Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21839 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Na Hamza Temba, Dodoma
..........................................................

Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic Affairs-SECO.


Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza  ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.


"Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la  Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.


Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 ambapo jumla ya Dola za Kimarekani milioni 3.5 zilitumika.


"Awamu ya pili ya mradi ilianza kutekelezwa mwaka 2017 na utarajiwa kukamilika mwaka huu 2018. Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimetumika katika awamu hii ya mradi" alisema.


Alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuhifadhi mazingira, na kufanya utafiti wa mazao mbalimbali ya utalii ambao utawezesha kuandaa Sera na Mikakati mipya ya kukuza Utalii hapa nchini.


Warsha hiyo ya siku moja imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja  iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Naibu Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii akichangia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo na kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsious Mdamu akitambulisha wajumbe wa meza kuu wakati wa warsha hiyo.
 Wajumbe wa Meza Kuu.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
 Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Warsha ikiwa inaendelea.
Baadhi ya washiriki na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

WAZIRI UMMY AMTAKA DED TANGA KUTENGA ENEO KWA AJILI YA TAASISI YA GIFT OF HOPE INAYOSIMAMIA KITUO CHA SOBBER HOUSE

$
0
0


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akimkabidhi pikipiki Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House cha Gift of Hope kilichopo Kange Jijini Tanga Saidi Bandawe kwa ajili ya kuitumia kwenye matumizi yao


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi ambao waliambatana nae ikiwemo vijana matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutenga eneo la hekari 10 kwa ajili ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Gift of Hope Foundation ambayo inasimamia kituo cha Sober House.

Hayo ameyazungumza alipotembelea kituo hicho kinachow asaidiawaat hirika wa madawa ya kulevya kilichopo eneo la Kange kata ya Maweniambapo alikabidhi pikipiki 1 kwa ajili ya kituo hicho.

Waziri Ummy alisema jambo linalofanywa na taasisi hi yo lazima liungwe mkono na Serikali kutokana na jitihada zao za kukabiliana na mapambanoya matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa waathirika.

Alisema nguvu kubwa inatumiwa na waanzishaji wa nyumba hizo kwa lengola kusaidia vijana huku wakikosa msaada wa kudumu wa kuwawezeshawaweze kujitegemea tofauti na ilivyo sasa wanavyoishi kwa kuomba misaada.

“Jambo linalofanywa hapa sobber house ni juhudi kubwa na lazima sis ikama serikali tuwaunge mkono hawa watu wakishindwa makundi haya kama yatarudi mitaani hali inaweza kuwa mbaya zaidi”Alisema.

Aidha alisema kufuatia taarifa ya taasisi hiyo ya kuhitaji eneo la
kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,shughuli za mikono ikiwamou fugaji,kilimo cha mbogamboga na hata ufundi ni jambo la msingi naviongozi wote wanatakiwa walione kwa jicho la tatu.

“Jamani hawa watu wasiishi kw a kuombaomba lazima wapatiwe eneo lao na waanzishe miradi yao itakayowasaidia kujikimu na mahitaji ya kila sikuna tukifanya hivi tutaokoa kundi kubwa la vijana linaloangamia sikihadi siku”Alisema Waziri Ummy.

Mbali na hilo alisema akiwa kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha dawa za Methadol zinafika Moani hapa kama ilivyo katika mikoa mingine ili kuweza kuwasaidia vijana hao kupunguza makali ya madawa.

“Kwanza nashangaa kama tanga haipati dawa hizi za methadol ikiwa ni mkoa wa pili baada ya dare s salaam kwa wingi wa watumiaji wa mada ninayo dhaama na dawa hazi zitafika sasa kwa ajili ya vijanawetu”Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo Said Bandawe alisema kwasasa wanaishi katika nyumba ya kupanga na wamepewa eneo na wamepewa eneo la mtu kwa kuazimwa kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga nashughuli za ufugaji.

Alisema maisha ya vijana  bado magumu hasa swala la chakula,malazi,dawa za Methadol, na namna ya kupata mahitaji ya kila siku kwa ujumla huku akijaribu kutafuta mahitaji kwa kuomba misaada kuwasaidia vijana haowanaokadiriwa kufikia 68 (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Kampuni ya Pennyroyal Kupitia Mradi Wake wa Best of Zanzibar Kwa Kushirikiana na Internalional Volunteers Oman Yakabidhi Viti na Meza Kwa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Zanzibar.

$
0
0


Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti 205 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na  International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti 205,Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal, kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na  International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja

Mkurungezi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Bi. Safia Rijal akikabidhi moja ya meza na viti kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi za Kijiji cha Kijini Maatemwe na Wawakilishi wa International Volunteers Oman Hemed Mohammad, Danny Kim na Nahya Khamis wa Mradi wa Best Of Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A, Unguja.
Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson akiwa na Mwakilishi wa Internalional Volunteers Oman Danny Kim, wamekali meza na viti walivyokabidhi kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja, kulia Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalazi Bi, Safi Rijal na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kijini Matemwe Mwalimu Ulimwengu Mkadam. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Kijini.
Mwakilishi wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar Mohammed Issa akitowa maelezo kabla ya hafla ya makabidhiano wa vifaa kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini  "A" Unguja.
Mwakilishi wa International Volunteers Oman Danny Kim akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205, kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja Skuli hizo zinapata ufadhili kupitia Mradi wa Bset of  Zanzibar, uliooko chini ya Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar, inayojenga kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar. 
Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibar B. Safia Rijal akizungumza wakati wa hafla hiyoya kukabidhiwa Viti na Meza 205 kutoka kwa Mradi wa Best of Zanzibar kwa kushirikiana na Internalional Volunteers Oman, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.na kuhudhuriwa na Wananchi wa kijiji hicho. 
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekongari na Msini Kijini Matemwe Mwalimu Ulimwengu Mkadam akitowa neno la shukrani kwa msaada huo na kusema umefika wakati muwafaka.
Wazee wa Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Meza na Viti vyake 205 kwa ajili ya matumizi ya Skuli ya Sekondari na Msini Kijini Matemwe, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Kijini. 



Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson, akiwasalimia Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kijini baada ya hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na  International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja


Pennyroyal Limited kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar wakishirikiana na International Volunteers kutoka Oman wametoa msaada wa madawati 200 yenye thamani ya Tsh 18,000,000/- ( Shilingi millioni kumi na nane).
Akiongea katika sherehe za kukabidhiana, Mkurungezi Mkuu Bw. Brian Thomson alikua na haya ya kusema:

“Best of Zanzibar imejitolea kuboresha elimu katika shule za Kijini na Mbuyu Tende. Tumejiwekeza katika progamu tofauti za kielimu katika shule hizi mbili zikiwemu Masomo ya ziada (After Hours Tutoring program) kwa wanafunzi 500, na  kuwasomesha walimu 30 masomo ya lunga ya Kingereza na mbinu za kufundishia ili kuongeza uwezo na ujuzi wa walimu hao.

Tunawashukuru sana International Volunteers kwa moyo wao wa kujitolea na kushirikiana nasi katika kutoa huduma kwa mashule.”

Mkurungenzi huyo alisisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii na ukuwaji wa uchumi wa nchi,  ndio maana Best of Zanzibar imejikita katika uboreshaji wa elimu Zanzibar.

“Nia yetu kuu ni kuleta manufaa na kuedeleza msingi mzuri wa kiuchumi Zanzibar. Kwa muda mrefu sana watoto wa shule ya msingi Kijini na Mbuyu Tende wamekaa chini bila madawati kuwaletea ugumu katika kuelewa masomo na kupunguza ufanisi wao wa masomo.

Best of Zanzibar inashirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Elimu katika kuboresha viwango vya elimu katika shule za Kijini na Mbuyu Tende. Na tunaishukuru sana Wizara ya Elimu kwa kutuunga mkono katika program zetu.” Aliongezea Bw. Brian Thomson.

Shule ya Kijini ina wanafunzi 903 na Mbuyu Tende inawanafunzi 603, katika wanafunzi hao 353 wanakaa chini bila madawati.

Mkurungezi wa Masomo ya Pre-Msingi na Msingi Wizara ya Elimu, Bi Safia Rajil alikua katika hafla hiyo  na alipongeza wawekezaji hao kwa msaada wao.

Kwa niaba ya Wizara ya Elimu napenda kutanguliza shukurani zetu za dhati kwa Best of Zanzibar na International Volunteers kwa kutoa madawati haya kwa shule hizi mbili. Msaasa huu utaleta madadiliko nakuongeza ufanisi wa watoto.”

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kijini Bw. Ulimwengu Mkada Makame alishukuru sana kampuni ya Pennyroyal Ltd kwa msaada wao.

“ Shule yetu ilikua haina madawati kwa muda mrefu sana, tunashukuru Best of Zanzibar kwa kutukumbuka shule yetu.”

Wakati Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo akiukana Waraka wa Pasaka wa MAASKOFU, siri imefichuka!!

$
0
0



SIRI IMEFICHUKA!!!!!!
• Maaskofu waukana Ujumbe wa Pasaka.
• Maaskofu 4 wa TEC waliouandika wajulikana
Majina yao haya hapa, kwa taarifa za uhakika.
Nimeshtushwa sana na taarifa niliyoipata juu ya Ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ulioelekezwa kwa waumini wakati huu wa toba ya Kwaresima iliyoanza Februari 14, 2018 hadi Pasaka siku ya kusherehekea ufufuko wa Bwana Yesu Kristo (Pasaka).

Mimi ni Mkatoliki wa Jimbo la Dodoma na Askofu wangu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya.
Nikiri nilianza kupata mashaka tangu mapema ujumbe huu ulipotoka, nilijiuliza sana na hivyo nikaamua kufanya juhudi za kujua kama kweli Kanisa langu Katoliki limefikia hatua hii? Naujua utaratibu na utamaduni wa kanisa langu ndio maana nilipatwa na mashaka haya.

Kwa ambao hawajausoma ujumbe huu, ulikuwa na sura nne lakini iliyoleta tafrani ni sura ya tatu yenye ujumbe kuhusu “Dalili za nyakati zetu Tanzania” hususani katika kipengele cha siasa. Imeleta tafrani kwa sababu katika eneo hili ujumbe huu umeenda kwenye masuala ambayo siku zote yamesababisha kuwepo malumbano kuwa viongozi wa dini wanaingia mambo ya kisiasa ama wanachanganya dini na siasa.

Kwa ufupi kabisa ujumbe huu umetoa shutuma na bila shaka dhidi ya Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa shughuli za siasa kama vile uenezi, mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na mikutano ya ndani zinazuiwa kwa kutumia vyombo vya dola.

Ujumbe unaendelea kushutumu kuwa vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, uhuru wa Mahakama na Bunge unaminywa na kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.

Ujumbe umeongeza shutuma nyingine kuwa chaguzi zinaharibiwa kwa vurugu na hivyo kuacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine na kwamba hali hiyo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu, ikiachwa izoeleke tusishangae huko mbele kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa.
NIMEPATA TAARIFA ZA UHAKIKA KABISA kuwa ujumbe huu haukuandikwa na Maaskofu 35 wa Kanisa Katoliki kama ilivyotolewa na Baraza la Maaskofu (TEC).

Katika shauku yangu hii ya kutaka kujua kwa nini viongozi wangu wa Kanisa lenye heshima hapa nchini wamefikia hatua hii nimepata taarifa za uhakika kuwa Maaskofu walioshiriki kuandika ujumbe huu ni wanne (nitawataja huko mbele) na Maaskofu wengine walikataa kushiriki kikao kilichofanya kazi ya kuandika ujumbe huu.

Mniwie radhi sana nimepata mashaka makubwa sana niliposoma majina ya Maaskofu waliofanya kazi ya kuandika ujumbe huu na historia zao za mahubiri yenye uchochezi mkubwa na hata mara kadhaa wametuhumiwa kwa ukabila na uchochezi na ushahidi upo.
Maaskofu walioandika ujumbe huu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Jimbo la Zanzibar na Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge-Ngara.

Maaskofu wengine hawakushiriki kuandika ujumbe huu na kwa kuwa wanatambua dosari iliyokuwa inafanyika wakatoa udhuru mbalimbali na kwa hivyo hao Maaskofu wanne wakaifanya kazi hiyo wakishirikiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padre Raymond Saba na wakamchukua Dk. Kasala kama mshauri wa uandishi wa ujumbe huo.

Kwa kuangalia safu hiyo utaona ujumbe huu umeandikwa pasi kuwepo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wala Mwadhama Polyacarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Nimepata taarifa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Dallu aliondoka mkutanoni na kuomba udhuru baada ya kubaini mwelekeo wa ujumbe huu.

Hapo ni kujiuliza kwa nini? Na kama kuna yeyote hayaamini haya basi na awaulize viongozi hawa kama walishiriki kuandika ujumbe huo, naamini hata wao wamekwazika na kwa namna yeyote hawawezi kukubaliana na yaliyomo katika ujumbe huu hata kama watakuwa na changamoto ya kuukana hadharani kulingana na utamaduni na nidhamu ya Kanisa.

Ukiangalia Maaskofu watatu kati ya wanne walioandika ujumbe huu wanatoka Mikoa ya ama Arusha ama Kilimanjaro ambako wanasiasa wake ndio wamekuwa wakishikia bango hizo hoja walizoziandika na wao wamekuwa mara kadhaa wakipambana kutumia Ibada na shughuli za Kanisa kueneza siasa hizo.

Askofu Niwemugizi ambaye mpaka sasa ana mgogoro mkubwa na idara ya Uhamiaji kutokana na uraia wake kuwa na mashaka na yeye amekuwa akitaka kujificha kwenye kichaka cha kudai anafuatwafuatwa kwa sababu anawakosoa watawala, anafahamika kwa namna alivyojipambanua kuegemea siasa za upinzani na kuungana na wanaharakati wanaopambana na Serikali.

LAKINI kwa kungalia hizo hoja wanazozitoa kuikosoa Serikali na kutaka kujenga taharuki kwa Watanzania kuwa nchi inakwenda vibaya, mimi nimejiuliza mambo mengi sana.

Maaskofu hawa wanne wanadai shughuli za kiasiasa zimezuiliwa, hivi ni mwanasiasa gani amezuliwa kufanya siasa? Maaskofu hawa wanawasikiliza akina Freeman Mbowe, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Tundu Lissu na genge lao linalojumuisha Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu kinachoongozwa na mwanachama wa CHADEMA Dk. Heleni Kijo-Bisimba ambao wanataka shughuli za siasa iwe ni kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya maandamano, fujo na uchochezi?

Wakawaulize wanasiasa hao ni lini wamekatazwa kufanya shughuli za siasa kwenye majimbo yao? Au kwa wao wanafurahishwa na kauli za Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuwa Watanzania wawe tayari kufa 100 hadi 200 kwa ajili ya yeye kwenda Ikulu? Hawataki hata kumuuliza Freeman Mbowe kwa nini kaatamia uenyekiti wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20?

Maaskofu hawa wanne wanashutumu kuwa vyombo vya habari vimefungiwa na vingine vimefungiwa kwa muda na hivyo kupunguza uwigo wa wananchi kupata habari, maoni na uhuru wa kujieleza. Hivi Maaskofu hawajui kuwa uhuru huu una mipaka na ni kwa mujibu wa sheria? Maaskofu hawajui vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kwa sababu vimevunja sheria? Nimejiuliza sana hivi hata ndani ya Kanisa Katoliki hakuna mipanga ya uhuru wa kujieleza?

Labda niwaulize Maaskofu kama mnahoji hilo, Je Kanisa Katoliki lenyewe limejihoji juu ya hatua lilizomchukua Padre Felician Nkwera? Kwa ambao hawajui Padre huyu alikuwa hodari wa mahubiri na alipendwa sana na waumini akawa tishio ndani ya vigogo wa Kanisa Katoliki, matokeo yake alipigwa fitina hadi Makao Makuu Roma Italia na mwishowe alitengwa na Kanisa.

Padre Privatus Kalugendo vivyo hivyo aliweka msimamo wake na akaamua kuoa ambayo ni haki ya mwanadamu yeyote, matokeo yake alitengwa na akafukuzwa kwa tamko la Papa, ambalo huwa halipingwi. Padre Titus Mageranga wa Iringa yalimkuta hayo hayo, na hata Askofu Jacob Koda wa Jimbo la Same Kilimanjaro naye yalimkuta hayo hayo.

Mifano ipo mingi, hivi kuna mtu anajiuliza Askofu Mkuu Norbet Wendelin Mtega yupo wapi? Askofu Mahiri kabisa aliyeliongoza Jimbo Kuu Katoliki la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba kule Songea, Ruvuma. Alipigwa fitna akaondolewa kimyakimya mpaka leo haijulikani yupo wapi na Kanisa Katoliki halijatoka kwa waumini kuwaambia alikosa nini na yupo wapi?

Na hili halipo Tanzania tu, huo ndio utamaduni wa Kanisa hili kwamba katika ngazi hizo za vigogo wakubwa, ukienda tofauti na matakwa yao bila kujali una haki au huna haki unafukuzwa, unafichwa Roma ama unawekwa popote duniani ama unapotezwa kabisa maana inakuwa hakuna mawasiliano na nyumbani wala ndugu zako. Wakatoliki wanaujua ukweli huu. Nausema kwa sababu walioanzisha kufukunyua mambo ya kuvuruga nchi ni vizuri wajue kuwa hata wao sio wasafi hivyo na sisi waumini tunajua mengi ila tunaheshimu tu.

Maaskofu hawa wanne wanasema vyombo vya habari vinafungiwa, nimewaza sana na nikakumbuka jinsi viongozi hawa hawa wa Kanisa Katoliki kule nchini Rwanda walipotumia kituo cha redio kueneza chuki miongoni mwa Wanyarwanda na kusababisha mauaji ya halaiki mwaka 1994, ambapo watu takribani Milioni 1 waliuawa kikatili kwa kuchinjwa, kuchomwa moto na kupondwapondwa kwa madai kuwa ni mende.

Kwa wasiojua mauaji ya halaiki ya Rwanda yaliibukia kwenye ukabila lakini fukuto lilianza zamani na miongoni mwa waliokuwa wanatengeneza fukuto hilo ni viongozi wa Kanisa Katoliki ambalo lina mizizi mikubwa nchini Rwanda.
Askofu Rwemugizi ambaye ana mgogoro na idara ya Uhamiaji kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania bali nchi jirani anaujua ukweli huu na anajua vizuri madhara ya mchezo anaoufanya, naamini ama anashauku ya kuona tena mauaji yale ama anafanya kwa malengo mahususi.

Maaskofu hawa wanne wanasema Mahakama na Bunge vinaingiliwa, lakini hawajasema ni wapi mihimili hii imeingiliwa.
Kwa ujumbe unaotoka kwa jina la chombo kikubwa kama Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) nilitegemea kusoma mifano na uthibitisho wa kuingiliwa kwa mihimili hii.

Hii ni hatari kubwa sana kutoa tuhuma nzito kama hizo dhidi ya mihimili ya dola halafu ukaacha zinaelea hewani. Watoke tena Maaskofu hawa wanne waseme kwa uwazi na kwa uthibitisho kuwa mihimili hii imeingiliwa hapa na hapa na hapa.
Maaskofu hawa wanne wanasema chaguzi zinafanywa kwa vurugu na zinaacha chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Japo kuwa kauli hii imeachwa inaelea lakini kwa namna yoyote Maaskofu wanatuhumu kuwa wanaoshindwa kwenye chaguzi nyingi hapa nchini ambao ni vyama vya upinzani ndio wanaobaki na hasira na chuki.

Hapa Maaskofu wanataka kutuambia kuwa ni Tanzania peke yake ambako wanaoshindwa kwenye uchaguzi ndio wananuna? Hivi kwenye chaguzi za ndani ya CHADEMA wanaokosa huwa hawanuni? Ina maana Maaskofu huwa hawaoni vurugu ambazo hutokea kwenye mataifa mbalimbali wakiwemo jirani zetu wa Kenya hata Taifa kubwa la Marekani ambao wamefanya uchaguzi karibuni? Mimi nilidhani jukumu la maaskofu lingekuwa kuponya kwa imani makovu ya uchaguzi hasa kwa wanaoshindwa na badala yake wanataka hapa Tanzania ndio paonekane pana tatizo kubwa na wanatuma ujumbe wa kuwachochea wananchi waikasirikie Serikali.

HITIMISHO.

Kwa sisi Wakatoliki hiki kilichofanywa na Maaskofu hawa wanne ni lazima kikemewe kwa nguvu zote. Naamini Kanisa linao Maaskofu wazuri, wacha Mungu na wanaotambua umuhimu wa Kanisa katika nchi, wanatambua umuhimu wao katika kuimarisha ustawi wa jamii badala ya kuivuruga.

Na hata katika mahubiri ya leo Jumapili ya Matawi (Machi 25, 2018) tumewasikia Maaskofu na Mapadre wazuri wakihubiri Injili juu ya Mateso ya Yesu na kusulubiwa kwake kwa ajili ya wanadamu. Wanafanya kazi ya Mungu ya kuwajenga waumini kwa imani, kutubu dhambi na kushika njia iliyonyooka, wametufundisha mambo muhimu katika maisha ya ukristo na kamwe viongozi hawa hawawi na mahubiri ya mihemko na siasa zinazoleta chuki na uchochezi.

Tunajenga Taifa la wachapakazi, nchi yetu ipo nyuma sana kimaendeleo, Maaskofu na Mapadre wetu wazuri wanahubiri matumaini, wanawaombea viongozi wa Serikali kuwa watumishi bora, wenye hofu ya Mungu, wanaviombea vyombo vya haki kutenda haki na wanawaombea Watanzania na dunia nzima kupigania amani, upendo, mshikamano na udugu badala ya kushabikia kauli na uchochezi wa kuleta vita, mapigano, malumbano na fitna.

Maaskofu na Mapadre Wakatoliki wazuri wanawahimiza Watanzania kufanya kazi mashambani na makazini ili kujipatia kipato halali kwa kuwa imeandikwa asiyefanya kazi na asile, wanawahimiza Watanzania kutovunja sheria na kuheshimu mamlaka zote badala ya kuchochea watu wakeshe kwenye maandano, malumbano na mapambano na Serikali.

Naamini mtazamo huu sio wa kwangu pekee yangu, naamini wapo Wakatoliki wengi ambao wamechukizwa na sehemu ya ujumbe huu wa Kwaresima ulioandikwa na Maaskofu hawa wanne, nawaomba tusiyumbishwe na hilo, tuendelee kuipenda nchi yetu na kuungana na Serikali hasa wakati huu ambapo kiongozi wa nchi Mhe. Rais Magufuli anafanya mambo makubwa ya kimageuzi katika uchumi, ustawi wa jamii, kutetea wanyonge na kudhibiti wizi wa mali za umma.

Natambua kuwa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) nao wamefanya makosa haya haya yaliyofanywa na TEC, natambua vinara wa kutoa Ujumbe wa Pasaka wa KKKT ni watu wa mlengo gani, natambua kwa nini wamekasirishwa hivyo lakini hili wacha niwaachie waumini wa KKKT wenyewe, mimi nipo na hawa wa kwangu Kanisa Katoliki.

Kwa Maaskofu wote na viongozi wengine wa dini, naomba niseme Tanzania ninayoijua mimi ina watu ambao wapo makini sana hasa linapokuja suala la nchi yao, sisi Watanzania tunapenda amani, tunapenda upendo, sisi ni ndugu sana, hatujazoea vurugu, hatupendi ukabila na ukanda, tunawapenda majirani kama Yesu alivyosema na ndio maana hao wanasiasa walioasisi haya mnayoyasema leo wameshindwa kwenye uwanja wa siasa na sasa wanataka kuwatumia nyie kwenye makanisa.

Ninachokiona kwa kuwa mmesahau kuwa Makanisani kwenu kuna waumini wenye milengo tofauti ya siasa tunakokwenda mtayavuruga Makanisa, kwa Kanisa Katoliki itakuwa ni mtihani mkubwa kwa sababu hakuna utaratibu wa Askofu kupigiwa kura ili aendelee ama asiendelee kama ilivyo kwa Makanisa mengine, kwa hiyo kitakachotokea ni kuendelea kukimbiwa na waumini kama ambavyo mmewapoteza waumini wengi kwenda kwenye makanisa ya Kilokole.

Kwa makanisa yenye uchaguzi wa Maaskofu ninachokiona ni kuendeleza mitafaruku ambayo mpaka leo inazitafuna baadhi ya Dayosisi zenu. Tena huku mlikoingia ndio kubaya zaidi maana sasa vyama vya siasa vitaanza kushindana kuweka Maaskofu wao. Inawezekana msilione hili lakini mkae mkijua kuwa litakapofika hapo hamtaweza kulidhibiti.

CHADEMA walipoanzisha kumchukua Mwana CCM Lazaro Nyalandu walidhani CCM watakaa kimya, walichokipata na wanachoendelea kukipata wote mnaona. Sasa na nyinyi mmeamua kuingia kwenye siasa za kushabikia hoja za CHADEMA na kutumwa na CHADEMA kuichokonoa Serikali ya CCM, mjiangalie siku CCM nao wakiingia huko Makanisani kwenu mjue shughuli itakuwa pevu.

Nawaombeni msituharibie Kanisa. Acheni Makanisa yafanye kazi yake ya kuhubiri Injili, siasa waachieni wanasiasa, harakati waachieni wanaharakati na vita waachieni wanajeshi.

Julius Kindonga
Mkazi wa Dodoma Machi 25, 2018

Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

$
0
0


Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali imesema itaendeleza mapambano ya Vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kuongeza kasi katika kuzuia maambukizi  mapya ikiwemo kutoa elimu kwa umma.
Akizungumza mjini Dodoma wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulikia Ukimwi na Madawa yakulevya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali baada ya kuanzisha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) ni kuhakikisha kuwa mfuko huo unajengewa uwezo ili lengo la kuanzishwa kwake litimie.
"Tayari mfuko umeweza kukusanya bilioni 279 katika kipindi kilichopita na mwaka huu bilioni 3 zimetengwa katika Bajeti na zitaingizwa katika mfuko huu ili uweze kutimiza majukumu yake kwa ufanishi na tumekuwa tukiwashirikisha wadau katika kuchangia na wamekuwa wakituunga mkono na tunaendelea kuwaomba wajitokeze zaidi  kuchangia mfuko huu " Alisisitiza Mhagama.
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa tayari mapendekezo kuhusu kuwepo kwa tozo maalum katika kodi yameshawasilishwa katika kamati husika kwa hatua zaidi dhamira ikiwa ni kuujengea mfuko huo uwezo wa kuwa na fedha za kutosha katika kufanikisha vita dhidi ya Ukimwi hapa nchini.
Mkakati mwingine ni ujenzi wa kituo maalum katika eneo la Mererani  Mkoani Manyara kitakachosaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli za uchimbaji madini.
Hatua nyingine ni kufanya kazi kwa kushirikiana kati ya TACAIDS  na Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuwafikia waathirika wa dawa za kulevya ambao ni moja ya makundi yanayoathika na ugonjwa wa ukimwi kwa mujibu wa tafiti mbalimbali.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.  Osca Mukasa (Mb) amesema kuwa kutengwa kwa fedha katika bajeti ya 2018/19 zitakazopelekwa katika mfuko wa kudhibi Ukimwi ni ishara nzuri kuwa serikali imeweka mkazo katika mapambano dhidi ya janga hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard  Maboko amesema Tume hiyo iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mkakati wa Nne unaolenga kuongeza  nguvu ili kufikiwa kwa malengo ya mkakati huo.
Akifafanua Dkt. Maboko amesema kuwa Tume hiyo imeandaa kampeni maalum kuhamasisha wananchi kupima ili kujijua kama wameambikizwa virusi vya ukimwi au laa hali itakayowasaidia kuchukua hatua stahiki na kwa wakati hivyo kuzuia maambukizi mapya hasa kwa vijana.
"Hapa nchini kwa mwaka kuna maambukizi mapya elfu 81,000 hivyo ni vyema tukaungana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu kwa kuwa uwezo wa kuzuia maambuki mapya tunao". Alisisitiza Dkt. Maboko.
Warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya imefanyika mjini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wote wa kamati hiyo, Aidha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) unalenga kuongeza rasilimali fedha kutoka asilimia 7 (2015) hadi asilimia 30  (2018).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama akizungumzia mikakati ya Serikali kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema Bungeni mjini Dodoma. kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira mhe. Antony Mavunde.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa yakulevya Mhe. Osca Mukasa (Mb) akisisitiza jambo wakati wa warsha kwa wabunge wa Kamati hiyo kuhusu hali ya Ukimwi hapa nchini iliyofanyika mapema mjini Dodoma.kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Happiness Ndalu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiwasilisha mada kuhusu hali ya Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema Bungeni mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi  (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko  (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Edward Mwalongo (Mb)  mara baada ya warsha kwa wajumbe wa Kamati hiyo mapema mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi  (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko (katikati) akitoka nje ya Viwanja vya Bunge mjini Dodoma mara baada yakuwasilisha mada kuhusu hali ya ukimwi  hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa yakulevya.
( Picha zote na Frank  Mvungi, Maelezo Dodoma)

VIDEO-FAHAMU KWA UNDANI FAIDA YA TUNDA LA PAPAI MWILINI

JINSI YA KUWAUA PANYA WENGI SHAMBANI AU MAJUMBANI

$
0
0

Wengi mmekua mkihangaika kumalizana na hawa jamaa hii ndo komesha yao twendeni :
Changanya mchanganyiko huu vizuri
Cement -Kilo 3
Unga wa ngano (wakiwandani) - kilo
Dagaa waliosagwa -robo kilo
Unga wa cocoa -vijiko sita
Chumvi laini -vijiko kumi vikubwa
Mchanganyiko utategemea na ukubwa wa vita yako .
Kisha nenda maeneo wanayopenda kushinda au ficho lao mwaga mchanganyiko huu ,pembeni weka maji ya kunywa .
INAFANYAJE KAZI !
Mchanganyiko huu ni mtamu sana kwa panya ,baada ya kufurahia mlo huu panya atasikia kiu kali ataenda kunywa maji,lahaula atakuwa amekamilisha mchanganyiko wa kutengeneza kitofari chakumbana tumbo ambacho kitamuua ndani ya siku 3 ,Mchanganyiko huu unauwezo wa kuua panya 1000 ndani ya siku 3.
Asanteni.
No automatic alt text available.
LikeShow more reactions
Comment

MBUNGE ROSE TWEVE KUWAWEZESHA WANAWAKE MKOA WA IRINGA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (KUSHOTO) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT-Tanzania Bara), Eva Kihwele na Katibu wa UWT Wilaya ya Kilolo, Judith Laizer wakiangalia bidhaa zinazotengezwa na wanawake katika Tarafa ya Mazombe.

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MACHI 29,2018

MTATURU AIPA MWEZI MMOJA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO

$
0
0


 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Miraji Mtaturu akiwa  na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na maafisa ardhi wilaya katika kikao cha pamoja kilichofanyika ofisini kwake.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akizungumza na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri na maafisa ardhi katika kikao cha pamoja ofisini kwake.
 Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiwa katika kikao na mkuu wa wilaya hiyo mh Miraji Mtaturu hayupo pichani.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Miraji Mtaturu akiwa ofisini kwake katika kikao cha pamoja na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri na maafisa ardhi ambao hawapo pichani.

...............................................................
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Miraji Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa halmashauri hiyo kuhakikisha wanaandaa maeneo na hati kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo kwa kila kata.

Mahakama hizo zitajengwa katika kata zote 28 zilizopo wilayani humo sambamba na mahakama ya wilaya.

 Mtaturu ametoa agizo hilo ofisini kwake alipokutana na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri na maafisa ardhi wilaya kwa lengo la  kujadili kuhusu  upatikanaji wa viwanja na hati kwa ajili ya kujenga mahakama hizo.

Akizungumza katika kikao hicho Mtaturu amesema mpango wa wilaya ni kujenga mahakama za mwanzo katika kata zote 28 zilizopo wilayani humo.

"Wilaya yetu ina jumla ya kata 28, mpango wetu ni kuwa na mahakama za mwanzo katika kata zote na kuwa na mahakama ya wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi,"alisema  Mtaturu.

Amesema wanaposimamia utawala bora wanapaswa kwenda sambamba na kuweka mazingira rafiki ya utoaji haki na hiyo itakuwa ni namna moja ya kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye katika uongozi wake anahakikisha anawatetea wanyonge.

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MACHI 30 , 2018

VIDEO:NDEGE ILIYOZUILIWA CANADA YAANZA SAFARI KUJA NCHINI

$
0
0


Ndege aina ya Bombadier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada imeshaondoka nchini humo kuja Tanzania.
Aidha, Ndege kubwa nyingine 3 ambapo mbili ni Bombadier CS300 kutoka Canada na Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani zitawasili baadaye mwaka huu. 

Duma aingia ndani ya gari la watalii Serengeti, Tanzania

$
0
0


Britton Hayes na mjomba wake, wote kutoka Seattle, Washington, walikuwa safarini kujionea wanyama katika mbuga ya taifa ya Serengeti nchini Tanzania pale duma huyu alipoamza kuwa mtalii ndani ya gari lao.
Mgeni huyo wasiyemtarajia alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swara.
Britton Hayes anasema walikuwa wamemuangazia duma mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao pale mwingine aliporuka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona.
“Tulianza kugundua duma hao walikuwa wameanza kuvutiwa na gari letu; lakini hatukuwa na muda wa kuondoka au kutoroka kwa sababu hutaki kuwashtua wanyama hao, ukifanya hivyo ndivyo mambo huenda mrama,” Hayes aliambia jarida la Komo News.
“Nilikuwa nimejawa na wasiwasi sana. Lakini wakati wote nilikuwa nauhisi uhai wangu,” anasema.

Urusi yawatimua wanadiplomasia 60 wa Marekani

$
0
0


Lavrov anasema Urusi itachukua hatua kwa nchi zote zilizowafukuza wanadiplomasia wake
Image captionLavrov anasema Urusi itachukua hatua kwa nchi zote zilizowafukuza wanadiplomasia wake
Urusi imewafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani, na kufunga ubalozi uliopo St Petersburg ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi juu ya shutuma ya Uingereza kuhusu kuhusika kwa Urusi katika shambulio la jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Kripal na binti yake huko Uingereza.
Hatua hiyo ilitangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.
Zaidi ya nchi ishirini zimewafukuza wanadiplomasia wa urusi nchini mwao katika kuunga mkono Uingereza.
Miongoni mwa nchi hizo ni Marekani ambapo mapema wiki hii iliwatimua wanadiplomasia 60 wa urusi kuondoka Marekani.
Boris Johnson anasema hatua hiyo ya Urusi ni sawa na kutaka kuwasha moto zaidi
Image captionBoris Johnson anasema hatua hiyo ya Urusi ni sawa na kutaka kuwasha moto zaidi
Katika kujibu hilo Urusi imewatimua wanadiplomasia 58 kutoka Moscow na wawili kutoka mji wa Yekaterinburg, chombo cha habari cha Interfax kiliripoti.
Lavrov alisema kuwa nchi nyingine zilizowafukuza Warusi wasubiri majibu kwa vitendo.
Ameongeza kuwa Ubalozi wa Marekani umepewa taarifa juu ya hatua hiyo kama majibu kwa Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake na kusimamisha ubalozi ulioko St. Petersburg.
Baada ya hatua hiyo msemaji wa Marekani amesema kuwa Urusi haina nia ya kuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingine, na hivyo Marekani ina haki ya kuchukua hatua nyingine dhidi ya Urusi.
''Urusi imeamua kujitenga Zaidi yenyewe, tunaangalia maamuzi ya kuchukua'' Heather Nauert aliwaambia waandishi wa habari.
Kripal (kulia) bado yupo katika hali mbaya hospitalini
Image captionKripal (kulia) bado yupo katika hali mbaya hospitalini
Urusi imekataa kuhusika kwa namna yoyote na jaribio la mauaji kwa jasusi wake wa zamanie.
Kripal bado yupo katika hali mbaya hospitalini lakini Binti yake anaendela vizuri na ameondoka katika hali ya hatari.
Kutokana na kuhusishwa kwa Urusi na tukio hilo mapema Uingereza ilisema kuwa hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya Malkia kushiriki kombe la dunia.
Itakumbukwa kuwa mwaka 1986 Rais wa Marekani Ronald Reagan aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Urusi.
Na mwaka 2016 uongozi wa Barack Obama uliwafukuza wanadiplomasia 35 kutokana na kudukua chama cha Democratic.

Mada zinazohusiana

Daunguro 'kubwa zaidi' la makahaba barani Asia lapata sura mpya

$
0
0


Muonekano wa jumla wa mtaa wa makahaba wa SonangachiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionPicha ya jengo lenye mchoro katika mtaa wa Sonangachi wa makahaba katika wilaya ya Kolkata
Wasanii wa michoro wasiokubali jinsia ya maumbile yao wamekuwa wakiipatia sura mpya ya michoro ya rangi za kuvutia wilaya yenye idadi kubwa ya makahaba ya Sonagachi iliyopo katika jiji lililopo mashariki mwa India la Kolkata (zamani likiitwa Calcutta).
Picha hiyo juu inaonyesha mchoro uliochorwa kwenye jengo la chama cha ushirika cha makahaba.
Ikisemekana kuwa wilaya yenye idadi kubwa zaidi ya mahahaba bara Asia, Sonagachi ni wilaya yenye mitaa yenye barabara nyingi nyembamba na njia za uchochoroni kati kati mwa jiji la Kolkata, ikiwa ni makazi ya makahaba takriban 11,000.
Indian commuters walk past a painted building at Sonagachi red light district in Kolkata,Haki miliki ya pichaEPA
Wakifanya kazi kwa ushirikiano na wasanii wenye makao yao Bangalore, wasanii wa michoro wasiokubali maumbile yao ya jinsia (transgender) walichora michoro kwenye michoro ya rangi za kuvutia kwenye baadhi ya majengo kama sehemu ya kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu haki za makahaba na pia kujaribu kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Uchoroji wa michoro hii ulichukua muda wa wiki nzima

Mengi kati ya madanguro haya yamechakaa.
Wapitanjia katika mtaa wa makahaba katika wilaya Sonagachi jijini KolkataHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWapitanjia wa Kihindi wakipita kwenye mtaa wa madanguro ya makahaba yenye michoro katika wilaya ya Sonangachi jijini Kolkata
Kuta katika mtaa wenye majengo yaliyosongamana pia zilipakwa rangi.
Wapitanjia katika mtaa wa makahaba katika wilaya SonagachiHaki miliki ya pichaEPA
Hapa wapitanjia na wafanyabiashara wanaonekana kwenye moja ya jengo lililopigwa rangi.
Kuna mipango ya kuyapaka rangi majengo zaidi katika wilaya ya Sonangachi.
Indian commuters walk past a painted wall at Sonagachi red light district in KolkataHaki miliki ya pichaEPA
Ukahaba umesalia kuwa tatizo kubwa kwa India, ambako wanawake milioni tatu wanaaminiwa kufanya biashara ya ukahaba.

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 30.03.2018: Isco ameendelea kutafutwa, Robert Lewandowski naye anaitaka Madrid

$
0
0


Isco
Image captionManchester City inatuma kusaini makataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Mhispania Isco
Manchester City wanaamini wanaweza kusaini makataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Mhispania Isco msimu huu wa majira ya joto. Mkataba kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 unaweza kuwa wa thamani ya Euro milioni 75. (Mirror)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ubelgiji Mousa Dembele, mwenye umri wa miaka 30, hatasaini makataba mpya na Tottenham kabla ya Kombe la Dunia la mwaka huu, na hivyo kuibua maswali kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29, atawasilisha maombi yake ya kutaka kuhamia Real Madrid msimu huu wa majira ya joto. Mchezaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 25 na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Alvaro Morata ni mmoja wa washambuliaji ambao Bayern Munich inamtaka kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Pole iwapo watampoteza. (AS - in Spanish)
Winga wa Crystal Palace Andros TownsendHaki miliki ya pichaHUW EVANS PICTURE AGENCY
Image captionWinga wa Crystal Palace Andros Townsend anasema kuwasaidia Eagles kuepuka kushuka daraja ni suala analolipa kipaumbele zaidi.
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Paris St-Germain midfielder Hatem Ben Arfa ametangaza kuwa ataondoka katika Ligi kuu ya Ufaransa mwisho wa msimu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, raia wa Ufaransa, amekuwa na uhusiano na Leicester City. (Sun)
Meneja wa Watford Javi Gracia amemkosoa Abdoulaye Doucoure, mwenye umri wa miaka 25, kwa kukataa kuhama katika msimu huu wa majira ya joto, huku Manchester United Tottenham, Liverpool na Arsenal kwa pamoja wakimthamanisha mchezaji huyo wa kiungo cha kati kwa kiwango cha Euro milioni 40. (Mail)
Mmiliki wa Newcastle United Mike AshleyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMmiliki wa Newcastle United Mike Ashley ataanza mkakati wake wa kuuza klabu hiyo
West Ham wana imani ya kusaini mkataba na nahodha wa timu ya Urusi Fyodor Smolov. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anayechezea klabu yake ya soka ya Krasnodar, anaweza kuhama kwa malipo ya Euro milioni £15m. (Mirror)
Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley ataanza mkakati wake wa kuuza klabu hiyo mara tu watakapohakikishiwa kwamba watafanikiwa kusalia Ligi ya Premia. (Telegraph)
Ligi ya Premia inatarajia kuanza kujaribu kupunguza idadi ya waamuzi katika mchakato wa video ya usaidizi wa maamuzi ya marefarii (VAR), badala ya kutegemea video rasmi bila kumuhusisha mtu yeyote. (Times)
Rhian Brewster
Image captionKijana Rhian Brewster mchezaji wa timu ya England ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 anasakwa na timu za Ligi ya Primia na nyingine
Manchester United imeanzisha msimu wa kupunguza gharama za tiketi za kuangalia michezo yake kwa vijana wenye umri wa miaka 16 hadi 25 kwa lengo la kuboresha uwepo wa watazamaji katika Old Trafford. (Telegraph)
Liverpool itaanzisha mazungumzo na kijana wa kikosi cha England kilichochukua kombe la dunia la vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Rhian Brewster. Klabu mbali mbali za Ligi ya Primia na nyingine zimeonyesha nia ya kumtaka na mkataba wake wa sasa unamalizika katika msimu wa majira ya joto. (Sun)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekosolewa na daktari wa zamani wa Bayern Munich, ambaye anasema kuwa anaweka mbele mafanikio mbele zaidi ya afya ya wachezaji. (Mail)
Winga wa Crystal Palace Andros TownsendHaki miliki ya pichaHUW EVANS PICTURE AGENCY
Image captionWinga wa Crystal Palace Andros Townsend anasema kuwasaidia Eagles kuepuka kushuka daraja ni suala analolipa kipaumbele zaidi.
Meneja wa timu ya Ubelgiji Roberto Martinez amemuonya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Tottenham Toby Alderweireld mwenye umri wa miaka 29, kwamba nafasi yake katika kikosi cha Kombe la dunia imo mashakani ataendelea kutopendelewa na Mauricio Pochettino. (Guardian)
Winga wa Crystal Palace Andros Townsend, mwenye umri wa miaka 26, anasema kwamba licha ya kwamba ananuia kurejeshwa na England , kuwasaidia Eagles kuepuka kushuka daraja ni suala analolipa kipaumbele zaidi. (Mirror)
Meneja wa Cardiff City Neil Warnock amejipapatia jina la mtu wenye roho nyepesi, akiongeza kuwa: "Ninalia sana ninapotazama kipindi cha televisheni cha - I watch Call the Midwife." (Mail)
Lee Bowyer anasema alikuwa mshindani sana kama mchezaji wakati fulani lakini anataka sana kujulikana kama meneja anayewajali wachezaji Charlton. (Express)
Mchezaji wa safu ya kati wa Arsenal mFaransa Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 31, ameanza kufanya yoga kwa ajili ya kurefusha muda wake kama mchezaji wa kulipwa. (Sun)

Mada zinazohusiana

Xdolls: Vyumba vya midoli ya mapenzi vinavyozua mjadala Paris vyanusurika

$
0
0


2004 file picture of silicone sex dolls in CaliforniaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMmiliki wa Xdolls amesema midoli yake ni sawa na vifaa vingine vya kujitosheleza kimapenzi
Madiwani katika jiji la Paris wametupilia mbali hoja ambayo ililenga kufunga biashara ambayo imekuwa ikihusisha watu kulipia kukaa na midoli ya mapenzi kwa saa moja.
Wateja hulipishwa €89 ($109; £78) kukaa na midoli hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya silicone.
Madiwani wa chama cha Kikomunisti pamoja na watetezi wa haki za wanawake walikuwa wameliomba Baraza la Jiji la Paris ambalo huhusika katika kusimamia jiji hilo kujadili uwezekano wa kufunga biashara hiyo ambayo imekuwa ikifahamika kama Xdolls.
Wamekuwa wakisema biashara hiyo inadhalilisha wanawake na kimsingi ni kama danguro.
Ni haramu kumiliki au kuendesha biashara ya danguro nchini Ufaransa.
Lakini polisi walifika katika biashara hiyo kabla ya mkutano wa baraza hilo la jiji kufanyika na wakatangaza kwamba hakuna sheria zozote zilizokuwa zimevunjwa.
Katika taarifa ya pamoja, madiwani wa chama cha Kikomunisti Nicolas Bonnet Oulaldj na Hervé Bégué walisema wamesikitishwa sana na uamuzi wa baraza hilo.
"Biashara hiyo, ambayo ina midoli ya ukubwa sawa na binadamu na inakaribia sana umbo la binadamu, ndio uvumbuzi wa karibuni zaidi wa kujaribu kurejesha biashara ya madanguro," walisema.
Walieleza kuwa Xdolls ni "kilele cha kuharibiwa kabisa kwa uhusiano wa wanawake na wanaume".
Harmony and Matt McMullen
Image captionMidoli ya mapenzi imekuwa ikipata umaarufu nchi mbalimbali. Doli kwa jina Harmony la kampuni ya RealDoll iliyoanzishwa na Matt McMullen katika eneo la San Marcos, California huweza kutembea na hata kuzungumza
Wamesema biashara hiyo inafanyia mzaha suala la kudhalilishwa kwa wanawake na mitandao ya biashara ya ukahaba na biashara husika ya ulanguzi wa binadamu.

Chumba huwa siri

Xdolls hupatikana katika jumba ambalo ni vigumu kulitambua katika jiji hilo la Paris.
Jumba hilo lilifunguliwa mapema mwaka huu na kujieleza kama "kituo cha michezo".
Wateja wengi huwa ni wanaume lakini wachumba pia hutembelea kituo hicho kwa pamoja, mmiliki wa kituo hicho Joachim Lousquy, ambaye zamani alimiliki maduka ya kuuza sigara, aliambia gazeti la Le Parisien.
Jumba hilo lina vyumba vitatu ambapo kila chumba kina doli la mapenzi la urefu wa 1m 45cm (futi 4 inchi 7) vya thamani ya euro elfu kadha.
Harmony and the artificial skull that lies beneath
Image captionHarmony anaonekana kama binadamu halisi lakini ndani yake ni roboti
Wateja huhifadhi nafasi kwenye chumba na kulipia huduma hiyo mtandaoni.
A photograph of a sex robot
Image captionUsifikirie hii ni picha ya mwanamke, ni picha ya roboti ya mapenzi
Anwani ya jumba hilo huwekwa ikiwa siri kubwa na hata majirani huwa hawafahamu ni biashara ya aina gani hufanyika humo, anasema Lousguy.
Anasema midoli hiyo ni sawa na vifaa vingine vya kujitosheleza kimapenzi na haoni ni jinsi gani vinawadhalilisha wanawake.
Midoli ya mapenzi imekuwa ikipata umaarufu nchi mbalimbali. Doli kwa jina Harmony la kampuni ya RealDoll iliyoanzishwa na Matt McMullen katika eneo la San Marcos, California huweza kutembea na hata kuzungumza.
Nchini Kenya wiki kadha zilizopita, doli la mapenzi lililobandikwa jina Samantha lilizua pia mjadala mkali.

Wana wa Kiume kurithi '' kasoro za uzazi za baba''

$
0
0


Wavulana waliozaliwa na baba wenye kasoro za uzazi hurithi kasoro hiyoHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionMbinu ya Kisayansi ya kutunga mimba
Wavulana waliozaliwa na baba ambao wana matatizo ya kutoweza kuwafanya wanawake kutunga mimba huenda wakawa na kasoro sawa na hivyo ikilinganishwa na wenzao waliotungwa kwa njiya ya kaiwaida.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya wa afya ya uzazi. Watafiti wamesema kwamba wavulana ambao baba zao hushindwa kuwafanya wanawake kutunga mimba watarithi matatizo hayo ya kizazi.
Wanasayansi hutumia njiya ya kutoa manii ya mwanamme aliye na uchache wake na kisha kuyadunga kwenye mayai ya mwanammke ili kutunga mimba. Mbinu hii ilianzishwa miaka ya tisini.
Watafiti walifawafanyia uchunguzi wanaume waliozaliwa kwa kwa njiya ya kutoa manii ya baba zao na kudunga kwenye mayai ya mwanammke na kugundua kwamba walikua na kasoro sawa na baba zao. Kwa mujibu wa mtafiti mkuu Profesa Andre Van Steirteghem amesema hii ndiyo mara ya kwanza imebainishwa kwamba watoto wa kiume wanaweza kurithi kasoro za uzazi zilizo na baba zao.

YANGA KUFANYA MKUTANO MKUU MEI 5 MWAKA HUU

$
0
0


Na Ripota waMafoto Blog, Dar
KLABU ya Yanga inatarajia kufanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka Mei 5 mwaka huu katika ukumbi utakaotajwa hapo baadaye jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ni matokeo ya kikao cha Kamati ya Utendaji cha Yanga kilichofanyika Jumapili ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga, ambacho kimewataka wanachama kujiandaa kwa ajenda zitakazotangazwa baadaye.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa alipozungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani Dar es Salaam.
Mkwasa, amesema kwamba mkutano huo utakuwa maalumu kwa wanachama kujadili masuala mbalimbali na mustakabali wa klabu.
Aidha Mkwasa amesema, wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada za uanachama wao mapema, kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.
“Mkutano utafanyika Mei 5 hapa Jijini Dar es Salaam, wanachama wenye kadi aina zote mbili wataruhusiwa kuingia ukumbuni, kwa maana ya wale wenye kadi za zamani na hizi zinazotolewa sasa kupitia benki ya posta,”amesema Mkwasa, aliyeongozana na Msemaji wa klabu, Dissmas Ten.
Ikumbukwe Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
Kabla ya kufikia maamuzi haya, Manji alipitia kwenye misukosuko na Serikali kuanzia Januari hadi Aprili, kwanza akikamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na baadaye akidaiwa kumiliki pasipoti mbili.
Hali hiyo ilisababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kiufadhili Yanga na kufanya wachezaji wakose mishahara kwa kipindi chote hicho kabla ya viongozi wenzake kuanza kufanya jitihada za kulipa taratibu.
Lakini kwa ujumla ni udhamini wa SportPesa ndiyo umekuwa mkombozi wa tatizo la kiuchumi la Yanga baada ya Manji kuondoka, ingawa hali ya kifedha bado si nzuri klabuni na hilo linatarajiwa kuwa miongoni mwa mambo yatakayajadiliwa Mei 5.

MAKAMU WA RAIS JERA MIAKA MITATU KWA KUVAMIA KITUO CHA UTANGAZAJI

$
0
0
ZAMBIA: Makamu wa Rais Mstaafu, Nevers Mumba amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela pamoja na kufanyishwa kazi ngumu kwa makosa mawili ikiwemo, kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma na kuvamia kituo cha utangazaji cha ZNBC mwaka 2016, kupinga taarifa iliyorushwa.

Viewing all 21839 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>