Uhusiano ulioanza kama urafiki kazini ulichochea mwengine -lakini kama mahusiano ya afisi ambayo yangeanza kutokana na mhusika mmoja kutokuwa na raha katika ndoa yake tatizo langu lilikuwa pepo wa ngono ambaye nililazimika kumpatia mahitaji yake kila siku.
Una uhusiano mmoja na baadaye unataka mwengine na baadaye unajiingiza katika mwengine. Na baadaye niligundua kwamba hatua mojawapo ya haraka ya kukabiliana na tatzio langu ni kulipia huduma hiyo .
Nilikuwa nikishiriki ngono na makahaba mara tatu ama hata nne kwa wiki.
Ni sawa na kuwa mlevi , ni tatizo linalokujia katika akili yako-Unahisi na kupanda hisia unapolifikiria na unapolitenda katika mipango yako na baadaye unapomaliza unajiambia kwamba hutawahi kufanya tena.
Graham alisita kuendelea na maisha hayo ya kutisha wakati mkewe alipopata barua pepe na kumshutumu.
Alitafuta usaidizi kwa mashirika yanayowasaidia watu wa tatizo lake nchini Uingereza kama vile Sex Addicts Anonymous (SAA), shirika ambalo lina makundi 78 nchini Uingereza na kwamba amewacha kujihusisha na ngono nje ya ndoa yake kwa miaka kadhaa.
Wakati nilipohudumiwa nakumbuka kuhisi kumshukuru Mungu- na kusema kitu kitabadilika .
Nileinda kwa shirikja hilo kwa tiba ya kuwacha kushiriki katika ngono za nje ya ndoa.
Nahisi afueni kulekea katika mikutano hiyo na kuona watu ambao wako katika hali mbaya zaidi ya nilivyokuwa. Kwa watu walio katika tatizo hili nataka wajue kwamba kuna njia nyengine na unaweza kujiondoa katika tatizo hilo.
Mwanamume akitoa pete yake ya ndoa.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGraham alisema wakati mke alibaini kwamba ametibiwa

NI KWELI MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAAA!!!!!

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MEI 3, 2018

Binyavanga Wainaina: Mkenya mpenzi wa jinsia moja kufunga ndoa na raia wa Nigeria

$
0
0


BinyavangaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Mwandishi vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina ambaye ametangaza wazi kwamba ni mpenzi wa jinsia moja amefichua kwamba atafunga ndoa mwaka ujao.
Mwandishi huyo ambaye alifichua hali yake ya kimapenzi mwaka 2014 siku yake ya kuzaliwa akiwa na umri wa miaka 2014 amesema harusi hiyo itafanyika nchini Afrika Kusini.
"Nilimuomba mpenzi wangu tufunge ndoa wiki mbili zilizopita. Na alikubali, karibu mara moja. Yeye ni raia wa Nigeria. Tutakuwa tunaishi Afrika Kusini ambapo atakuwa anahudhuria masomo mwaka ujao. Tutaoana huko, mapema mwaka ujao," Bw Wainaina aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Aliahidi kwamba kutakuwa na karamu kubwa kwa Wakenya jijini Nairobi mwaka ujao.
Baadaye, aliongeza kwamba ana uhakika kutakuwa na sherehe kubwa kwa Wanigeria pia.
"Hakuna lililonishangaza zaidi kuliko kupendana na mtu huyu, ambaye ni mpole na mwenye moyo wa ukarimu.
"Najichukulia kuwa mwenye bahati sana kwamba yeye ananipenda na tulipendana majuzi tu, lakini tumefahamiaka na tumekuwa tunachumbiana tangu 2012."
Bw Wainaina alifichua kuwa yeye ni mpenzi wa jinsia moja mwaka 2014 kwenye makala aliyoipa jina „Mimi ni mpenzi wa jinsia moja, mama."
Presentational grey line

Binyavanga ni nani?

  • Kenneth Binyavanga Wainaina ambaye ana umri wa miaka 47 sasa ni mwandishi wa vitabu na mwanahabari.
  • Mwaka 2002 alishinda tuzo mashuhuri ya uandishi kuhusu Afrika ya Caine.
  • Jarida la Time mwaka 2014 lilimuorodhesha Wainaina kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.
  • Mnamo 1 Desemba, 2016 alitangaza kupitia Twitter Siku ya Ukimwi duniani kwamba alikuwa ana virusi vya Ukimwi.

Raia wa Ujerumani atekwa Somalia

$
0
0


Wapiganaji nchini SomaliaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWapiganaji nchini Somalia
Mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundu raia wa Ujerumani ametekwa nyara katika mji mkuu wa Somalia.
Habari zinasema watu wasiofahamika waliokuwa wamebeba silaha, walimteka ndani ya eneo la ofisi hizo mjini Mogadishu na kumtoa nje kwa kutumia mlango wa nyuma, ili kuweza kuwakwepa walinzi waliokuwa katika lango kubwa la mbele.
Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu amesema wana wasiwasi mkubwa na usalama wa mfanya kazi mwenzao.
Amesema muuguzi huyo aliyetekwa alikuwa akifanya kazi kila siku kuokoa maisha ya baadhi ya Wasomali wenye hali mbaya.

Wachezaji wazuri ambao hawana kandarasi: Reina, Robben, Buffon, Can, Ribery, Wilshere

$
0
0


Wachezaji 11 ambao kandarasi zao zimekamilika
Image captionWachezaji ambao hawana kandarasi na timu zao wanaweza kuunda timu nzuri
Msimu wa kananda unaelekea ukingoni , swala linalomaanisha kitu kimoja: ,maajenti kunaza kufanya biashara mwish wa msimu huu.
Dirisha la uhamisho la ligi ya Uingereza halifunguliwa hadi 17 Mei lakini kuna wachezaji wengi waliokamilisha kandarsi zao ambao wako tayari kufunga virago na kuondoka.
Miongoni mwao ni kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, ambaye amepewa mkataba mpya Arsenal, wachezaji wawili wa Bayern Arjen Robben na Franck Ribery na kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can.
Lakini je unawajua wachezaji wngi ambao walionyesha mchezo mzuri msimu huu kulingana na shirika la utafiti la soka CIES footbal Observerytory?
Kundi hilo la utafiti limetengeza orodha ya wachezaji 50 kulingana na majukumu sita ya wachezaji ikiwemo, kupokonya mpira, kusambaza, kutengeza na fasi za magoli, kushambulia. Kipa wanapimwa kulingana na mbao waliofungwa kwa dakika mbali na asilimia ya mabao waliookoa.T

Wachezaji 10 ambao wamekamilisha kandarasi zao

Pepe ReinaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJe kipa wa Napoli Pepe Reina atarudi Liverpool alikotoka?
Shirika hilo la utafiti wa soka CIES linawapima wachezaji hao katika viwango vya hadi 100 kutoka wale waliocheza hadi chini ya dakika 10000 msimu huu. Orodha hiyo ya kumi bora inawapigia upatu mabeki kutoka Itali , iwapo kocha wa Liverpool anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi.
1. Pepe Reina - ameorodheshwa wa 91. Kipa huyo mwnye umri wa miaka 35 aliyeichezea Liverpool ameisaidia Napoli kusalia katika ligi ya Serie A akiwa hajafungwa kwa takriban mechi 17 ikiwa ni zaidi ya kipa yoyote yule.
2. Vicente Guaita - ameorodheshwa wa 90. Kipa huyo wa Getafe, 31, imeripotiwa alitia kandarasi na Crystal Palace mapema msimu huu lakini sasa amepokea maombi kutoka Atletico Madrid. Raia huyo wa Uhispania ana rekodi nzuri ya kuokoa mashambulizi.
3. Nafasi ya tatu. Arjen Robben - ameorodheshwa wa 89. Winga huyo wa Bayern mwenye umri wa miaka 34 huenda amepunguza kasi yake lakini kwa kuwa ni mchezaji anayeweza kutamba na mpira anaweza kuwa na thamani nzuri. Tayari amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kusalia na klabu hiyo.
3..Nafasi ya 3. Gianluigi Buffon - ameorodheshwa wa 89. kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 ameonyesha ubora wake Juventus msimu huu. Anatarajiwa kustaafu mwisho wa msimu huu ijapokuwa amesema kuwa huenda akaendelea.
5. Andrea Barzagli - Ameorodheshwa wa 86. Ana sifa za kuimarisha safu ya ulinzi ya Juventus akishirikiana na Giorgio Chiellini, baada ya kushindwa mechi moja pekee kati ya 21 msimu huu. Kumuuza mchezaji huyo wa umri wa miaka 36 nje ya Juventus itakuwa vigumu.
6. Andrea Masiello - Ameorodheshwa wa 84. beki huyo wa klabu ya Atalanta 32, amekuwa katika ligi ya Serie A tangu kashfa ya kuuza mechi 2011 lakini ameonyesha thamani yake msimu huu huku klabu hiyo ikiwa na lengo la kufuzu katika michuano ya ligi ya Yuropa.
Emre CanHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionEmre Can alijiunga na Liverpool kutoka Bayer Leverkusen mwaka 2014
6. Emre Can - Ameorodheshwa wa 84. Amehusishwa pakubwa na uhamisho wa Juventus, iwapo mchezaji huyo wa kiungo cha kati atafanikiwa kuvutia mchezaji mmoja wa Turin kujiunga na Liverpool .Ana mabao matatu katika ligi ya premia na ametoa pasi 4 zilizosababisha magoli katika msimu wa 2017-18,.
8. Milan Badelj - Ameorodheshwa wa 83. mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ametoa pasi nzuri katika kila mechi ikilinganishwa na mchezaji mwengine yeyote wa klabu ya Florentina msimu huu huku ikiripotiwa kwamba Tottenham ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia raia huyo wa Croatia.
8. Kwadwo Asamoah - ameorodheshwa wa 83. Inter Milan wanapigiwa upatu kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia anaweza kucheza katika kiungo cha kati. Mchezaji huyo wa Ghana pia anahusishwa na uhamisho wa Everton na Tottenham.
8. Rafinha - ameorodheshwa katika nafasi ya 83. Mchezaji huyo wa Bayern mwenye umri wa miaka 32 amepewa kandarasi mpya ya kusalia na mabingwa hao wa Bundesliga lakini hakupendelea.

Majina ya wachezaji nyota ambao bado wana thamani

Franck RiberyHaki miliki ya pichaAFP
Image captionFranck Ribery ameshinda taji la Bundesliga kwa mara nane ndani ya msimu 11 Bayern Munich
Chini katika orodha kuna wachezaji ambao wanaonyesha umahiri wao na ambao bado wanaweza kuwa nyota wa Ulaya.
11. Franck Ribery - Ameorodheshwa wa 82. Kama Robben, winga huyo wa Ufaransa amepewa mkataba mpya wa kusalia Bayern ambapo anaweza kushinda taji lake la tisa la Busliga lakini huenda akeleka katika klabu nyangine kw amkataba wa kudumu ughaibuni
13. Jack Wilshere - Ameorodheshwa wa 81. Kuimarika kwa kiungo huya wa kati wa Arsenal ambako kumezongwa na majeraha lakini ni mchezaji ambaye amekuwa akitamba na mpira zaidi ya kiungo wa kati mwengine yeyote katika ligi ya Uingereza. Je kupunguzwa kwa mshahara wake kutamfanya asalie katika klabu hiyo?
18. Sergio Canales - ameorodheshwa wa 78. Klabu ya Real Betis ni miongoni mwa klabu ambazo zimeripoti kuwa na hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Real Sociedad ambaye ametoa pasi 11 zilizosababisha mabao katika mashindano yote msimu huu.
Stefan de VrijHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBeki wa Lazio Stefan de Vrij amefunga mabao mengi zaidi ya beki yeyote yule katika ligi ya Serie A msimu huu (six)
18. Stefan de Vrij - Ameorodheshwa wa 78. beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26 ameshiriki katika mechi za Lazio msimu huu, akifunga mabao mengi zaidi ya beki mwengine yeyote wa Serie A.
Raia huyo wa Uhalonzi amehusishwa na uhamisho wa Inter Milan, Manchester United na Barcelona.
18. Max Meyer - Ameorodheshwa wa 78. kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 2 kutoka klabu ya Schalke ambaye amekamilisha pasi asilimia 92% msimu huu anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu huku Arsenal na Liverpool zikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Ujerumani
47. Holger Badstuber - Anaorodheshwa wa 72. Beki huyo wa zamani wa Bayern mwenye umri wa miaka 29 anakaribia kukamilisha kandarasi yake ya mwaka mmoja katika klabu ya Stuttgart.
Mbali na majera ni miongoni mwa wachezaji wenye pasi nzuri zaidi katika ligi ya Bundelsiga . Lazio ni miongoni mwa timu zinazomnyatia.
Yohan CabayeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionYohan Cabaye alijiunga na Crystal Palace mwaka 2015
32. Yohan Cabaye - Amorodheshwa wa 75. kiungo huyo wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 32 bado anaonyesha mchezo mzuri kwa pasi zake murua mbali na kuharibu pasi za upinzani- swala ambalo linaweza kuchochea kupewa kandarasi mpya katika klabu hiyo.
41. James Collins - Ameorodheshwa wa 73. West Ham haijakuwa na msimu mzuri , lakini beki huyo mwenye umri wa miaka 34 huonyesha thamji yake anapokuwa vizuri. West Ham imeshinda asilimia ya mechi 34 anapocheza ikilinganishwa na asilimia 19% wakati anapowekwa benchi.

Mchezaji mwengine ambaye amekamilisha kandarasi yake lakini hayuko katika orodha ya CIES

Mario BalotelliHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMario Balotelli amefunga maboa katika ligi akiichezea klabu ya Nice msimu huu na amewashukuru mashabiki kwa misimu miwili mizuri.

Mada zinazohusiana

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 03.05.2018

$
0
0


Anthony Martial
Image captionAnthony Martial
Jose Mourinho yuko tayari kumchezesha Anthony Martial katika safu ya kati ya mashambulizi msimu ujao iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atakubali kusalia Manchester United. (Mail)
Manchester United imempatia kipau mbele beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27, kuchukua mahala pake beki wa kushoto wa Uingereza Luke Shaw, 22, msimu ujao. (Manchester Evening News)
Manchester United imempatia kipau mbele beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester United imempatia kipau mbele beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27,
Manchester City inapima uzito wa kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Jamaican Leon Bailey, 20. (Goal)
Claude Puel huenda akapoteza kazi yake kama mkufunzi wa Leicester iwapo hatamaliza vizuri ligi hiyo(Talksport)
Fernando Torres
Image captionFernando Torres
Klabu ya ligi ya Major League nchini Marekani DC United ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Uhispania Fernando Torres, 34, au mshambuliaji wa Boca Juniors na Argentina Carlos Tevez, 34. (Goal)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Marouane Fellaini, 30, anaamini kwamba Manchester United ilifanya makosa kwa kukataa kumuongezea kandarasi yake mara moja na badala yake kumwacha katika hali nzuri ya kuhamia klabu nynegine. (Sport Voetbal Magazine. via Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Marouane Fellaini, 30,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
West Brom iko tayari kuanza mazungumzo na mkufunzi wa Brentford Dean Smith na naibu kocha wa Leicester Michael huku wakianza kumsaka meneja mpya.. (Mail)
Rafael Benitez anataka kuwepo kwa makubaliano kuhusu hatma yake na Newcastle kuhusu bajeti yake ya uhamisho na uwezo huku klabu hiyo ikijaribu ikimfunga kwa kumpatia kandarasi mpya ya muda mrefu. (Mirror)
Rafael Benitez
Image captionRafael Benitez
Mshambuliaji wa Uhispania Gerard Deulofeu, 24, hatarajii kurudi katika klabu iliomkuza Barcelona mwisho wa msimu huu akisema kuwa Watford bado inamtaka kusalia msimu ujao.. (Cadena SER - in Spanish)
Chelsea inataka kulipwa kitita cha £10m ili kumuuuza kiungo wa kati wa Uholanzi Marco van Ginkel, 25, ambaye ameshiriki katika ligi ya Premia kwa dakika 11 pekee (Football.London)
Kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 24Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 24, anasema kuwa hafikirii kuhusu hatma yake na kwa sasa anajaribu kuisaidia timu hiyo kutoshushwa daraja kutoka katika ligi ya Premia msimu ujao (Reuters)
Burnley inapanga kuwasajili beki wa Bristol City Joe Bryan, 24 kwa kitita cha £6m. (Mirror)

Asbel Kiprop: Bingwa wa Kenya wa Olimpiki adaiwa kutumia dawa zilizoharamishwa

$
0
0


Asbel KipropHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAsbel Kiprop alimaliza wa sita katika mbio za 1500m mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016
Bingwa wa zamani wa Olimpiki katika mbio za 1500m Mkenya Asbel Kiprop amesema atathibitisha kwamba yeye ni "mwanariadha msafi" baada ya taarifa kuibuka kwamba aligunduliwa akiwa ametumia dawa zilizoharamishwa michezoni.
Mwanariadha huyo wa miaka 28 ambaye ni bingwa wa dunia mara tatu alipatikana akiwa ametumia dawa za kuimarisha damu aina ya EPO.
Aligunduliwa baada ya kufanyiwa vipimo wakati akiwa hashiriki mashindano.
Kiprop alimaliza wa pili Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 jijini Beijing lakini akakabidhiwa dhahabu baada ya mshindi Rashid Ramzi kutoka Bahrain kubainika kwamba alikuwa ametumia dawa zilizoharamishwa.
Kupitia taarifa, Kiprop amesema hawezi kuharibu maisha yake ya uanariadha kwa kutumia dawa zilizoharamishwa.
"Nimekuwa kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini katika michezo Kenya - na nina imani na naunga mkono vita hivi," alisema Kiprop ambaye anashikilia nafasi ya tano ya muda bora zaidi katika historia kwenye mbio za 1500m.
"Siwezi kutaka kuharibu mambo ambayo nimeyafanyioa kazi tangu niliopokimbia mbio zangu za kwanza za kimataifa 2007. Ninatumai kwamba ninaweza kuthibitisha kwamba mimi ni mwanariadha 'msafi' kwa njia yoyote ile inayowezekana."
Asbel Kiprop ndiye Mkenya wa karibuni zaidi kujipata katika sakata la kutumia dawa zilizoharamishwa.
Mabingwa wengine waliopatikana na kosa hilo ni pamoja na Jemima Sumgong ambaye alipigwa marufuku ya kutoshiriki shindano lolote kwa muda wa miaka minne.
Bingwa wa zamani wa Boston na Chicago Marathon Rita Jeptoo alipatikana na makosa ya kutumia EPO mwaka 2014 na akapigwa marufuku ya miaka minne pia.
Wanariadha zaidi ya 40 kutoka Kenya wamepatikana na kosa la kutumia dawa za kutitimua misuli katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

NI KWELI MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAAA!!!!!

PICHA 2: Hatimae Neymar amerudi Ufaransa

$
0
0

Staa wa timu ya taifa ya Brazil anayecheza club ya Paris Stain Germain ya Ufaransa Neymar baada ya kuchukua headlines wiki kadhaa zilizopita kutokana na kutoonekana wakati wa game ya PSG na Monaco ya kutangaza Ubingwa wa Ligue One sasa amerejea.
Neymar amerejea Ufaransa baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake mwezi March nyumbani kwao Brazil na alikuwa anategemewa kuwa atarejea uwanjani wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi lakini kuna tetesi kuwa anaweza kuichezea PSGkabla ya msimu kumalizika.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Neymar alichukua headlines wiki kadhaa zilizopita baada ya kutoonekana siku ya PSG wakitangazwa kuchukua Ubingwa na yeye akiwa kwao Brazil kitendo ambacho kilitafsiriwa na baadhi ya watu kama dharau.

UTAFITI: Kutokula matunda kunavyochelewesha kushika mimba

$
0
0

Bila shaka umewahi kusikia tafiti nyingi pamoja na wataalamu wa masuala ya afya wakieleza madhara ya ulaji wa vyakula vya mafuta mengi ikiwa ni pamoja na kuongezeka uzito, magonjwa ya shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na mengineyo.
Utafiti mpya ambao umefanywa na wanasayansi wa Chuo kikuu cha Adelaide, Australia wamegundua kuwa ulaji wa vyakula vya mafuta mengi na sukari bila kula matunda mengi, huweza kusababisha tatizo la kuchelewa kupata ujauzito kwa wanawake.
Utafiti huu ambao umefanyika kwa wanawake nchini Australia, New Zealand, Ireland naUingereza wameeleza kuwa walibaini kuwa wanawake wanaotumia matunda mara tatu kwa mwezi, wanachukua kiwango cha nusu mwezi kwa wastani kushika mimba.
Hii ni tofauti na wanawake ambao hula matunda mara tatu au zaidi kwa siku ambao hushika mimba haraka zaidi.
Utafiri umeeleza kuwa wanawake wasiokula matunda kwa wingi wana hatari ya 12% ya kutokuwa na uwezo wa kushika mimba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja ukilinganisha na 16% ya wanaokula chakula chenye mafuta mengi, mara nne au zaidi kwa wiki.

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MEI 6, 2018


SERIKALI YAWAAGIZA MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI KOTE NCHINI KUWA CHACHU YA MABADILIKO

$
0
0


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Tixon Nzunda akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu  na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye kikao kazi cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OR-TAMISEMI  jijini Dodoma leo.
 Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Beatrice Kimoleta akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Tixon Nzunda kufungua kikao kazi cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OR-TAMISEMI  jijini Dodoma leo.

Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu  na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Elimu ( hayupo pichani ) wakati  akifungua kikao kazi cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OR-TAMISEMI  jijini Dodoma leo.
............................................................
Na Angela Msimbira, OR Tamisemi.

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa maelekezo ya kimkakati kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Serikali za Mitaa kote nchini kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko yenye kujenga ustawi wa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI  anayeshughulikia elimu Mhe. Tixon Nzunda katika  Kikao kazi  cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kwa Makatibu Tawala Wasaidizi  wa Mipango na Uratibu na Makatibu Tawala wa Serikali za Mitaa kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Akifungua kikao hicho Nzunda amesema kuwa ili kuleta mabadiliko yenye lengo la kujenga ustawi wa wananchi lazima kuwe na rasilimali watu wanaoamini mabadiliko,  hivyo Makatibu Tawala Wasidizi wa Mipango na Uratibu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa  ndio viongozi wanaopaswa kuelimisha jamii kuhusu dira, dhima  na programu ambazo Serikali inataka kufikia katika malengo makuu ya kujenga Ustawi wa wananchi.

Amewataka kubadilika kwa fikra, mtizamo, mwelekeo  na mikakati  ili kuleta mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa Serikali  kwa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na serikali katika kutoa huduma bora kwa jamii na kuleta maendeleo nchini.

“Ninyi ndio “engine” (gurumudu) ya kuleta maadiliko. Ndio kitovu cha kuleta Mabadiliko saidianeni na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi, msiogope kuwashauri, kuwakosoa, na kuwaelekeza ili kuleta maendeleo katika jamii mnazozihudumia” Amesema Nzunda 

Mhe. Nzunda  amesema kuwa Serikali imejipanga  kuona mabadiliko makubwa  ya kiutendaji kuanzia ngazi  za Serikali za Mitaa hivyo amewataka kutoa maelekezo ya Serikali yanazingatia Sera, sheria, kanuni  na programu za uendeshaji  kazi ndani ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“ Makatibu Tawala wa Mipango na Uratibu na Makatibu Tawala Wasidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanapaswa kujua dira ya Serikali  na mipango ya Mikoa  na kuwa na dhana ya usimamiaji na ufuatiliaji mtakuwa mmesaidia kuleta mabadiliko makubwa kwenye Mikoa yenu” Amesema Nzunda

Katika suala ya matumizi wa fedha za miradi Mhe Nzunda amesema kuna tatizo linaloendelea la kubadilisha matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi, fedha kukaa muda mrefu kwenye akaunti bila kufanyiwa kazi kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuchelewa kukamilika kwa miradi.

Aidha amezitaja baadhi ya changamoto za uandaaji wa mpango zinazoikumba mamlaka ya serikali za mitaa kuwa ni kutozingatia mpango mkakati, kutozingatia vipaumbele vya serikali  pamoja na kushindwa kusimamia bajeti ipasavyo.

Katika hatua nyingine Nzunda ameoneshwa kukerwa na tabia za baadhi ya Wakurugenzi ambao hadi sasa hawajawalipa fedha za uhamisho walimu waliohamishwa kutoka shule za msingi kwenda kufundisha shule za sekondari wakati serikali ilishatoa fedha hizo, hivyo aliwataka suala hilo kusimamiwa kikamilifu.

Akizungumzia juu ya baadhi ya halmashauri kupata hati chafu na nyingine kutapa hati zisizoridhisha amesema kitendo hicho kinasababishwa na uzembe wa watu wengi na sio Mkurugenzi peke yake bali wahusika wote watawajibishwa ili kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika ipasavyo katika majukumu yake.

Awali akimkaribisha Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa  Bi. Beatrice Kimoleta amesema lengo la kikao hicho ni kujitathmini juu ya bajeti iliyomalizika sasa pamoja na kuandaa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019.

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, ALGIERS
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC leo wanatupa karata yao ya kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika watakapomenyana na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers kuanzia Saa 4:00 usiku.
Yanga SC jana ilifanya mazoezi yake ya mwisho Uwanja wa Julai 5, 1962 na wachezaji wake walionekana wachangamfu pamoja na hali ya hewa ya baridi kali mjini Algiers.
Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera anayesaidiwa na Mzambia, Noel Mwandila na wazawa Nsajigwa Shadrack na juma Pondamali kocha wa makipa walionekana wenye kujiamini kuelekea mchezo huo.
Wachezaji watano nyota wa Yanga SC, mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, kiungo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na washambuliaji Ibrahim Ajib na Mzambia Obrey Chifrwa hawajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali.
Pamoja na Yanga na U.S.M. Alger, timu nyingine zilizpo Kundi D ni Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya ambazo zitamenyana zenyewe katika ufunguzi wa hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
Baada ya mechi ya kwanza ugenini Jumapili, Yanga itamenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
Kila la heri Yanga SC. Mungu ibariki Yanga DC, Mungu ibariki Tanzania. Amin. 

Chombo cha Satelaiti kilichoundwa Kenya kitarushwa katika anga za juu leo kutoka Japan

$
0
0


Mfano wa Satelaiti ndogoHaki miliki ya pichaSKY AND SPACE GLOBAL
Image captionMfano wa Satelaiti ndogo
Kenya inajiandaa kutimiza ndoto kubwa ya kisayansi leo Ijumaa. Chombo cha Satelaiti kilichoundwa nchini humo kitarushwa katika anga za juu hii leo kutoka nchini Japan.
Wanasayansi wa anga za juu kutoka Kenya waliokiunda chombo hicho tayari wako katika makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za juu nchini Japan, (JAXA) ambapo chombo hicho kitarushwa kutoka huko.
Nchini Kenya kwenyewe raia wataweza kufuatilia shughuli hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa You Tube, na sherehe maalumu ya kushuhudia imeandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi.
Satelaiti hiyo ndogo ni ya thamani ya dola milioni moja - gharama inayoonekana kuwa ndogo kifedha kwa kiwango cha sayansi ya anga za juu.
Satelaiti
Imebandikwa kamera mbili pamoja na vyombo vya kunasa na kupeperusha sauti.
Wahadhiri wa vyuo vikuu wanasema satelaiti hiyo inaweza kutoa huduma tofuati ikiwemo kukusanya taarifa zitakazosaidia katika kilimo na usalama, kutabiri hali ya hewa na hata kukabiliana na majanga.
Kenya kwa sasa inakabiliwa na janga la mafuriko ambalo limesababisha maafa makubwa.
Takriban watu mia mbili wamepoteza maisha yao, huku wengine zaidi ya laki mbili wamepoteza makaazi yao.
Huenda ufanisi katika uzinduzi wa satelaiti hii utaisaidia serikali pakubwa katika kujitayarisha kupambana na majanga ya aina hiyo.
Ndege zisizo na rubani kusafirisha damu Rwanda
Uzinduzi wa satelaiti hiyo leo unatokana na ushirikiano kati ya Idara ya Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, afisi ya masuala ya anga za juu ya Umoja wa Mataifa, na Shirika la utafiti wa anga za juu la Japan.
Kenya itaanza kushughulika kuunda satelaiti kubwa na bora zaidi iwapo uzinduzi wa leo utafanikiwa.

Tanzania yakanusha tuhuma za kukandamiza haki za Wamaasai

$
0
0


Mfugaji Parakapooni na ndugu yake na mwanawe Serengeti, Tanzania.
Tanzania imekanusha ripoti mpya inayoishutumu serikali ya Tanzania na baadhi ya kampuni za kitalii na uwindaji kwa kuendelezwa kwa vitendo vya unyanyaswaji na ukiukwaji wa haki za binaadamu kwa watu wa jamii ya Kimaasai wanaoishi katika baadhi ya vijiji wilayani Loliondo.
Serikali ya Tanzania inasema tuhuma hizo ni "potofu" na kwamba zina lengo la kuipaka matope serikali ya Tanzania.
Katika ripoti hiyo, taasisi ya Oakland inadai kwamba, ukiukwaji huu wa haki za binaadamu unahusiana na mgogoro wa ardhi ambao umekuwepo kwa miaka mingi kati ya watu wa Jamii ya Kimaasai wanaopigania urithi wa ardhi yao na serikali kwa upande wingine inayodai kutaka kutunza ardhi hiyo kwa ajili ya shughuli za uhifadhi.
Ripoti hiyo yenye kurasa zaidi ya arobaini imesheheni shuhuda za watu wa jamii ya Wamaasai wanaoishi katika ardhi hiyo inayopiganiwa.
Watu hao wamewaambia watafiti wa ripoti hiyo kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikitumia sheria za uhifadhi kuwatoa kwa nguvu katika ardhi ya urithi kutoka kwa mababu zao.
Wameongeza pia kwamba, kampuni hizo za kitalii na uwindaji zimekuwa zikiwazuia kutumia vyanzo muhimu vya maji na kushutumu kampuni hizo kutumia polisi kuwapiga na kuwakamata
Awali, kampuni mojawapo inayoshutumiwa iliwahi kuiambia BBC kwamba, wakati pekee ambao jamii hizi zinazuiliwa kuingia katika maeneo ya uwindaji kufikia vyanzo vya maji ni miezi kati ya Julai na Desemba ambao ni msimu wa uwindaji - kitu ambacho ni msimu wa upungufu wa maji pia.
Serikali kwa upande wake imekuwa ikikataa kuhusika na unyanyasaji wowote ule wa jamii hizi za Wamasai na kudai kwamba sheria za uhifadhi zilizopo zinalenga kutunza na kuendeleza tu maeneo ya uhifadhi na viumbe vilivyomo ndani ya maeneo hayo
Wamasai wakataa kuondoka katika ardhi ya Serengeti Tanzania
Mwishoni mwa mwaka jana serikali ilikatisha mkataba wa ruhusa ya uwindaji wa takribani miaka 25 wa kampuni ya OBC huku waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kigwangala akiamuru uchunguzi ufanyike juu ya utendaji wa kampuni hiyo.
Kwa takribani miaka sita sasa, sekta ya utalii imekuwa ndio chanzo kikubwa zaidi cha fedha za kigeni kwa Tanzania, huku ikikadiriwa kwamba sekta hiyo inaiingizia nchi kiasi cha Dola Bilioni 2 za Kimarekani kila mwaka.

Serikali ya Tanzania imesema nini?

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla amesema kupitia taarifa kwamba Watanzania na jamii ya kimataifa wanafaa "kupuuza taarifa hiyo potofu yenye lengo la kuipaka matope serikali na kuleta uchonganishi baina yake, wananchi na wawekezaji kwa lengo la kuleta uvunjifu wa amani."
Amesema kutokana na umuhimu wa eneo hilo kwa uhifadhi, uwepo wa vyanzo vya maji, eneo la mzunguko wa uhamiaji wa wanyamapori na maisha ya watu, serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ilichukua hatua stahiki za kutatua mzozo huo.
Dkt Kigwangalla amesema serikali ilichukua hatua hizo ikihusisha wadau wote muhimu yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, wawekezaji pamoja na wananchi.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wenye nia njema kwa uhifadhi na maendeleo ya wananchi katika kusimamia na kuendeleza rasilimali zilizopo katika eneo la Loliondo na maeneo mengine nchini kwa maslahi mapana ya Taifa," amesema waziri huyo.


Mwanamke ahukumiwa kifo kwa kumuua mumewe aliyembaka Sudan

$
0
0


Wanawake nchini Sudan wamekuwa wakiishi katika jamii zinazodhibitiwa na wanaumeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake nchini Sudan wamekuwa wakiishi katika jamii zinazodhibitiwa na wanaume
Mahakama moja nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mwenye umri wa miaka 19 kwa kumuua mumewe aliyembaka.
Jaji wa mahakama hiyo iliopo Omdurman alithibitisha hukumu hiyo ya kifo baada ya familia ya mumewe mwanamke huyo kukataa kufidiwa kifedha.
Wakati alipokuwa na umri wa miaka 16 , Nourra Hussein alilazimishwa kuingia katika ndoa na familia yake.
Hakuwa na raha hatua iliomlazimu kutoroka na kujificha katika nyumba ya shangazi yake.
Lakini miaka mitatu baadaye , anasema kuwa alidanganywa arudi nyumbani na familia yake ambayo ilimrudisha tena kwa mumewe.
Baada ya siku sita mumewe aliwaita binamu zake ambao walimzuia chini na mumewe akambaka. Wakati alipojaribu kumbaka tena siku iliofuata Nourra alimdunga kisu mumewe hadi akafariki.
Alitoroka na kurudi kwa wazazi wake ambao walimwasilisha kwa maafisa wa polisi.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake Jaji huyo aliipatia familia ya mumewe chaguo la kumsamehe Nourra lakini ikachagua auwawe.
Kesi yake imevutia hisia kali katika mitandao ya kijamii ambapo kampeni kwa jina #JusticeforNoura imekuwa ikisambazwa katika mtandao wa Twitter.
Mawakili wake wamewasilisha ombi la hukumu ndogo ya mauaji.
Wakati huoho kundi la wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu la Equality Now limesema kuwa litamwandikia rais Omar al-Bashir kumuomba amuonee huruma.
Mahakama inoyosimamiwa na Sheria ya kiislamu ilimuhukumu bi Hussein kwa mauji yaliopangwa mwezi uliopitwa na siku ya Alhamisi ikatoa hukumu ya kumnyonga kulingana na chmbo cha habari cha reuters
Mawakili wake wana siku 15 kukata rufaa.
Chini ya sharia za kiislamu familia ya mume inaweza kutaka ifidiwe kwa kulipwa fedha au iombe kifo, kulingana na mwanaharakati Badr Eldin Salah kutoka kwa vuguvugu la vijana ambaye alikuwa katika mahakama hiyo.
''Walichagua kifo na sasa hukumu imetolewa''.
  • Je mashirika ya haki za kibinaadamu yanasema nini?
Yasmeen Hassan wa Equality Now, mojawapo ya makundi yanayotaka hukumu hiyo kubadilishwa , aliambia BBC kwamba hukumu hiyo haikumshangaza.
''Sudan ni taifa ambalo wanawake wanaishi chini ya usimamizi wa wanaume na kanuni za kijinsia hufuatwa'' , alisema.
Ni taifa ambalo wasichana huruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 10.Kwa Noura ni msichana ambaye alitaka elimu na alitaka kufanikiwa na amekwama katika hali hiyo na sasa ni mwasiriwa wa utawala wa eneo hilo.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa hukumu ya mwanamke ya kifo ambaye alikuwa akijitetea inaangazia uzembe wa serikali kukabiliana na ndoa za watoto , ndoa za lazima na ubakaji katika ndoa.
''Utawala wa Sudan ni lazima ukabiliane na hukumu hiyo isiokuwa ya haki na kuhakikisha kuwa Nourra anapewa hukumu ya haki'', ilisema AI .
Viewing all 21576 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>