Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21579 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI

$
0
0


Na Mwandishi Wetu- Arusha
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kufanya mabadiliko katika Sera zake mbalimbali ili kuweza kuendana na wakati na kuwezesha kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa huduma kwa watanzania.

Katika kulifanikisha hilo Wizara imeamua kuipeleka Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 kwa wadau ili iweze kutolewa maoni na baadae kufanyiwa marekebisho kuiwezesha kuendana na wakati.

Akifungua kikao kazi cha wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali kuijadili Sera ya Taifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini Arusha, Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amesema  kuwa  maoni ya wadau ni muhimu sana  katika mchakato wa maboresho wa Sera hiyo.

Bibi. Sihaba Nkinga ameleza kuwa Serikali imeamua kuwashirikisha wadau hao kwani kwa asilimia kubwa ndio watekelezaji wa Sera hiyo katika majukumu yao ya kila siku.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa kazi zinazofanywa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na zoezi hili la kuiboresha Sera hiyo litaleta mageuzi makubwa katika Sekta.

Katibu Mkuu Sihaba Nkinga amesisitiza kuwa upatikanaji wa Sera nzuri utasaidia kupata Sheria nzuri na kukiwa na Sheria nzuri itasaidia utendaji mzuri wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.

“Tuitumie fursa hii kujadiliana vizuri ili tupate Sera itakayopeleka Sekta yetu ya NGOs mbele” alisisitiza Bibi. Sihaba.

Kwa upande wake Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Marcel Katemba amewataka wadau kuzingatia kikao kazi hicho kwani ndio fursa ya kutoa maoni yao ya kuiboresha Sekta ya Mashirika ya Yasiyo ya Kiserikali nchini

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Nicholous Zakaria ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na kuahidi kuendelea kusimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuratibu upatikanaji wa maoni kwa ajili ya maboresho ya Sera ya Mashirka Yasiyo ya Kiserikali nchini.
  Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Marcel Katemba akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali  ya kisera wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau wa NGOs kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Nicholous Zakaria  akieleza kuhusu umuhimu wa Baraza katika kuratibu utendaji kazi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
  Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini mara baada ya kufungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali watatu kulia waliokaa  ni Mkurugenzi na Masajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

NDEGE KUBWA YA ABIRIA YA EMIRATE KUTUA NCHINI YAIPANDISHA TANZANIA KATIKA UTOAJI WA UTOAJI HUDUMA YA USAFIRI WA ANGA

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imesema kuwa kutua kwa Ndege kubwa ya ‘gorofa’ A380 ya Fly Emirates imedhihirisha kuwa uwanja  wa Kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius K Nyerere  na vyombo vyake kuwa madhubuti katika usafiri wa anga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema  kuwa ndege hiyo licha kupata udhuru wa kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mauritius kumeipa heshima nchi katika kuwa na viwango katika utaoaji huduma ya usafiri wa anga.

Amesema kuwa Rubani wa ndege A380 ya Fly Emirates alifanya busara ya kuamua  baada ya kuona hali ya hewa ya Mauritius kutokuwa nzuri na  kuamua kutua kwenye Uwanja wetu wa kimataifa wa Mwalimu Julius  K Nyerere  na kuamini kuwa atatua bila wasiwasi.

Johari amesema kufuatia kutua kwa ndege hiyo kubwa  nchi imeweza kupata mapato katika huduma mbalimbali za kijamii kutokana na abiria waliokuwa katika ndege hiyo zaidi ya watu 500 ambao wote walilala katika hoteli zilizopo nchini.

Amesema kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria duniani ndio mara ya kwanza kutua katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu  Julius K. Nyerere hivyo inaonyesha kujizatiti katika utoaji katika utoaji wa huduma ya usafiri wa anga.

Ndege hiyo imetua Aprili 24 katika uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere ikitokea Dubai ambaye ilishindwa kutua mara tatu katika uwanja wa Mauritius na kuja kutua Tanzania

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa wamekuwa na asilimia  64 kutoka 37 kwa viwango vilivyowekwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) hivyo tuzo yake itatolewa na Rais wa shirika hilo kwa kumkabidhi Rais Dk.John Pombe Magufuli na mawasilino yanafanyika yanafanyika ujio wa Rais wa ICAO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kutua kwa ndege kubwa ya ya Emirate abiria duniani ya A380 ya Ghorofa iliyotua katika uwanja wa Ndege wa Mwalumu Julius Nyerere , jijini Dar es Salaam
Labels: 

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA DODOMA-BABATI ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Chemba Juma Nkamia mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251
  Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria  katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma-PICHA NA IKULU

DKT. MWAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA SEKTA ZA WIZARA YA HABARI BUNGENI LEO

$
0
0


 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Habari mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Utamaduni mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa na Mitindo mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Muziki mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.

Rais Magufuli awataka Watanzania kutolalamika kuhusu njaa

$
0
0


John Pombe MagufuliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJohn Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa raia wa Tanzania hawafai kulalamikia njaa wakati ambapo kuna mvua ya kutosha mbali na kwamba serikali inawajengea barabara mpya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wa barabara kuu ya Dodoma-Babati katika eneo la Kondoa, Magufuli alisisitiza kuwa Tanzania haifai kutarajia msaada wa chakula wakati ambapo kuna mvua na barabara.
''Musilalamikie njaa ama kusubiri misaada wakati ambapo taifa lina hali nzuri ya hewa huku barabara zikiendelea kujengwa'', alisema tumieni barabara na mvua kujipatia kipato.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, serikali ya Tanzania inatumia shilingi bilioni 107.6 kuhusu barabara kuu mpya ikiwa ni miongoni mwa ufadhili wa barabara wa shilingi bilioni 378.4 kutoka kwa shirika la msaada nchini Japan Jica na benki ya African Development Bank kulingana na rais Magufuli.
Barabara hiyo mpya yenye urefu wa kilomita 10,228 itapitia mataifa manane ikiwemo Afrika Kusini, Zimbabwe, zambia, Tanzania, Kenya, Sudan, Ethiopia hadi Misri.
Nchini Tanzania barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 1,222 na inatarajiwa kuchukua miaka 20.
Mvua kubwa inayonyesha Tanzania hivi sasa imetatiza huduma za usafiri kwa mabasi ya mwendokasi.
Usafiri wa mabasi hayo umesitishwa kutokana na mafuriko eneo la Jangwani.
Muandishi wa BBC Mjini Dar es Salaam anaeleza kuwa kila mvua kubwa inaponyesha huduma za mabasi hayo husitishwa kutokana na sababu kadhaa.
Mojawapo ya sababu ni kufurika maji kwa njia ambazo mabasi hayo yanapitia na pia kufurika maji kwenye kituo hicho kikuu ambapo mara ya mwisho mabasi kadhaa yaliharibika sababu ya kujaa maji.
Sababu nyingine ni kukatika kwa umeme kwenye vituo vyake wakati wa mvua - hivyobasi kusababisha kukwama kwa mfumo wake wa ukataji tiketi.

Uganda yaomboleza kifo cha Sokwe mkubwa zaidi nchini

$
0
0


Mbali na kuhifadhiwa, Sokwe huwa bado wanakuwa hatariniHaki miliki ya pichaTERENCE FUH NEBA, WWF CENTRAL AFRICAN REPUBLIC
Image captionMbali na kuhifadhiwa, Sokwe huwa bado wanakuwa hatarini
Ijumaa kutakuwa na mkesha kuomboelza kifo cha Sokwe mkubwa zaidi nchini Uganda ambaye amekufa akiwa na miaka 54
Mwaka 1964, zakayo alikuwa na mwaka mmoja alipokutwa ametelekezwa magharibi mwa Uganda.Kituo cha elimu ya Hifadhi ya wanyamapori kimesema kuwa alitunzwa na wataalam na baadae alifikishwa kwenye hifadhi ya taifa akiwa na miaka 13.
Zakayo aliishi sehemu kubwa ya maisha yake katika hifadhi ya Entebbe, ingawa hapo kwa mujibu wa mamlaka nchini humo, alikuwa hatarini.Watalii walikuwa wanampa sigara na pombe ili awafurahishe.
Hifadhi hiyo kwa sasa imeboreshwa na Zakayo anayeitwa 'Babu' wa Sokwe wote nchini Uganda aliweza kuishi kwa raha
Wataalam wa uhifadhi wamemsifu Zakayo kwa kuwa balozi wa sokwe na wanyama wengine nchini Uganda.Wanasema wasifu wake ulisaidia kujipatia fedha kwa juhudi za uhifadhi na kuongeza idadi ya watalii
Mabaki ya Zakayo yatatunzwa kwa ajili ya utafiti na elimu.
Sokwe barani Afrika
Maisha ya Sokwe katika misitu barani Afrika hutegemea miti.
wanasayansi wameeleza hayo kutokana na utafiti walioufanya
utafiti ulibaini kuwepo kwa sokwe wengi kuliko wanyama wengine.
Sokwe katika nchi ya Cameroon,Afrika ya kati na Congo wanakabiliwa na tishio la ujangiliHaki miliki ya pichaEMMA STOKES/WCS
Image captionSokwe katika nchi ya Cameroon,Afrika ya kati na Congo wanakabiliwa na tishio la ujangili
Hata hivyo , wanyama hao wengi wako kwenye maeneo yasiyo na usalama,ambapo huwa hatarini kuuawa na majangili,Ebola na uharibifu wa mazingira
Hali hiyo pia imewakuta sokwe wa kwenye misitu ya nchini Cameroon,Afrika ya kati ,Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Guinea ya Ikweta na Gabon.
Silaha inamaanisha uwindaji: vijidudu inaamisha Ebola:na miti inaashiria kuwa wanyama wanahitaji msitu kuweza kuishi,amesema Dokta Fiona Maisels,Mwanasayansi wa hifadhi kutoka taasisi ya hifadhi ya wanyama.
Ikiwa misitu itakatwa.Ikiwa misitu itabadilishwa na kuwa kwa ajili ya kilimo, hakutakuwa na sokwe.
Kwa mujibu wa jarida la kisayansi, Watafiti wa kimataifa wanasema viumbe wa aina hii wanahitaji uangalizi zaidi ya wanaoupata.
Jitihada za uhifadhi lazima zizingatie kuimarisha hatua za kupiga vita ujangili, hatua za kudhibiti magonjwa na kutunza mazingira, wameeleza.

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 28.04.2018: Je Wenger atakubali kuwa kocha tajiri duniani?

$
0
0


Arsene Wenger
Image captionArsene Wenger
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amepewa fursa kuwa mkufunzi tajiri zaidi duniani iwapo atajiunga na ligi kuu ya China.(Mirror)
Wenger ameombwa kuchukua wadhfa wa meneja mkuu katika klabu ya PSG(Le10 via Talksport)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa kipa David de Gea hataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu.
De Gea 27Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDe Gea 27
De Gea 27 anakamilisha mwaka wake wa mwisho wa kandarasi yake lakini United ina chaguo la kuongeza mwaka mwengine na wanajiandaa kwa mkataba mpya. (Manchester Evening News)
Mshambuiaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 27, anasema kuwa ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu hatma yake ya siku zijazo. Amehusishwa na Barcelona na Manchester United (Sun)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumzuia Mikel Arteta kusalia miongoni mwa makocha wake licha ya raia huyo wa Uhispania kuhusishwa na Arsenal. (Mirror)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumzuia Mikel Arteta kusalia miongoni mwa makocha wake licha ya raia huyo wa Uhispania kuhusishwa na Arsenal. (Mirror)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumzuia Mikel Arteta kusalia miongoni mwa makocha wake licha ya raia huyo wa Uhispania kuhusishwa na Arsenal. (Mirror)
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte huenda akakosa wadfha wa ukufuzi wa timu ya taifa ya Itali. Conte mwenye umri wa miaka 48 anataka mkataba mpya wa miaka mitano lakini shirikisho la soka nchini Itali limekataa kuafiia mahitaji hayo.(Times - subscription only)
Rafael Benitez
Image captionRafael Benitez
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anasema kuwa beki Jamaal Lascelles ni miongoni mwa wachezaji waliopo katika mipango yake ya siku za usoni. Mchezaji huyo amehusishwa na Chelsea pamoja na Liverpool. (Newcastle Chronicle)
Benitez amefungua mazungumzo ya kandarasi mpya na klabu hiyo kupitia washirikishi wake na anatumai kupata suluhu ya haraka ambayo itakuwa nzuri kwa kila mmoja.". (Times)
Eliaquim Mangala
Image captionEliaquim Mangala
Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce hajui iwapo beki wa Ufaransa Eliaquim Mangala ambaye ameichezea klabu hiyo mara mbili atapatiwa kandarasi ya kudumu baada ya kuwasili katika klabu hiyo kwa mkopo kutoka ManCity.(Liverpool Echo)
Maurizio SarriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaurizio Sarri
Mkufunzi wa Napoli Napoli Maurizio Sarri, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Chelsea, ana kipengee katika kandarasi yake kinachomaanisha kwamba anaweza kuondoka kwa dau la £7m iwapo klabu hiyo ya Itali itapokea ombi kabla ya mwisho wa mwezi Mei.(London Evening Standard)
Tottenham ina mwezi mwengine kukamilisha mpangilio wa mechi za msimu ujao huku wakijiandaa kuanza kampeni mpya ya mechi za ugenini.. (London Evening Standard)


KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

$
0
0
KWAHERI!! MTWA Cadre Baba Mhe Ndugu Comrade Abbas Kandoro "MWAGITO"; MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI MYALUKOLO; Tulikuzoea, Tulikupenda, Tuliwiwa na Upendo wako wa dhati katika Kujenga Maisha yetu Kisiasa, Kiuchumi na hata Kijamii; Uliongea kwa Taratibu iliyojaa Tunu ya Busara, Hekima na Upendo!! MTWA Baba Mhe Abbas Kandoro ulichukua Kijiti cha Kulijenga Jiji la Arusha Mwaka, 2006 kutoka kwa Mhe Mohammed Babu, na bado Ukatumikia Utumishi wako kwa Kumpa Kijiti Mhe Samuel Ndomba; Hilo ni Jiji uliliongoza kwa Umahiri Mkubwa Ustahdhi Abbas Kandoro; Ni Mkuu wa Mkoa pekee wa Jiji la Dar-es-salaam aliyeweka heshima kwa Wauzaji wadogowadogo “Matching-guy” katika Mtaa wa Condo na Mitaa mingine katika Jiji la Dar-es-salaam “the house of peace" yaani “Nyumba ya Amani”; Jiji ambalo zamani liliitwa Mzizima; Jiji lililokana katukatu kuitwa "house of war" (Dar al-harb) yaani ‘Nyumba ya Vita”; Sitosahau ulipounda Tume ya Uchunguzi kuchunguza Chanzo cha Kuanguka kwa Jengo lenye ghorofa Kumi hapa jijini lililoanguka Jumamosi ya Tarehe 21 Juni, 2008 alfajiri na kuuwa watu wanne na kujeruhi watu kadhaa na huku mwili wa mtu mmoja ukifukuliwa akiwa amekufa kutoka katika kifusi cha Jengo hilo; Uliwaamini Wajumbe wazito uliowateua akina Mhandisi Joseph Malango kutoka Bodi ya Wakandarasi, Eng(Arch)Elias Mwakalinga kutoka Wizara ya Miundombinu, Luteni Kanali Mkohi Kichogo kutoka Jeshi la Wananchi Wa Tanzania, Mhandisi Dkt Kiguma kutoka Usalama wa Taifa, Ndugu Daniel Mtupa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Ndugu Joseph Ringo kutoka Bodi ya Usanifu wa Majengo, Dkt Paul Ndumbalo kutoka Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam; Hawa wote hakika ni Vichwa vya Uhakika, Hayati wetu wewe!! Hatimaye ukamwachia Jiji hili Mhe William Vangimembe Lukuvi; Utawambia nini Wakazi wa Mwanza, “The Rock City” walivyofaidi Bidii zako za kulifanya Jiji la Mfano Mzee Kandoro wewe!! Ukabeba Majukumu Kuanzia Mwaka, 2009 hadi Mwaka, 2011; Jiji la Mwanza likitamkwa huwezi kuacha kuoanisha na Jina lako Tukufu la Abass Kandoro!!; Ukilichukua Jiji hilo kutoka kwa Mhe Eng Dkt James Msekela na Kumuachia Kijiti Mhe Eng Evarist Ndikilo; Ulichukua kwa Mhandisi ukamwachia Mhandisi, siri anayo Mhe Ndugu Dkt Col Jakaya Halfani Mrisho Kikwete; Kabla ya kupelekwa Mbeya niliipata habari kuwa unaondoka Mwanza; Mimi Handley Mtoto wa Stella!! Sikujua Unaenda Kwetu Mbeya “The Scoland of Africa”, “The Green-City”; Nikakupigia Simu; Mzee naomba Uje kwenye Chama usaidie Dawati la Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi!! Ukanijibu bila Kusita “Mafwenga!! I am not interested to serve in the Party as active politician in advocacy desk, but let me think on your advice”: Mara Ukapelekwa Nyumbani Mbeya………………………….Duu MTWA Comrade Abass Kandoro Umeniliza Mtani wangu: Kwa kweli, sitosahau Ulipolisimamia Jiji la Mbeya, mara Ulipoteuliwa Tarehe 16 Septemba, 2011 na Kuapishwa saa 4.00 Asubuhi katika Viwanja vya Ikulu, kwani moja ya Kitu kilichonigusa ni pale ulipofanya mkutano wa hadhara saa 11.00 alfajiri, katika kituo kikuu cha mabasi Jijini Mbeya uliowahusisha abiria na madereva wa mabasi makubwa; Ulikuwa Mtatuzi wa Kero, Mtatuzi wa Migogoro Mhe Kandoro; Ulitatua Vifo vya ajali hasa pale ulipotoa Takwimu ukisema tangu Januari hadi Tarehe 14/09/2014, kuwa ajali 297 zilitokea na kusababisha vifo vya watu 210 na majeruhi 402; Kwa lugha ya aina yake ya Upole na Ukali wenye Diplomasia ya Kubembeleza ukasema “Madereva, chonde chonde kuweni makini mnapokuwa kwenye usukani, endesheni kwa kufuata sheria na taratibu ili kupunguza ajali zisizo za lazima’’; Sitosahau Program yako ya kutusaidia Tuuze Mazao yetu Dubai, Sisi wana Mbeya! Sisi! sisi! Tulioziea zaidi Biashara ya Ndizi na Mchele; Uliweka kivutio cha Maksudi ukisisitiza umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Songwe!! KIKI BE!! KIKI MWAGITO!! KIKI MTWA? HAYA BWANA!! Aidha, uliwafundisha Mbeya kuheshimu na Kutunza Mazingira ukiwataka Viongozi wa Jiji hilo kuingilia kati kunusuru hali ya uchafu iliyokithiri ndani ya jiji la Mbeya kwa kuwataka Viongozi kusimamia Sheria; Ulipambana na Wizi wa Kutumia Mitandao na hukusita kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) kushirikiana na kampuni za simu za mkononi kudhibiti wimbi la wizi wa Kutumia Mitandao, Baba Ulienda sambamba na Techological changes!!; Hakika ulirinusuru Jiji hilo kuitwa “shamba la bibi,”; Aidha, Hukusita Mnamo Tarehe 17 Machi 2016 Ulipomkabidhi Majukumu Mazito ya Mkowa wa Mbeya Comrade Amosi Makala; Hakika "Medali ya Utumishi Uliotukuka" Uliotuzwa na Mhe Ndugu Dkt Col Jakaya Mrisho Halfani Kikwete imetuachia alama kubwa ya Utumishi na Utawala Bora hapa Nchini; Utawambia nini Wakazi wa Singida leo jinsi ulivyowatumikia? Wasalimie Mtwa Mkwawa! Mtwa Amran Mayagila! Mtwa Peter Mgongolwa Siyovelwa! na wengine wengi waliotangulia Mbeleza za Haki: "Inna lillaahi wa inna ilayhi Raaji'oon" MTWA CADRE NDUGU MHE COMRADE ABASS KANDORO (Prof (Dr) Comrade Handley Mpoki Mafwenga Simba Mwai-Holler Nkulu Gwa Kipanga “MUNDU GWA JESU”)
Image may contain: 3 people, people sitting
LikeShow more reactions
Comment

Stormy Daniels amshtaki Trump juu ya ujumbe wa Twitter

$
0
0


Trump at press conferenceHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels amemshtaki Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu ujumbe wa Twitter anaodai ni wa kumharibia jina, wakili wake amesema.
Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, anasema alitishiwa na mwanamume mmoja katika maegesho ya magari mjini Las Vegas na kutakiwa kuacha kuendelea na madai yake kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw Trump.
Rais huyo wa Marekani alipakia kwenye Twitter mchoro wa mwanamume mshukiwa na kisha kuandika "hii ni kazi ya utapeli kabisa".
Wakili wa Bi Daniel aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Trump "anafahamu vyema kabisa yaliyotokea".
"Bw Trump alitumia fursa ya mamilioni ya watu katika taifa hili na kimataifa (wanaomfuatilia katika mtandao huo wa kijamii) kutoa taarifa ya uongo yenye lengo la kumshushia hadhi na kumshambulia Bi Clifford," kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya dola mjini New York inasema.
Stormy Daniels, seen here with her lawyer Michael Avenatti, outside a federal court in Manhattan talking to reportersHaki miliki ya pichaAFP
Image captionStormy Daniels akiwa na wakili wake Michael Avenatti
Kesi hiyo inasema ujumbe huo wa rais ulikuwa wa kumharibia mtu jina kwani ulimtuhumu Bi Daniels kwa "kutekeleza kosa kubwa" - hususan, la kumtuhumu mtu mwingine kwamba alimtishia.
Bw Trump alikuwa amepakia mtandaoni mapema mwezi huu picha ya mchoro wa mshukiwa huyo na kumweleza kuwa "mwanamume asiyekuwepo".
Bi Daniels anasema yeye na rais huyo walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kuanzia 2006.
Bw Trump amekanusha tuhuma hizo.
Mwanamke huyo aliambia kipindi cha CBS News kwamba baada ya kutamatika kwa uhusiano wao, mwanamume mmoja alifika alipokuwa yeye na binti yake katika maegesho hayo ya magari Las Vegas na kumwambia "sahau taarifa hiyo, mwache Donald Trump".
Bi Daniels awali alimshtaki wakili wa Bw Trump, Michael Cohen, akitaka kuvunjwa kwa mkataba wa kutofichua siri kuhusu uhusiano huo, ambao anasema Bw Trump hakuutia saini.
Bw Cohen awali alikiri kwamba alimpa Bi Daniels $130,000 zake mwenyewe, lakini alisema kwamba hakueleza ni kwa nini alitoa pesa hizo.
Michael Cohen photographed as he arrives at the US Courthouse in New York on April 26, 2018Haki miliki ya pichaAFP
Image captionTrump amekana kuwa na ufahamu wowote kumhusu Cohen ambaye hapa anaonekana akiingia mahakamani
Kesi hiyo hata hivyo ilisitishwa kwa siku 90, huku jaji akisema kwamba haki za Bw Cohen zingekuwa hatarini iwapo kesi hiyo ingeendelea akiwa bado anachunguzwa.
Bw Cohen anachunguzwa na Mwanamashtaka Maalum Robert Mueller kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 na kwamba taifa hilo lilishirikiana na maafisa wa kampeni wa Rais Trump.

Magufuli: Wapuuzeni wanaodai serikali ya Tanzania inakopa sana

$
0
0


Magufuli akizungumza na wananchi katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Aprili 29,2018.Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionMagufuli akizungumza na wananchi katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma Jumapili
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka raia nchini humo kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa sana.
Kiongozi huyo alisema mikopo inayochukuliwa na taifa hilo ina manufaa na itachochea ukuaji wa uchumi.
Dkt Magufuli alikuwa akihutubu alipokuwa anaifungua rasmi barabara ya lami ya Iringa - Migoli - Fufu yenye urefu wa kilometa 189.
Barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma na Barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya kuanzia Cape Town nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri (The Great North Road).
Ujenzi wa barabara hiyo uligharimu Shilingi Bilioni 207.457 ikiwa ni ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa asilimia 65.9, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa asilimia 21.3.
Serikali ya Tanzania ilitoa asilimia 12.8.
Tanzania imekuwa ikikopa kutoka kwa mashirika ya kimataifa kufadhili miradi mingi ya miundo mbinu ikiwemo miradi ya barabara na reli.
Ripoti ya mwaka wa kifedha wa 2016/2017 ripoti ya Bank Kuu ya Tanzania inaonesha deni la taifa hilo limefikia Dola 23.78 bilioni (zaidi ya Sh52.29 trilioni).
Deni hilo liliongezeka kwa asilimia 9.1 katika mwaka huo ulianza Juni 2016.
Hata hivyo, serikali imesisitiza kwamba kiwango hicho cha deni badi hakijapita kiwango kinachokubalika kimataifa.
Deni hilo ni sawa na asilimia 48.9 ya pato la Taifa, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya BOT.
Deni Tanzania
Sehemu kubwa ya deni hilo ni kutoka kwa wakopeshaji wa nje ambao wameikopesha Tanzania dola za Marekani bilioni 18.5.
Kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 8.9 ukilinganisha na kiwango cha deni mwaka uliodangulia ambapo deni lilikuwa dola za Marekani bilioni 16.4.
Baadhi ya wachanganuzi wameikosoa hatua ya serikali kukopa kiasi kikubwa cha fedha lakini Dkt Magufuli amesema hakufai kuwa na wasiwasi wowote.
Akihutubu Iringa, Rais huyo alisema na fedha hizo hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa muda mrefu, na kwamba ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kuchochea uchumi.
Wakati wa kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, kiongozi huyo alieleza matumaini kwamba uchumi wa Tanzania utatengemaa.
"Taifa letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 4," alisema.
Baadaye alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinumwi Adesina.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ilisema Dkt Adesina alimpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuimarisha uchumi wa Tanzania na kusema wamejadiliana mambo kadhaa yakiwemo namna benki hiyo ilivyosaidia juhudi za maendeleo za Tanzania tangu mwaka 1971 na inavyoendelea kusaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alitaja baadhi ya maeneo ambayo AfDB itatoa ufadhili kuwa ni uzalishaji na usambazaji wa nishati, uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Jiji la Dodoma hasa barabara.
"Yote kwa yote nimemhakikishia Rais Magufuli kuwa AfDB itamuunga mkono katika mipango yake na maono yake ili tuweze kuisaidia Tanzania kukua zaidi, nimefurahi kuzungumza na Mhe. Rais na naona Tanzania ipo katika njia sahihi," alisema Dkt Adesina kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ikulu.
Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, AfDB imefadhili miradi ya maendeleo yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.457 (sawa na Shilingi Trilioni 7.78 Tanzania) zikiwemo fedha za miradi 25 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2017 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.986 (Shilingi Trilioni 4.47 Kitanzania).

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 01.05.2018: Jack Wilshere, Gareth Bale, Joe Hart na Santi Cazorla

$
0
0


Jack Wilshere kujiunga na Bournemouth
Arsenal wameimarisha ofa yao kwa kiungo wa kati Jack Wilshere. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 26 unafikia kikomo mwisho wa msimu na amekuwa akitafutwa na Wolves na Everton. (Mirror)
Mchezaji anayesakwa sana na Liverpool Max Meyer hatachezea tena Schalke baada yake kufukuzwa kutoka mazoezini na kutoka kwenye kikosi cha kwanza. Meyer, mshambuliaji mwenye miaka 22, aliadhibiwa baada yake kumkosoa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Bundesliga Christian Heidel. (Sky Sports)
Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema Gareth Bale, 28, anataka kusalia Bernabeu licha ya tetesi kwamba huenda mshambuliaji huyo wa Wales akahama. (Sun)
Pep Guardiola amesema uamuzi ufaao utafanywa kuhusu kipa wa Manchester City Joe Hart iwapo West Ham wataamua kutobadilisha mkataba wake wa sasa wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu. (Mirror)
Marouane Fellaini, 30, anataka Manchester United wampe mkataba wa muda mrefu zaidi kushinda mwaka mmoja ambao wamemuahidi kwa sasa Old Trafford. (ESPN)
Gareth BaleHaki miliki ya pichaHUW EVANS PICTURE AGENCY
Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla anatumai kwamba ataweza kurejea kucheza kabla ya mwisho wa msimu. Mhispania huyo mwenye miaka 33 hajachezea Gunners tangu mwaka 2016 kutokana na jeraha la mguuni ambalo limekosa kupona. (AS)
Meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca amekataa ofas kutoka kwa Everton baada ya kuanza kuangazia kumrithi Arsene Wenger Arsenal, kwa mujibu wa mwanahabari Guillem Balague. (Express)
Thierry Henry na Tony Adams ni miongoni mwa watu mashuhuri 100 wa Arsenal ambao wamealikwa kwa mechi ya mwisho ya Wenger nyumbani, ambapo watasherehekea miaka 22 ya Mfaransa huyo katika klabu hiyo. (Mail)
Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 29, alifukuzwa kutoka mazoezini Jumatatu na meneja wa klabu hiyo David Moyes baada ya wawili hao kukorofishana. Klabu hiyo inatarajiwa kuanza uchunguzi kuhusu kisa hicho. (Telegraph)
Andy CarrollHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wolves ambao wamepanda daraja kucheza Ligi ya Premia watakuwa wanamtaka kipa wa Stoke Jack Butland iwapo klabu yake itashushwa daraja. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa miaka 25 pia anatafutwa na Liverpool na West Ham. (Express)
Beki wa Manchester United Ashley Young amesema atasikitika sana kuhusu msimu huu hata kama watafanikiwa kushinda Kombe la FA. (ESPN)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe amevunjwa moyo na uchezaji wa klabu hiyo karibuni, huku wakiwa wamecheza mechi tano sasa bila ushindi. (Bournemouth Daily Echo)
Sunderland wanamtaka straika wa zamani Kevin Phillips, 44, awe meneja wao baada ya kuondoka kwa Chris Coleman kufuatia kushushwa daraja kwa klabu hiyo hadi League One. Phillips, aliyefunga mabao 116 katika mechi 210 ligini akichezea klabu hiyo kwa sasa ni mkufunzi Derby. (Sun)
Meneja wa Everton Ronald Koeman amesema amesikitishwa na mchezaji Davy Klaassen waliyemnunua mwanzo wa msimu. Nahodha huyo wa zamani wa Ajax ameshindwa kuvuma katika soka England. Mholanzi huyo Klaassen, 25, amewachezea mechi 14 pekee msimu huu. (Liverpool Echo)
Davy KlaassenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Winga wa Watford Gerard Deulofeu, kwenye Twitter, alishangazwa na hatua ya kuachwa kwa jina lake kwenye jezi ya Barcelona ya kusherehekea kushinda ligi. Mhispania huyo wa miaka 24 yupo Watford kwa mkopo lakini alichezea Barca mechi 10 kabla ya kuhamia England. (Mail)
Kipa wa Penarol Kevin Dawson alilazimika kuomba jezi kutoka kwa shabiki baada yake kusahau jezi yake nyumbani kabla ya klabu yake kucheza dhidi ya Progreso katika ligi kuu ya Uruguay, Primera Division. (Mail)

Bora kutoka Jumatatu

Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema washambuliaji wake Gareth Bale, 28, na Karim Benzema, 30, "watasalia" katika klabu hiyo licha ya tetesi kudokeza kwamba huenda wakahama. (Star)
Meneja wa Arsenal anayeondoka Arsene Wenger atachukua "miezi minne hadi mitano" kuamua kuhusu mustakabali wake. (London Evening Standard)
Meneja msaidizi wa Liverpool Zeljko Buvac ameihama klabu hiyo baada ya kuzozana na meneja wa sasa Jurgen Klopp. (Daily Record)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema City hawatasaini wachezaji zaidi ya wawili mwisho wa msimu. (Manchester Evening News)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana wasiwasi kwamba huenda mshambuliaji wake Romelu Lukaku, 24, asiweze kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea baada yake kuumia mguuni akicheza dhidi ya Arsenal Jumapili. (Times )
Meneja wa Leicester City Claude Puel amesema pengine wachezaji wameanza kuleweshwa na Kombe la Dunia au mambo mengine baada ya uchezaji wa timu yake kudorora. Walichapwa 5-0 na Crystal Palace. (Guardian)

Fahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa

$
0
0


Nchi nyingi barani Afrika ni kinyume cha sheria kulima, kuuza au kutumia bangiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNchi nyingi barani Afrika ni kinyume cha sheria kulima, kuuza au kutumia bangi
Lesotho
Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.
Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.
Afrika Kusini
Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa.
Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi, vivyo hivyo kwa makampuni kutengeneza bidhaa zitokanazo na bangi na mawakala kusambaza bidhaa.
katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma, wale walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha bangi wameleta maendeleo makubwa kufungua milango katika uzalishaji wa bangi kwa ajili ya dawa.
Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi
Ghana
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .
kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.
Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.
pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.
Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.
wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.
Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.

Forbes: Trump ashuka orodha ya matajiri duniani 2018

$
0
0


Donald TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Rais wa Marekani Donald Trump ameshuka nafasi 222 katika orodha ya kila mwaka ya watu tajiri zaidi duniani ambayo hutolewa na jarida la Forbes.
Mali yake imeshuka thamani kutoka $3.5bn (£2.5bn) hadi $3.1bn.
Jarida hilo limesema kushuka kwa utajiri wa Trump kumetokana zaidi na kushuka kwa thamani ya nyumba na vipande vya ardhi New York na pia kushuka kwa mapato kutoka kwa viwanja vyake vya kuchezewa mchezo wa gofu.
Anayeongoza orodha ya matajiri wa kupindukia ni mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos.
Utajiri wa Bezos umepanda na kufikia $112bn kutoka takriban $39.2bn mwaka jana.
Kuimarika kwa utajiri wa Bw Bezos ndiko kwa juu zaidi katika historia.
Amemuondoa mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kutoka uongozini kwenye orodha hiyo.
Utajiri wa Gates unakadiriwa kuwa $90bn mwaka huu kutoka $86bn, na ndiye anayeshikilia nafasi ya pili.
Bw Gates ameongoza orodha hiyo kwa miaka 18 kati ya miaka 24 iliyopita.
Forbes wanasema kuna mabilionea 2,208 (kwa kutumia dola za Marekani) ambao walishirikishwa katika orodha ya 32 ya kila mwaka ya jarida hilo.
Matajiri hao kwa pamoja wana utajiri wa $9.1 milioni.
Miongoni mwao, kuna mabilionea 259 wapya ambao walijipatia utajiri wao kutoka wka biashara za aina nyingi zikiwemo nguo za harusi, wanasesere wa kuchezewa na watoto na magari yanayotumia umeme.
Mwekezaji mmarekani Warren Buffett ndiye wa tatu utajiri wake ukiwa $84bn. Utajiri wake umepanda kutoka $75.6bn mwaka uliotangulia.
mtu tajiri zaidi Ulaya ndiye wa nne kwenye orodha hiyo, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya bidhaa za kifahari ya LVMH, Bernard Arnault, ambaye utajiri wake ni $72bn.
Matajiri
'Kupanua pengo'
Marekani ndiyo nchi iliyo na mabilionea wengi duniani, ambapo ina mabilionea 585, ikifuatwa na China. Jimbo la California pekee lina mabilionea 144, zaidi kushinda mataifa yote isipokuwa Marekani na China.
Ujerumani ndiyo nchi inayoongoza Ulaya ikiwa na mabilionea 123.
India ina mabilionea 119 nayo Urusi mabilionea 102.
Kuna mabilionea 53 kutoka Uingereza kwa mujibu wa Forbes na idadi hiyo imeshuka kutoka 54 mwaka 2017.
Luisa Kroll na Kerry Dolan kutoka kwa Forbes Media alisema: "Watu matajiri kupindukia wanazidi kupanua mwanya kati yao wenyewe, na pia kati yao na watu wengine."
Orodha ya mabilionea ya Forbes inatumia takwimu za kufikia Februari 9, 2018.
Jarida hilo hutumia bei ya soko la hisa na ubadilishanaji wa fedha za kigeni ya siku hiyo kutoka kila pembe duniani kuandaa orodha hiyo.

Davido afanya kufuru kwenye birthday ya mpenzi wake

$
0
0


Staa wa muziki kutokea Nigeria Davido amechukua headlines katika mitandao ya kijamii baada ya kumzawadia mpenzi wake Chioma gari aina ya Porshe yenye gharama zaidi ya Shillingi Millioni 200 za Kitanzania katika siku yake ya kuzaliwa ambapo sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wengi wakiwemo mastaa mbalimbali 
Davido pia amemzawadia mpenzi wake wimbo ambao ameutunga kwa ajilli yake unaoitwa “Assurance” ambapo pia ndio plate namba ya gari hilo alilozawadiwa Chiomakatika siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 23 iliyofanyika jana April 30,2018 Lagos Nigeria.
Billnas aongelea ishu ya kuoa mwakani

LIVE: JPM KWENYE MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI – IRINGA

$
0
0



Rais Magufuli ni miongoni mwa viongozi wa Kitaifa waliowasili uwanja wa Samora, Iringa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi. TAZAMA LIVE KWA KUBONYEZA PLA HAPA CHINI
MAGAZETI LIVE: Mabilioni yayeyuka, Lissu Nimesahau kutembea, Kigezo kipya Mikopo Vyuo Vikuu


JUMUIYA YA KIJANI TANZANIA YAANZA KWA KISHINDO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Kijani Tanzania (TGA), Abraham Nyantory akielezea umuhimu wa jumuiya hiyo katika kuwaendeleza wakulima nchini, wakati wa mkutano wa kukiridhia chama hicho kinachotarajiwa kusajiria hivi karibuni.

Mkutano huo uliowashirikisha wanachama wa Mtandao waKijani Kibichi Tanzania (Mkikita) na wasio wanachama, lengo lake lilikuwa ni kutangaza fursa za kujiunga nacho, Hatma ya uanachama wa Mkikita na kuelezea umuhimu wa shamba la umiliki wa pamoja la  Kiwangwa lenye jumala ya heka  250.Heka moja inauzwa sh. mil 1 na kukodi kwa mwaka sh 500,000.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea jinsi ndoto yake ya kuanzisha TGA ilivyotimia na kuwaomba wanachama kuchangamkia kujiunga na chama hicho ili kusonga mbele katika maendeleo ya kilimo biashara.

"Safari yangu na Mkikita leo (jana) imeandika historia mpya kujenga misingi ya mageuzi toka kilimo njaa au kilimo uti wa mgongo kwenda kilimo uwekezaji au kilimo hisa kupitia kilimo biashara," amesema Adam na kuongeza kuwa 

TGA ni njia sahihi kumilikisha huduma kwa wanachama wa Mkikita ili kuvutia mitaji na uwekezaji  wa ndani na nje kwa ajili ya kuyakamata masoko ya ndani na nje ya nchini.

Mikutano kama huo imepangwa kufanyika pia siku zijazo  katika mikoa ya TAanga, Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma, Lindi, Mtwara , Songwe na Ruvuma. 
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA; 0715264202,0689425467
 Wana TGA wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Mkikita.
 Wakisikiliza kwa makini
 Baadhi ya maofisa wa Mkikita Makao Makuu wakiwa katika mkutano huo.
 Mambo yamenoga

 Ni furaha iliyoje
 Wakisikiliza kwa makini maendeleo ya mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Anatoglo, Mnazi Mmoja, Dar
 Wadau wakichangia hoja za kuiboresha TGA


 Mkurugenzi wa Masoko wa Mkikita, Deo Liganga akifafanua sababu za kuanzisha TGA.
 Mkurugenzi wa Mashamba wa Mkikita, Catherine Ndamgoba  akihangia hoja.
 Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema Ngowi akielezea taratibu za kujiunga TGA na ununuzi a shamba la Kiwangwa
 Mdau akiuliza swali jinsi ya kujiunga TGA
Adam akionesha moja ya vitabu vinavyotumika kumuendeleza mkulima kuingia kwenye mpango wa kilimo biashara.

MKIKITA YATOA MSAADA KILO 1700 ZA UNGA WA MUHOGO KWA KITUO CHA YATIMA CHA HOCET

$
0
0

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Dk. Kissui Steven Kissui (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha HOCET, Hezekia Mwalugaja mfuko wa unga wa muhogo ikiwa ni sehemu ya tani 1.7 za unga huo unaozalishwa na Mkikita. Unga huo una thamani ya sh. mil. 3.3. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ya Mkikita, Dar es Salaam.Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange na baadhi ya Yatima wanaosomeshwa na kituo hicho kwenye shule. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;0715264202,0689425467
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Dk. Kissui Steven Kissui (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha HOCET, Hezekia Mwalugaja mfuko wa unga wa muhogo ikiwa ni sehemu ya tani 1.7 za unga huo unaozalishwa na Mkikita. Unga huo una thamani ya sh. mil. 3.3. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ya Mkikita, Dar es Salaam.
 Mwalugaja akiwashukuru Adama Ngamange na Dk. Kissui kwa msaada huo.
 Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema Ngowi akielezea sababu zilizoifanya Mkikita kutoa msaada huo, ikiwemo kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kuanza kuzalisha unga huo.
 Ngamange akiwa na baadhi ya Yatima wa Kituo cha Hocet ambao pia waliimba wimbo wa kuishukuru Mkikita kwa msaada huo.
 Baadhi ya maofisa wa Mkikita
 Hamida Shabaan wa Hocet akitoa shukrani kwa niaba ya yatima wenzie
Baadhi ya maofisa wa Mkikita wakiwa na jamii ya Hocet

Donald Trump alijitungia barua kuhusu afya yake, daktari Harold Bornstein asema

$
0
0


US President Donald Trump at the White House in Washington DC, 1 May 2018Haki miliki ya pichaEPA
Aliyekuwa daktari wa Donald Trump amesema kwamba si yeye aliyeiandika barua iliyomweleza mgombea huyo wa chama cha Republican wakati huo kuwa aliyekuwa na "afya nzuri ajabu", vyombo vya habari Marekani vinasema.
"[Trump] alitunga na kuamrisha kuandika kwa barua yote," Harold Bornstein aliambia runinga ya CNN Jumanne.
Ikulu ya White House haijazungumzia tuhuma hizo za daktari huyo.
Bw Bornstein pia amesema maafisa wa serikali walitekeleza "uvamizi" katika afisi zake Februari 2017 na kuondoa nyaraka zote zilizohusiana na taarifa za kimatibabu za Bw Trump.
Katika mahojiano na CNN, Bw Bornstein amesema barua hiyo ya mwaka 2015 iliyodokeza kwamba Bw Trump angekuwa "mtu mwenye afya bora zaidi aliyewahi kuchaguliwa kuwa rais" haikuwa utathmini wake wa kitaalamu wa hali yake ya afya.
"Nilitayarisha nilipokuwa nasonga," anasema.
Haijabainika ni kwa nini Bw Bornstein anatoa tuhuma hizo kwa sasa.
Presentational white space
Barua hiyo ilisema nini?
Barua hiyo ilikuwa na miongoni mwa mengine tamko kuhusu nguvu za kimwili za Bw Trump na ukakamavu wake, ambavyo vilielezwa kuwa "vya kipekee".
Vipimo kuhusu shinikizo la damu yake na pia uchunguzi mwingine wa maabara vilielezwa kuwa "vya kushangaza kwa uzuri wake" na kwamba alikuwa amepoteza uzani wa kilo 7 katika kipindi cha mwaka mmoja.
Barua hiyo iliongeza kwamba Bw Trump hakuwa na aina yoyote ya saratani na hajawahi kufanyia upasuaji wowote wa maungo.
Wiki kadha kabla ya kutolewa kwake, Bw Trump alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba barua ya kimatibabu ya Bw Bornstein ingeonesha hana kasoro.
Nakala ya barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na Bw BernsteinHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionNakala ya barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na Bw Bernstein
"Nina bahati sana kwamba nilibarikiwa na vinasaba vizuri sana," Bw Trump, ambaye ndiye mtu aliyechaguliwa kuwa rais akiwa na umri mkubwa zaidi Marekani, aliandika kwenye Facebook wakati huo.
Januari mwaka huu, Bw Trump alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu ambao ulidumu saa tatu kuhusu afya yake ya kiakili.
Daktari wake wa White House Ronny Jackson alisema wakati huo kwamba: "Sina wasiwasi wowote kuhusu uwezo wake wa kufahamu, kufikiria na kuelewa mambo."

Uvamizi wa afisi ya Bornstein ulihusu nini?

Daktari huyo mwenye makao yake New York City anasema walinzi wa kibinafsi wa Bw Trump walifika katika afisi zake New York wakiandamana na wanaume wengine wawili mnamo tarehe 3 Februari 2017.
"Walikaa hapa kwa dakika 25 au 30 hivi, walizua vurugu sana," Bornstein aliambia NBC News, na kuongeza kwamba kisa hicho kilimfanya kujihisi kama "aliyebakwa, kuwa na hofu sana na masikitiko na huzuni."
Anasema nakala halisi ambayo ndiyo pekee aliyokuwa nayo ya rekodi ya afya ya Trump, ikiwa ni pamoja na ripoti za uchunguzi wa maabara, vyote vilitwaliwa na walinzi hao wa Trump.
Kisa hicho kilitokea muda mfupi baada ya gazeti la The New York Times kuchapisha taarifa ambapo Bw Bornstein alisema alikuwa amempendekezea Trump danywe dawa ya Propecia, ambayo ni ya kuzuia upara.
Afisa wa habari wa White House Sarah Sanders baadaye alisisitiza kwamba kisa hicho hakikuwa uvamizi bali lilikuwa tukio la kawaida kwa kitengo cha matibabu cha ikulu ya White House kuchukua umiliki wa nyaraka zote za kimatibabu za rais wa Marekani.

Odinga awataka wafuasi waache kususia bidhaa za kampuni nne Kenya

$
0
0


Kinara wa Muungano wa upinzani Kenya Raila OdingaHaki miliki ya pichaAFP
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amewaambia wafuasi wake wasitishe kampeni ya kususia bidhaa na biashara za kampuni zilizohusishwa kuwa na uhusiano na chama tawala nchini Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta.
Safaricom, kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu nchini na Brookside, ambayo ni kampuni ya kutengeneza bidhaa kama maziwa na siagi nimiongoni mwa kampuni zilizolengwa.
Bwana Odinga alitoa tamko hilo leo katika sikuukuu ya Mei mosi au 'Leba dei' katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguziHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWafuasi wa upinzani nchini Kenya
'Tulikuwa na hasira nyingi kwa yale makampuni yaliokuwa yanaunga mkono serikali ya Jubilee. Tukasema safaricom, Brookside, Bidco na tukaongeza Haco, tulisema ni makampuni ambayo yanatesa watu wetu, ambayo yamekataa kukubali uamuzi wa wananchi na tukasema watu wetu wote wasusie bidhaa za kampuni hizo.
'Sasa tumeshikana mkono na Uhuru, tumekubaliana kufanya kazi pamoja tusulishe mambo, na tumeweka sasa kamati ya ushauri ya kuleta suluhu ya kudumu. Kwa hiyo leo hii tunatangaza tunatoa ile amri ya kususia'. Alitangaza Raila Odinga mbele ya umati wa watu waliokusanyika katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi kwa sherehe hizo za Mei Mosi.
Ruto: Tuko tayari kuzungumza na Odinga

Kampuni ambazo Nasa ilisema wafuasi wake izisusie ni:

•Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, ambayo ndiyo tajiri zaidi miongoni mwa kampuni za Kenya
•Kampuni ya maziwa ya Brookside, inayomilikiwa na familia ya Kenyatta
•Kampuni ya kutengeneza mafuta ya kupikia na sabuni ya Bidco
•Kampuni ya Haco inatengeneza na kusambaza bidhaa za urembo, na za usafi wa nyumba nchini Kenya, Uganda, na Tanzania
Muungano wa upinzani Nasa uliyaorodhesha makampuni hayo kwa kile ilichokitaja kuunga mkono utawala usio halali uliomnyima Raila ushindi katika uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Image captionRais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Mnamo mwezi Machi mwaka huu kiongozi huyo mkongwe wa kisiasa Kenya alipatana na rais Uhuru Kenyatta na viongozi hao wawili kwa sasa wanashirkiana katika 'kujenga madaraja'.
Tangazo hilo la kususia bidhaa za wanaotajwa kuwa washirika wa chama tawala lilitolewa mnamo Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na mzozo ulioshuhudia Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika na ye nne pekee duniani kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais.
Raila Odinga amesema maafikiano yake na Uhuru Kenyatta yalioidhinishwa kwa kusalimiana kwa mikono viongozi hao wawili mnamo Machi 9, yamechangia amani na kuruhusu Wakenya kuendelea.
Tangazo la leo litaonekana kama mfano mwingine wa kupatana na kurudi kwa uhusiano mwema baina ya viongozi wawili.

Facebook kuanzisha programu ya kuwapatanisha wapendanao, huku ikiimarisha kiwango cha faragha

$
0
0


Zuckerberg ameahidi tatizo hilo kutokujitokeza tena
Image captionZuckerberg ameahidi tatizo hilo kutokujitokeza tena
Kampuni ya facebook inaongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya ulichokitafuta katika mtandao huo wa kijamii.
Aidha amesema kwamba programu hiyo itaangazia uhusiano wa muda mrefu na sio urafiki wa muda mfupi na itawatenganisha marafiki na watu wanaotarajiwa kuwa na uhusiano.
''Programu hii itakuwa na kiwango cha juu cha siri na usalama kutoka mwanzo'', aliongeza.
Hivi karibuni kampuni hiyo ilikumbwa na kashfa ya kutothamini faragha za watumiaje wake huku watumiaji zaidi ya millioni hamsini walidukuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani.
Facebook imekua katika sakata la faragha ya watumiaje hivi karibuni, mamilioni ya taarifa za watumiaji zilichukuliwa bila ridhaa na kampuni ya Cambridge Analytical kwa matumizi ya wanasiasa.
Mark Zuckerberg amesema kuwa atahakikisha suala kama hilo halitajitokeza tena, kwa kutengeneza ulinzi zaidi wa mtandao huo.
Sakata hilo lilishusha mapato ya Facebook kwa asilimia 15
Image captionSakata hilo lilishusha mapato ya Facebook kwa asilimia 15
''Kilichotokea kwa Cambridge Analytica ilikua uvunjifu wa uaminifu wa hali ya juu, walichukua data za watu na kuziuza, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa suala hili halitokei tena, kwanza tunaweka vizuizi kwa data ambapo mtu atakua anaombwa kwa ridhaa yake, na pili tunahakikisha tunazijua program mbaya zote zilizo'' alisema Zuckerberg.
Katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo ya mjini California, Zuckerberg emeongeza pia wanaimarisha faragha ambapo itamruhusu mtumiaji kufuta historia ya kitu alichotafuta.
Viewing all 21579 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>