Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21933 articles
Browse latest View live

WABUNGE SITA WAPATA AJALI MOROGORO

$
0
0


Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepata ajali ya gari wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilitokea jana usiku majira ya saa tatu mkoani Morogoro ambapo majeruhi walikimbizwa hospitali ya mkoa huo.
Hata hivyo wabunge hao leo asubuhi wamepatiwa rufaa kwa ajili ya kwenda kutibiwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili na kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Wabunge waliopata ajali wanatokea visiwani Zanzibar, wabunge hao ni pamoja na Haji Ameir Haji, Khamis Ali Vuai, Bhagwanji Maganlakal Meisuia, Makame Mashaka Foum, Juma Othman Hija.

KIVITA, MKOMBOZI WA WAKULIMA TANZANIA YAANZISHWA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushito), akizungumza katika kikao cha pamoja  na Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema) cha kujadili uanzishwaji wa Taasisi ya Kilimo, Viwanda Tanzania (KIVITA), Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mratibu wa Washona Mahema, Azory Lugamba, Ofisa Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Washona Mahema, Ulimbumi Korosso, Mwenyekiti wa Washona Mahema, Shadrack Chilongani na Mkurugenzi Mtendaji wa Washona Mahema, Askofu, Edger Mwamfupe.

Na Richard Mwaikenda, Mnazi Mmoja
TAASISI mpya ya Kilimo Viwanda Tanzania (KIVITA), imeundwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi kuhusu maendeleo ya Kilimo Biashara na Viwanda.

Kivita imeanzishwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) na Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema).

Taasisi hizo mbili ambazo karibu malengo yao yanafanana zimeamua kuuanda Kivita ili kutimiza ndoto ya kuwaendeleza wananchi kwa njia ya mafunzo ili wazalishe mazao yenye ubora ili kutosheleza soko la ndani na nje ya nchi.

Pia wazalishe mazao ambayo tayari yana soko la uhakika hivyo kuondokana na hasara walioyokuwa wanaipata awali kwa kuzalisha mazao bila kujua soko liko wapi.

Pia, Kivita itasaidia jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kuendeleza viwanda nchini, kwa kuwaelekeza wananchi kuzalisha mazao yatakayokidhi mahitaji ya malighafi ya viwanda vitakavyojengwa nchini.

Mkikita na Washona Mahema ambao kwa ujumla hivi sasa wana zaidi ya wanachama 12,000 nchini, wana mipango ya kutoa mafunzo ya kuwabadilisha kifikra watanzania kutoka kwenye kilimo cha kutumia jembe la mkono na kuwapeleka kwenye kilimo cha kutumia zana za kisasa chenye mafanikio makubwa.

 Kivita itawatumia wataalamu waliobobea katika masuala ya kilimo na ufugaji pamoja na masoko kutoka Mkikita na Washona Mahema. Wataandaa makongamano kuanzia vijijini, wilayani na mikoani. 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0689425467,0754264203



 Wakiendelea na kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mkikita, Deo Liganga na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkikita, Elizabeth Ndamgoba.
  Ofisa Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Washona Mahema, Ulimbumi Korosso,
 Mwenyekiti wa Washona Mahema, Shadrack Chilongani 
  Mratibu wa Washona Mahema, Azory Lugamba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Washona Mahema, Askofu, Edger Mwamfupe.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkikita, Elizabeth Ndamgoba.

NI KWELI MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAAA!!!!

Mpiga picha wa Diamond ‘Kifesi’ aacha kazi WCB, atoa sababu mbili kubwa

$
0
0




Kifesi ameeleza kuwa muda aliyofanya kazi WCB wa takribani miaka mitano unatosha ila kilichomsukuma zaidi kuacha kazi ni kutaka kujiajiri na kuwa karibu na Mungu wake kwani kazi aliyokuwa anaifanya ilimbana zaidi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kifesi ameandika;
Leo ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku nilioamua kufanya maamzi yatayobadili maisha yangu, nimeamua rasmi kuacha kazi kama mpiga picha wa Diamond na mwajiriwa wa WCB.. Well It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me naacha kazI kwa mtu alikuwa zaidi ya Rafiki kwangu, naacha kazi ambayo ni ndoto ya vijana wengi out there but to me..i see miaka yngu 4/5 ya kufanya kazi hapa inatosha niachie nafasi kwa vijana wengine nimeamua kufata moyo wangu.
Ni uamzi niliokua nao karibu mwaka sasa but kama ilivyo kwa waajiriwa wengi is so hard kufanya maamzi ya kuacha kazi but IN ORDER TO GROW WE NEED TO MAKE CHANGE.. Naacha kazi to pursue my Dreams life ikiwamo kujiajiri mwenyewe. Naacha kazi ili nipate muda mwingi wa kuwa flexible nitumie muda wangu mwingi ku-unleash my potential for excellence.  reason ya mwisho na kubwa zaid kwangu.
Naacha hii kazi ili niwe karibu zaidi na Mungu wangu kwa imani yangu kama Mkristo nilikua nafanya kazi katika lifestyle na mazingira ya kazi yasiyompendeza Mungu, ilinibidi kujihusisha na mziki, kwenda kwenye matamsha ya mziki, kwenda maeneo ya starehe kutokua na muda wa kwenda kanisani sababu ya kazi at the end we need to choose GOD over everything, sifa, umaarufu na fahari yote ya Dunia vitanifaidia nini endapo nitaukosa ufalme wa Mungu.
Nimeamaua ku-drop kila kitu i just want to be happy, do my works live my life and have time with God, ukimchagua Mungu hata hivi vingine atakuongezea najua kutakua na changamoto nyingi, Up and downs but Mungu He knew me before was born aliahidi ukimchagua yeye he will open the doors atatufnya kuwa kichwa na siyo mkia.
Mwisho nashukuru familia yote ya WCB  kwa kuwa na mimi for all these years was great working with u.. but zaidi nimshukuru Diamond kwa muda wote niliofanya nae kazi since chini mpaka sasa, nimefnya kazi kwa mapenzi, bidii na uaminifu mkubwa kwangu haukua boss bali rafik na nilkua rafiki wa kweli kwako a will always appreciate mchango wako kwangu.. Tusameheane pale tulipowahi kukoseana we are just humans, hatutakuwa pamoja kikazi but nina imani tutaendelea kuwa marafiki. God bless you, uzidi kufika unapopenda kufika, GOD Bless me.. God bless my next Hustles #happysabbathDay
Utakumbuka Siku chache zilizopita, March 28, 2018 mara baada ya aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady kupata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Softcare Diapers, Kifesi alitupa lawama kwa Diamond kwa kumuacha Zari kwa kudai alikuwa ni mwanamke wa Baraka aliyepewa na Mungu.

Marufuku za utawala wa Rais Magufuli Tanzania

$
0
0


Rais wa Tanzania John MagufuliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Tanzania John Magufuli
Rais wa Tanzania,John Magufuli ameonekana kuwa ni kiongozi anayetoa maamuzi ya haraka kwa kutoa marufuku ya jambo au kuwaachisha kazi watendaji katika nyadhifa zao.
"Kutumbua majipu" ni neno ambalo limekuwa maarufu katika vinywa vya wengi baada ya kiongozi huyo kuwafukuza kazi watendaji pale ambapo anaona mambo hayaendi sawa.
Mfano hivi karibuni, Rais Magufuli amewaachisha kazi wakurugenzi wawili mkoani Kigoma mara tu baada ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kumkabidhi ripoti ambayo ilikuwa na matokeo mabaya katika eneo hilo.
Lakini haya chini ni orodha ya marufuku aliyoyatoa Rais Magufuli yanaoathiri sekta mbali za serikali ya Tanzania tangu aingia madarakani;
Maandamano na mikutano ya Kisiasa
Polisi wamekuwa wakitahadharisha juu ya maandamano mara kwa mara
Image captionPolisi wamekuwa wakitahadharisha juu ya maandamano mara kwa mara
Rais Magufuli amenukuliwa akisema shughuli za siasa ikiwa ni pamoja na maandamano na mikutano ya hadhara isimame hadi uchaguzi ujao mwaka 2020.
Amedai baada ya uchaguzi uliopita, "sasa ni wakati wa kazi tu"
Vyombo vya usalama vimekuwa vikitahadharisha mara kwa mara kuwa hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo.
Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania.
Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.
Shughuli za siasa, ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ni haki ya raia kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Usafirishwaji wa madini nje ya nchi

Rais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini alipofanya ziara ya kushtukiza MachiHaki miliki ya pichaIKULU
Image captionRais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini alipofanya ziara ya kushtukiza Machi 2017
Mwaka jana, Rais Magufuli alipiga marufuku usafirishwaji wa madini yasiyo chenjuliwa mpaka pale kodi za nyuma ziwe zimelipwa.
Serikali hiyo iliweka mpango wa utaratibu utakaowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia yaani Smelter, hapa nchini ili kudhibiti upotevu wa mapato na kutengeneza mapato kwa watanzania.

Waliopata mimba shuleni wasirejee shule

watapata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanafunzi watakaopata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleni
Rais Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wanafunzi wa kike ambao watakaopata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleni.
Aidha Magufuli alikumbusha kwamba sheria inasema mwanaume ambaye atapatikana na hatia ya kumpa mimba mtoto wa shule, atafungwa jela miaka 30.
Magufuli aliongeza kwamba mwanaume huyo atapata fursa ya kutumia nguvu alizotumia kumpachika mimba msichana huyo, kufanya kilimo akiwa gerezani.
Nchini Tanzania kuna takriban wasichana 8,000 ambao huacha shule kila mwaka kutokana na kuwa wajawazito, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch.

Usajili wa meli mpya

Miongoni mwa meli za kigeni zilizosajiliwa TanzaniaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMiongoni mwa meli za kigeni zilizosajiliwa Tanzania
Miongoni mwa mambo ambayo yamepigwa marufuku nchini Tanzania tangu rais Magufuli aingie madarakani ni pamoja na kusitisha usajili wa meli mpya nchini humo 'mpaka itakapotangazwa vinginevyo'.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli aliagiza utoaji wa vibali na usajili usimame hadi hapo uchunguzi kina ufanyike kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa Tanzania na zinapeperusha bendera ya Tanzania.
Agizo hilo lilikuja baada ya taarifa za kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha huku zikiwa zinapeperusha bendera ya Tanzania.
Mbali na marufuku hizo ambazo zimetolewa na yeye mwenyewe zipo nyingine ambazo zimetajwa wakati wa utawala wake.

Shisha

shishaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionshisha
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini humo na kulitaka jeshi la polisi kufanya kila juhudi kutokomeza uraibu huo.
Tanzania
Image captionUvutaji wa shisha ni marufuku Tanzania
Katazo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Paulo makonda lilifuatiwa na lile la Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambapo alitoa agizo na kusema uvutaji shisha umekuwa ukichangia katika kudorora kwa maadili miongoni mwa vijana, na kuwapunguzia uwezo wa kiakili na kimwili wa kufanya kazi.

Viroba

Kenya wakiteketeza pombe haramu 2015Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKenya wakiteketeza pombe haramu 2015
Mapema mwaka jana,pombe zilizokuwa zinauzwa kwenye mifuko midogo ya plastiki zimepigwa marufuku kuuzwa katika maeneo yeyote nchini humo.

Nataka Kuleta Heshima ya Bongo movie- Duma

$
0
0
Nataka Kuleta Heshima ya Bongo movie- Duma

Muigizaji wa Bongo movie Duma amefunguka na kusema anataka kurudisha heshima ya Bongo movie baada ya kupotea kwenye ramani.
Miaka Kama mitano nyuma Bongo movie ilikuwa mbali tofauti na ilipofikia Leo kwani hivi sasa no Kama imeshakufa kabisa hii yote ikisababishw na kukosekana kwa ubunifu.

Lakini mkali wa Bongo movie Duma amesema anataka kuketa heshima tena katika Bongo movie na ndiondio maana ameamua kmleta muigizaji John K kutoka Australia ambaye alikulia Tanzania na mwenye asili ya Burundi wafanye naye filamu hapa nchini.
Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv , Duma aamefungua haya kuhusu kuleta heshima kwenye tasnia hii ya Bongo movie.
Kwanza naomba Watanzania watusapoti Sana kwani tunataka kuleta heshima ya Bongo movie, nimemleta John K na tunarudisha heshima ya filamu Tanzania na kuonyesha jinsi gani Duma anapambana kwa ajili ya tasnia hii na sio ya mtu mmija mmoja so Mimi napambana kwa ajiki ya industry nzima na sina matatizo na mtu”.
Duma amesisituza anaamini yeye na John K watafanya vizuri kwa sababu John K ni staa anayefanya vizuri katika filamu nchini Australia.

Dimpoz Hana mvuto, Hajakaa Kama Mwanaume-Amber Lulu

$
0
0
Dimpoz Hana mvuto, Hajakaa Kama Mwanaume-Amber Lulu

Msanii wa muziki bongo Amber Lulu amefunguka na kusema kuwa msanii Ommy Dimpoz hana mvuto wa kuwa mwanaume anaeweza kumuona kwa sababu amekaa kama kongo au mtu hasiejielewa hivi.Akiongea katika online tv ya Jonijo, mwanamuziki huyo alifunguka hayo alipoulizwa kuwa ikitokea kati ya jux na ommy dimpoz wakataka kumuoa ni na atamchagua ndipo alipokuja na majibu haya.
Unanitafutia bifu za Vannesa lakini obviously nitamchagua jux na wala sio ommy kwa sababu kwanza ommy hana ule mvuto na hajakaa kama mwanaume,yaan hajakaa kivile ila jux ndo yule mwanaume ambae hata ukimwamnagalia kwa macho tu unaona , lakini Ommy Dimpozi hawezi kukaa sehemu moja na Jux ku-battle  ni zero yani hana mvuto sijaona kitu ambacho kimenivutia kwake.”

RC SHIGELLA MGENI RASMI TANGA CITY MARATHON JUMAMOSI WIKI HII MJINI TANGA

$
0
0



Mratibu wa Mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon, Juma Mwajasho kulia akitetea jambo na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea mashindano hayo Jumamosi wiki hiikushoto ni Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao niwaandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein na Katibu wa Chama cha Riadha Mkoani Tanga (RT) Hassan Mwagomba
Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uwepo wawashiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapat afursa ya kuonyesha umahiri wao kulia ni Meneja wa Mkwabi Super Marketya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein,

Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo, Kawkab
Hussein akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huu kuhusiana na zawadi zitakazotolewa msimu huu

Sehemu ya medali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo

MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ametarajiwa kushuhudia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon msimu wa piliyanayotazamiwa kufanyika Jumamosi wiki hii mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku baadhi ya washiriki wakithibitisha kushiriki.

Alisema katika mashindano hayo msimu huu watazamia washiriki zaidi ya600 ambapo washindi watakabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo medali ambazo zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo.

Aidha alisema mashindano hayo yatashirikisha wakimbaji kwenye umbali wa kilomita 21,10 na 5 ambapo wataanzia mbio hizo kwenye eneo la Mkwabi Super Market kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia eneo hilo.

“Lakini kwa mara ya kwanza washiriki wote watakaoshiriki mashindano hayo watapewa medali na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo pia yatashirikisha washiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapata fursa yakuonyesha umahiri wao.

Alisema njia zitakazopitia mashindano hayo zimeboreshwa zaidi kiusalama kwa wakimbiaji ili kuweza kuepukana na adhari zinazoweza kujitokeza wakati yakiendelea.

Naye kwa upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein alisema msimu huo wameboresha mashindano hayo kwa kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi.

Alizitaja zawadi zinazotolewa kuwa ni mshindi wa kwanza km 21 atapata700,000 wa pili 500,000, huku mshindi wa tatu akipata 300,000 huku wengine kuanzia wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha 50,000.

Hata hivyo alisema katika kilomita 10 mshindi wa kwanza atapata 250,000, wa pili 150,000 na wa tatu 100,000 huku washindi wa kuanzia nafasi ya nne mpaka 10 watapewa 30,000 pia kutakuwa na vituo maalumu kwaajili ya kutoa huduma ya maji kwa wakimbiaji (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

SERIKALI YATOA BARAKA SHINDANO LA MISS TANZANIA

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea mpango mkakati wa Mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi ambaye sasa ndiye muendeshaji wa Mashindano hayo. Serikali imetoa baraka zake kwa uongozi wa The Look Company Limited kwa nia yake ya kurudisha heshima, hadhi na mvuto wa tasnia ya urembo hapa nchini kupitia Mashindano hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) na Naibu wake, Juliana Shonza (kushoto) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi baada ya mazungumzo yao, jana katika ofisi za Ukombozi wa bara la Afrika, zilizopo Garden avenue, Jijini Dar es salaam.

3 of 3,717 MZUKA WA SOKA NA COKA YAWAFIKIA KANDA YA KASKAZINI

$
0
0

Baadhi ya shehena ya zawadi za pikipiki watakazojishindia wateja.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi wa promosheni.
Wafanyakazi wa Bonite wakisherekea kuzinduliwa kwa promosheni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bonite wakiandamana katika mitaa ya mji wa Moshi wakati wa uzinduzi *Kuangalia mashindano ya kombe la Dunia wakiwa majumbani kwao Wakati mashindano makubwa na maarufu ya soka ya Kombe la Dunia 2018 yanakaribia kuanza, kampuni ya Coca-Cola kupitia kampuni kiwanda cha Bonite Bottlers, imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha watumiaji wa vinywaji yake kujishindia luninga bafa za kisasa (flat screen TV sets) zinakazowawezesha kufurahia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia wakiwa wakiwa na familia zao majumbani kwao. Promosheni hii mpya inajulikana kama “Mzuka wa Soka na Coka” na itanufaisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola ambavyo ni Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparletta, Schweppes Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida. Mbali na kujishindia luninga bapa za kisasa watumiaji wa vinywaji vya Coca-Cola kupitia promosheni hii wanayo fursa ya kujishindia zawadi kubwa ya pikipiki, fedha taslimu kuanzia shilingi 5,000/- hadi shilingi 100,000/- ikiwemo pia kujishindia soda za bure. Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk, amesema kampuni ya Coca-Cola ikiwa ni mdhamini mkuu wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia ,imewaandalia promosheni hii wakazi wa kanda ya Kaskazini ili kuhakikisha wanafurahia “Mzuka wa Soka na Coka” wakiwa majumbani kwao kupitia luninga za kisasa wakati huohuo wakiburudika na vinywaji vya Coca-Cola. “Tukiwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Kombe la Dunia yatakayoanza mwezi June mwaka huu tumeona kuna umuhimu wa kuwaletea wateja promosheni itakayowaunganisha na kufurahia mashindano haya makubwa duniani kupitia kunywa zetu.Zawadi za ushindi zitakuwa zinapatikana katika ganda lililopo chini ya kizibo” Kwa upande wa zawadi kubwa za pikipiki,alisema anachotakiwa kufanya mywaji wa soda ni kukusanya maganda matatu ya chini ya vizibo yanayoonyesha sehemu 3 za pikipiki, yapo yanayoonyesha sehemu ya mbele, sehemu ya kati na sehemu ya nyuma ambayo yakiungaishwa yanaonyesha picha halisi ya pikipiki “Katika promosheni hii zawadi ya soda za bure zitatolewa madukani na zawadi za fedha taslimu, luninga na pikipiki zitakabidhiwa kwa washindi kutoka ofisi za kampuni ya Bonite,” Alisema, Chris Loiruk. Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sialouise Shayo, alisema promosheni hii imelenga kuwaandaa washabiki wa soka nchini kujiandaa kufurahia mzuka wa kombe la Dunia na kufurahia mashindano haya pindi yatakapoanza.

VIDEO;WASANII WAASWA KUJIEPUSHA NA MIGOGORO

VIDEO;UHURU WA HABARI NA KUJIELEZA UNA MISINGI YAKE

NAIBU WAZIRI SHONZA , DIAMOND SASA MAMBO MURWA

MENEJA KAMPENI WA GODBLESS LEMA AHAMIA CCM

$
0
0
Katibu Mwenezi wa CHADEMA ambaye pia alikuwa Meneja Kampeni wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Gabrieli Kivuyo (kushoto) amekihama chama hicho na kujiunga na CCM. Asema, amefikia uamuzi huo kutokana na utovu wa nidhamu uliopo ndani ya CHADEMA.

MAASKOFU WAKANA NJAMA ZA KUMPINDUA MUSEVENI


MAN UNITED YAIPIGA SWANSEA 2-0

$
0
0
Man United imeshinda na kurejea kwenye nafasi ya pili ikiitoa Liverpool. Man United 2 - 0 Swansea City Lukaku 5' Sanchez 20'

DOKTA MANYUKI AFUFUA TUMAINI JIPYA KWA WAATHIRIKA WA VVU/UKIMWI AELEZEA MAAJABU YA DAWA MPYA YA KUTIBU VVU/UKIMWI.

$
0
0
Mkurugenzi wa MANYUKI HERBAL CLINIC RESEARCH(MHCR) Ndugu Hassan Rajabu Maarufu kama Dokta Manyuki anayejishughulisha na utafiti wa mitishamba na tiba mbadala ya mitishamba,Mnamo tarehe 1/4/2018 tulipata wasaa wakufanya naye mahojiano katika studio zetu za Kamanda Wa matukio zilizopo Gongo la mboto ,Kupitia mahojiano hayo Dokta Manyuki alieleza yafuatayo
Ameanza utafit
i wa mitishamba tangu mwaka 1991,akijikita zaidi katika utafiti wa ugonjwa wa HIV/UKIMWI ,Mnamo mwaka 2000 kupitia Kliniki yake yake ya MANYUKI HERBAL CLINIC RESEARCH walifanikiwa kupata fomula ambayo iliwawezesha kugundua dawa mpya ya Kupambana na Virusi Vya UKIMWI,Waliifanyia majaribio ya kutosha fomula hiyo hatimaye walipata dawa mpya aina ya HARAIVIR,Baada ya kupata matokeo mazuri kwenye majaribio  ya dawa hiyo ndipo walipoamua kuingiza sokoni rasmi kwaajili ya kusaidia watu wenye VVU/UKIMWI, HARAIVIR ni tumaini jipya kabisa la wagonjwa wa VVU/UKIMWI Kwani kwa mujibu wa Dokta Manyuki HARAIVIR Inatibu VVU/UKIMWI kwa 85% ndani ya kipindi cha miezi mitatu tu,Mtaalamu huyo aliyebobea kwenye miti shamba alisisitiza kwa kusema tumefanya tafiti kwa kipindi kirefu hatimaye tumepata jibu sahihi.
HARAIVIR NDIYO DAWA SAHIHI YA KUPAMBANA NA VVU/UKIMWI KWA 85% ASIYE IKUBALI LEO ATAIKUBALI KESHO.








Ili kuweza kupata matibabu ya HARAIVIR mgonjwa anatakiwa kuwa na vipimo vya CD4,CD8 ,VIRAL LOAD NA BLOOD PICTURE
Hii itamsaidia mgonjwa kwani kila baada ya wiki mbili au mwezi mmoja mgonjwa anashauriwa kupima ili kujua maendeleo yake kwani ndani ya kipindi cha wiki moja na nusu hadi mbili tu mgonjwa ataona matokeo ya nguvu za HARAIVIR Kwani
1.Inaongeza CD4 Haraka zaidi
2.Inapunguza CD8 Haraka zaidi,
3,Inamfanya Mgonjwa kujisikia Mwenye Nguvu.
4.Inapunguza Viral Load Haraka zaidi.
5.Inaondoa tatizo kumbukumbu kwa wale wagonjwa  walio athiriwa na VVU/UKIMWI
6.Inaondoa na kukukinga na magonjwa nyemelezi ya mara kwa mara.
 Hadi sasa HARAIVIR Imekuwa ikitumika na wagonjwa mbali mbali wa nje na ndani ya mipaka ya Tanzania.
Hivyo basi Dokta manyuki amewaasa na kuwashauri wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo sugu la VVU/UKIMWI kuanza kutumia dawa hiyo ili kurejea katika afya zao kama ilivyo kuwa awali,
KUANGALIA VIDEO YA DOKTA MANYUKI BONYEZA HAPO CHINI
ANGALIA DOKTA MANYUKI AKIELEZEA DAWA MPYA YA VVU/UKIMWI

KWA MAWASILIANO NA DOKTA MANYUKI PIGA NAMBA +255 787 88 61 60 

TUMIA HARAIVIR SASA NA BAADA YA KUPIMA CD4,CD8 NA VIRAL LOAD UONE MAAJABU YAKE

TAMASHA LA PASAKA LAFANA MWANZA

$
0
0

KIRU1
Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba na Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion wakizindua albam ya mwimbaji Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo waimbaji mbalimbali wa injili wameshiriki katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rose Muhando amefanya mambo makubwa wakati alipotumbuiza moja ya kibao chake kipya cha "Lazima Wakae" kilichomo katika albam yake hiyo ambapo mashabiki walishindwa kukaa jukwaani na kucheza wakati wote alipokuwa akitumbuiza.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika tamasha hilo leo kwenye tamasha hilo ni, Upendo Nkone, Christina Shusho, Beatrice Mwaipaja, Martha Baraka, Joshua Mlelwa, ,Paul Clement, Sifaeli Mwabuka Dan M kutoka Kenya, Christopher Mwahangila,Bonny Mwaiteje, na wengine wengi.
KIRU
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionyesha albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
1
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akifurahia albam ya mwimbaji Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” baada ya kuizindua kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kushoto ni Mwimbaji Rose Muhando.
2
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza katika tamasha hilo mara baada ya kuzindua albam hiyo kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion na kushoto ni mwimbaji Rose Muhando pamoja na maaskofu na wachungaji mbalimbali waliohudhuria kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
3
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akimsikiliza Elibariki Kingu Mbunge wa Singida Magharibi wakati wa tamasha la pasaka kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
4
Dk, Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi na Makazi na mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza akizungumza na kuwakaribisha wageni mbalimbali katika tamasha hilo.
5
Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa Msama Promotion Kanda ya Ziwa akisoma risala katika tamasha hilo.
6
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akimpongeza mwimbaji Bonny Mwaiteje wakati alipokuwa akitumbuiza katika tamasha hilo leo.
7
Hapa Bonny Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani.
8
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akicheza na Mwimbaji Bonny Mwaiteje,
9
Nyomi la Tamasha la Pasaka leo
1011
Mwimbaji Upendo Nkone akiimba huku akicheza na Mkurugenzi wa Msama Promotion.
12
Mwimbaji Joshua Mlelwa akiimba na Mwimbaji mwenzake Martha Baraka.
13
Joshua Mlelwa akifanya mambo makubwa.
14
Christina Shusho akashusha bonge la Burudani.
15
Martha Baraka akiimba na Mashabiki wake,
1617
Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Dk. Angelina Mabula akimtunza mwimbaji Christopher Mwahangila,
19
Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Dk. Angelina Mabula akikaribishwa na Alex Msama alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
20
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akilakiwa na Mkurugenzi wa Msama Promotion wakati alipowasili kwenye uwanja CCM Kirumba kama Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka.
21
Mwimbaji Rose Muhando akiimba na Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion mara baada ya kuzindua albam yake Usife Moyo
22
Mwimbaji Rose Muhando akifanya mambo makubwa jukwaani.
23
Bony Mwaiteje naye akashusha burudani nzito
24
Chrstopher Mwahangila akamwaga burudani.
25
Upendo Kone akawachezesha mashabiki wake,
26
Sifaeli Mwabuka akaimba nyimbo zake za kusifu na kuabudu ilikuwa ni burudani kabambe sana.

JK AWAPONGEZA WAANDAJI WA TUZO ZA FILAMU TANZANIA

$
0
0
Leo nimepata heshima ya kuwa mgeni rasmi katika Tuzo za Filamu za Kiswahili zijulikanazo kama Sinema Zetu zinazoandaliwa na . Nawapongeza kwa kuandaa tuzo hizi zitakazotoa chachu kwa filamu za bongo movie kuboresha filamu zao na kuzitangaza kimataifa
 

VIDEO WANANCHI WAONESHA IMANI NA TAARIFA ZA VIONGOZI

$
0
0
Attachments area Preview YouTube video WANANCHI WAONYESHA IMANI NA TAARIFA ZINAZOTOLEWA NA VIONGOZI WAKUU UTAFITI TWAWEZA
Viewing all 21933 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>