Dear Mheshimiwa Naibu Waziri Mh. J. Shonza we have always been kool kwa sababu wote tupo Chama kimoja yaani Chama Tawala I have always respected your views lakini kwenye hili la kushirikiana na huyo "MUNGU MTU" wa hicho kituo cha Radio anayetaka Wasanii wampigie magoti ninaomba kutofautiana na wewe ...hua sio rahisi kwangu kusimama against Kiongozi yoyote wa Serikali na Chama changu in the Public lakini kwenye hili la wewe kushindana na Msanii maarufu kioo chetu cha Taifa Dunianiiani on a serious note umeshauriwa vibaya sana na naona kama unataka kurudia makosa ya waliokutangulia ya Kiongozi kuchukua side za mabifu ya kijinga na kitoto baina ya Wanajamii hasa katika our Entertainment industry ...in the first place Kiongozi wa Taifa of your level badala ya kwenda kwenye neutral ground like TBC kuongelea Wasanii uliowafungia wewe ukaenda kwa "MUNGU MTU" mwenye mabifu na Msanii maarufu Duniani Mtanzania kama wewe na mimi ambaye na yeye umefungia miziki yake huku ukijua wazi kua yule "MUNGU MTU" ana mabifu ya kufikia kufungia miziki yake kutopigwa kwenye Radio anayoifanyia kazi what was that? ni nani aliyekupa huu ushauri so shallow minded na so low? na ulikua unajaribu kutuambia nini Wanachi ambao some of us tunao uwezo wa kuona na kujua kila kitu kinachoendelea behind the scene? ..I mean WaTanzania tumeaibika sana kwenye music industry Duniani na kwa muda mrefu sana leo finally Mungu amesikia kilio chetu tuna Msanii anayetuweka kwenye ramani ya Dunia ni majuzi amechaguliwa kutengeneza Wimbo na Show ya ufunguzi katika Mashindano ya Kombe la Dunia leo wewe upo busy kupigana naye kwenye Social Media hivi sisi Wabongo what has gone wrong na our thinking? ..halafu naomba kuuliza Naibu Waziri hivi kweli ndiye anayetakiwa kufungia miziki au Basata? hivi ni kweli Naibu Waziri ndiye uliyetakiwa kuwaita kina Gigi Money na Sanchi kweli seriously kuhusu mavazi na tabia zao kama wasanii? ..I mean something is wrong mheshimiwa aidha unatumiwa bila kujijua au you are missing something but kitendo cha wewe kuungana na "MUNGU MTU" against Diamond HAKIKUBALIKI CHANGE NOW! - @lemutuz_superbrand
↧
WAZIRI SHONZA AZIDI KUPINGWA NYIMBO ZA DIAMOND KUFUNGIWA
↧
Wasichana 100 waliotekwa na wanamgambo 'waachiliwa huru Nigeria'

Serikali ya Nigeria imesema wengi wa watoto 110 waliotekwa na wapiganaji wa Kiislami kutoka mji wa Dapchi mwezi uliopita wamerejeshwa.
Wizara ya habari nchini Nigeria imesema wanafunzi 101 kati ya 110 walirudishwa mapema hii leo baada ya 'juhudi za kichinichini za hapo awali.''
Jeshi ''lilisimamisha kwa muda'' operesheni katika eneo hilo ili kuhakikisha ''maisha ya watoto hao hayamo hatarini,'' taarifa hiyo imeendelea kusema.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikuzingatia idadi ya wasichana waliofariki na imesema hakuna kikombozi kilicholipwa kwa wapiganaji hao.
Taarifa hata hivyo zinadokeza kwamba wasichana takriban watano walifariki wakiwa mateka, na msichana mmoja ambaye ni Mkristo bado hajasalimishwa na anaendelea kushikiliwa mateka.
Babake msichana huyo amesema anaendelea kuzuiliwa na wanamgambo hao kwa sababu amekataa kuslimu. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, amesema ana furaha kwamba msichana huyo hakuikana dini yake.
Waziri wa habari na tamaduni, Alhaji Lai Mohammed, amesema kwenye taarifa kwamba wasichana hao waliachiliwa ''katika hali isiyo ya kawaida'' na kwa "usaidizi wa marafiki wa nchi hii.''
"Serikali ilikuwa na uhakika kwamba vita na majibizano havingekuwa suluhu kwani ingehatarisha zaidi maisha ya wasichana hao, na mfumo wa kutotumia nguvu ndio uliokuwa umependekezwa," Bw Mohammed aliongeza.
Pia alidokeza kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu wasichana hao hawakukabidhiwa kwa mtu binafsi , ili kutoa idadi rasmi ya wasichana hao.

Mzazi Kundili Bukar aliambia BBC waasi hao wanaoaminika kuwa wa Boko Haram - waliingia katika mji huo kwa masafara wa magari mapema siku ya Jumatatu na kuwasalimisha wasichana hao kwa jamii.

Waasi hao wanaaminika kuondoka mara moja.
Alisema wasichana hao walionekana kudhoofika na kuchoka - licha ya kwamba ripoti zinasema wasichana hao walipata nguvu ya kukimbia na kurudi nyumbani baada ya kuachiliwa huru.
Mzazi mwengine, Manuga Lawal, amesema aliweza kuzungumza na mwanawe ambaye alikuwa miongoni mwa waliotekwa kwa njia ya simu.
Mmoja wa wasichana walioachiliwa, akizungumza kwa simu na mmoja wa jamaa zake, amesema wasichana watano walikangagwa na kufariki walipokuwa wanalazimishwa kuingia kwenye magari na kuondoshwa wakati wa kutekwa.
Msichana huyo amesema walipelekwa msituni hadi kwenye eneo lililokuwa limezungushwa ua. Alipoulizwa iwapo walikuwa wanalishwa vyema, amesema walilazimika kujipikia chakula chao.
Serikali haijazungumzia vifo hivyo.
'Janga la kitaifa'
Wasichana hao walitekwa walipokuwa shuleni siku ya Jumatatu jioni, tarehe 19 , na kundi la waasi ambao walikuwa wameuvamia mji wa Dapchi.
Hapo awali, ilidaiwa kwamba wasichana wengi walikuwa wametoroka na hakuna aliyekuwa ametekwa.
Lakini wiki moja baadaye, viongozi walikiri walikuwa wametekwa na waasi wa Kiislamu.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alikitaja kisa hicho cha utekaji kama ''janga la kitaifa'' na kuomba radhi familia za wasichana hao, na kudokeza mwezi Machi tarehe 12 serikali ilikuwa ikifanya majadiliano na waasi ili kuwasaidia wasichana hao kuachiliwa huru wala hawakutaka suluhu ya kijeshi.
''Tunajaribu kuwa makini. Ni heri kuwapata wasichana wetu wakiwa hai,'' alisema kwenye taarifa iliyoonekana na shirika la habari la AFP.
- Trump apiga picha na wasichana wa Chibok
- Wasichana 82 wa Chibok walioachiliwa wakutana na jamaa zao
- Boko Haram watoa kanda ya video kuhusu wasichana wa Chibok
Utekaji nyara umezua wasiwasi mara dufu tangu kutekwa kwa wasichana wa Chibok, waliotekwa shuleni katika jimbo jirani mwezi Aprili mwaka 2014.
Jeshi na serikali hapo awali lilikuwa limekana utekaji nyara kwa wasichana wa Chibok, uliotokea kilomita 275 (Maili 170) kusini mashariki mwa Dapchi.
Rais wa zamani Goodluck Jonathan alilaumiwa kwa kutofanya bidii kuwaokoa wasichana wa Chibok.
Utekaji nyara huo ulizua mjadala ulimwengu mzima na kusababisha kampeini kwenye mitandao ya kijamii.
Zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 walitekwa nyara wamesalia ufungwani.
↧
↧
Trump atarajiwa kutangaza vikwazo dhidi ya China baada ya uchunguzi

Utawala wa rais Trump unapanga kutangaza vikwazo dhidi ya China siku ya Alhamisi baada ya kubaini kwamba taifa hilo linashinikiza wizi na uhamisho wa ubunifu kutoka biashara za Marekani.
Ikulu ya whitehouse imesema kuwa hatua hiyo inajiri baada ya miaka kadhaa ya mazungumzo yalioshindwa kupata suluhu kuhusu wala hilo.
Vikwazo hivyo vitashirikisha ushuru na masharti mengine.
Mpango huo umezua hofu kuhusu vita vya kibiashara. Ikulu ya whitehouse iliripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuweikea ushuru wa kati ya $30bn-$60bn kwa mwaka pamoja na masharti ambayo yatazuia uwekezaji .
- Mark Zuckerberg aomba radhi kwa kashfa ya Analytica
- Tanzania na Kenya zinajitenga na Afrika?
- Mimea sita ya kushangaza zaidi duniani
Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamishi yake kwa shirika la biashara duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara.
Mpatanishi mkuu wa biashara nchini Marekani Robert Lighthizer aliambia wabunge wa Congress siku ya Jumatano kwamba Marekani inafaa kuiwekea China shinikizo kali na shinikizo ya chini watumiaji wa Marekani.
Bwana Lighthizer amesema kuwa kulinda ubunifu ni muhimu kwa uchumi wa Marekani.
''Ni swala mushimu sana'' , alisema bwana Lighthizer. ''Nadhani kitakuwa kitu muhimu ambacho kitafanyika katika kuleta usawa wa kibiashara''.
Je nini kilichoshinikiza kuwekwa kwa ushuru huo?
Afisa wa biashara nchini Marekani ambaye alizungumza na wanahabari alisema kuwa Marekani ina ushahidi kwamba China inataka kampuni za Marekani kuingia katika ushirikiano na kampuni za China ili kuingia katika soko la taifa hilo kwa lengo la kuzishinikiza kampuni hizo kuhamisha teknolojia yao.

Marekani pia iligundua kwamba China inawekeza katika kampuni muhimu za Marekani na kufanya mashambulio ya mitandao.
Matokeo hayo yanatoka katika uchunguzi ulioagizwa na rais Trump mwezi Agosti kwa jina 301.
Katika kipengee cha 301 cha sheria ya biashara, serikali imejipatia uwezo wa kuwekea vikwazo mataifa ambayo inahisi hayafanyi biashara kwa usawa.
Bwana Trump mara kwa mara amekuwa akilalamika kuhusu ukosefu wa usawa kibiashara kati ya Marekani na China.
Je hatua hiyo inaungwa mkono na wengi?
Kuna wasiwasi mkubwa nchini Marekani kwamba China inatafuta teknolojia ambayo wanaweza kuitumia kijeshi. Bunge la Congress pia linapanga kupitisha sheria ambayo itaipatia serikali uwezo wa kubadilisha mikataba ya biashara za kigeni kutokana na vitisho vya kununua viwanda vya Marekani.
Lakini wanasiasa na viwanda ikiwemo watumiaji wameonyesha wasiwasi kwamba huenda China ikalipiza kisasi.
Bwana Lighthizer amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa China ikalipiza kisasi akidai kwamba Kilimo cha Marekani huenda kikaathiriwa , lakini akasisitiza kwamba hatua hiyo haitaizuia Marekani kuchukua hatua.
Iwapo watalipiza kisasi basi Marekani italazimika kuwalinda wakulima wake.
Je China imesema nini?
China imesema kuwa hakutakuwa na mshindi yeyote katika vita vva kibiashara.
Siku ya Jumanne , siku ya mwisho ya kikao cha kila mwaka cha chama tawala cha taifa hilo, kiongozi wa China Le Keqiang amesema kuwa ombi lake ni kwamba pande zote mbili zinafaa kutulia.
Pia alisema kuwa anatumai kwamba Marekani itapunguza masharti kuhusu bidhaa za kiteknolojia zinazoingia China.
↧
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 22.03.2018

Manchester United inapanga kumsajili beki wa Real Madrid Raphael Varane, 24, kwa dau la £50m. (Mirror)
Jose Mourinho hakufurahia kitendo cha ukosefu wa nidhamu cha kiungo wake wa kati Paul Pogba wakati alipoingilia kati mahojiano ya runinga ya mkufunzi huyo kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Liverpool mapema mwezi huu. (Sun)
- Mkenya kukosa Michezo ya Madola juu ya mafunzo ya jeshi
- 'Shaw anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji bora dunia'
- 'Kwa nini Mourinho amepitwa na wakati'

Chelsea imejiunga katika harakati za kumsajili beki wa Tottenham Toby Alderweireld, 29, ambaye anaweza kuondoka katika klabu hiyo kwa malipo ya £25m yaliowekwa katika kandarasi yake.(Mirror)
Kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 24, anasema kuwa anataka kuchezea klabu kubwa msimu ujao. Kandarasi ya raia huyo wa Ujerumani Anfield inakamilika mwisho wa msimu huu.(Suddeutsche Zeitung, via Liverpool Echo)

Ili kuchukua mahala pake Can, Liverpool wanaamini kwamba watamsajili kiungo wa kati wa Napoli Jorginho 26 ambaye anadaiwa kuwa na thamani ya £50m. (Mirror)
Arsenal italazimika kulipa dau la £35m iwapo inataka kumsajili beki Ruben Dias, 20, kutoka klabu ya Ureno Benfica. (Record, via Football London)

Mkufunzi wa Southampton Mark Hughes anataka kumsajili kiungo wa kati Xherdan Shaqiri, 26, kutoka Stoke kwa dau la £20m. (Star)
Everton inachunguza hali ya beki wa kushoto Luke Shaw katika klabu ya Manchester United na tayari walituma maskauti wake kumtazama mchezaji huyo 22 katika kombe la FA dhidi ya Brighton. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Besiktas Oguzhan Ozyakup, 25, anatarajiwa kujiunga na Everton katika uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu iwapo timu hiyo ya Merseyside itashindwa kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26. (Turkish-Football.com)
Burnley itajiunga katika harakati za kumsaka beki wa West Brom Craig Dawson, 27, kwa dau la £10m iwapo timu hiyo itashushwa daraja. Aston Villa na Middlesbrough pia wanamsaka mchezaji huyo. (Mirror)

Real Madrid wamekubali ombi la dau la £113m la winga Gareth Bale, 28, kutoka klabu ya ligi ya China , lakini raia huyo wa Wales anataka kuondoka katika klabu hiyo ya La Liga iwapo atajiunga na klabu nyengine kubwa Ulaya.(Diario Gol - in Spanish)
Barcelona itawatuma maskauti wake kumchunguza kinda wa Ajax Matthijs de Ligt, 18, wakati mchezaji huyo wa Uholanzi atakaposhiriki katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uingereza na Ureno. Mundo Deportivo - in Spanish)

Atletico Madrid italazimika kulipa dau la £105m kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala, 24, kutoka Juventus. (Mail)
Reading inapanga kumsajili mkufunzi wa zamani wa Swansea Paul Clement na Steve Cotterill, aliyeifunza Birmingham hivi majuzi , kuchukua mahala pake Jaap Stam ambaye alipigwa kalamu siku ya Jumatano. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid Raul anatarajiwa kuwa kocha wa vijana katika klabu hiyo. (Marca)
Nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldinho anatarajiwa kuwania ubunge katika taifa lake la Brazil. (Mail)
↧
Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo apandishwa kizimbani

Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo amepandishwa mahakamani leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mjini ambapo anashatakiwa kwa kosa la kudanganya kuwa alitekwa na kudaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.
Leo ni siku ya 21 tangu kushikiliwa kwa mwanafunzi huyo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya kufikishwa mahakamani kijana huyo amenyimwa dhamana na hakimu mkazi wa mahakama hiyo kwa sababu ya "usalama wake kuwa hatarini".
Imeelezwa kuwa kupewa dhamana kunaweza kuleta hatari zaidi, aidha hakimu huyo ameahirisha kesi hadi siku ya Jumatatu ili aweze kupitia vifungu vya sheria na kujihakikishia kama ni salama kumuachia kwa dhamana au la.
Wakati mwanafunzi huyo akiwa mahakamani mkoani Iringa kesi nyingine iliyofunguliwa na jopo la mawakili wake wakiongozwa na wakili Mpale Mpoki juu ya utaratibu mzima wa kukamatwa kwa kijana huyo pamoja na suala la dhamana, ilikua inaendelea katika mahakama kuu jijini Dar es salaam na kuahirishwa hadi tarehe nne mwezi wa nne ili pande zote ziwasilishe nyaraka zao.
Kesi hiyo ilifunguliwa dhidi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI), Mwanasheria mkuu wa serikali na mkuu wa jeshi la polisi IGP kwa madai ya kuchelewesha kumshtaki mahakamani mwanafunzi Abdul Nondo na kumnyima dhamana bila sababu ya msingi.
↧
↧
MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MACHI 23,2018
↧
UHAMISHO WA WALIMU SEKONDARI KWENDA SHULE ZA MSINGI SIO ADHABU
Afisa Elimu wa mkoa wa Pwani bwana Abdul Maulid (kulia) aliyekaa mstari wa mbele akiwa pamoja na Maafisa wenzake wa Elimu wa Mikoa na Wilaya wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Joseph Kakunda (hayupo) pichani wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Joseph Kakunda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Joseph Kakunda akimpongeza Bibi Dyness mosha ambaye ni mmoja wa Maafisa Elimu wanaostaafu mwaka huu.
...............................................................
Na Mathew Kwembe, TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema uamuzi wa Serikali kuwahamisha baadhi ya Walimu wa shule za Sekondari wanaofundisha masomo ya sanaa kwenda kufundisha shule za Msingi ulilenga kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu uliopo katika shule za Msingi nchini na kamwe siyo adhabu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema uamuzi wa Serikali kuwahamisha baadhi ya Walimu wa shule za Sekondari wanaofundisha masomo ya sanaa kwenda kufundisha shule za Msingi ulilenga kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu uliopo katika shule za Msingi nchini na kamwe siyo adhabu.
Katika hotuba yake Waziri Jafo iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Joseph Kakunda katika mkutano mkuu wa tano wa mwaka wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya Tanzania Bara jana mjini Dodoma,ametaka maafisa elimu hao kuwapanga walimu kwa vigezo vilivyoweka na serikali na sio kama adhabu.
Amema kamwe maafisa elimu wasiwapangie walimu hao wa sekondari kwenda shule ya msingi kwa kigezo cha kutoa adhabu kwa walimu bali wazingatie vigezo hivyo.
Waziri huyo amesema ameshaagiza kuwa kigezo cha mikondo ndio kiwe kigezo sahihi cha kupanga walimu.
“Nitalisimamia kwa karibu sana suala hili, pia kigezo cha kupanga walimu shule za msingi kwa kutumia idadi ya wanafunzi kinazinyima shule zenye wanafunzi wachache kuwa na walimu wa kuweza kufundisha darasa la Awali hadi darasa la saba kwa ufanisi.
“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa upo upungufu wa walimu kwa shule za msingi na walimu wa sayansi kwa shule za sekondari,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Jafo, amesema kuna upungufu wa walimu wa shule za msingi 85,000 nchini wakati ziada ya walimu wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari ni 21,000.
Waziri Jafo amesema kulingana na takwimu hizo serikali imeona ni vema walimu hawa wa masomo ya sanaa wapelekwe kufundisha shule za msingi kwani uamuzi huo wa serikali umezingatia suala la matumizi mazuri ya rasilimali watu.
Waziri Jafo amesema kulingana na takwimu hizo serikali imeona ni vema walimu hawa wa masomo ya sanaa wapelekwe kufundisha shule za msingi kwani uamuzi huo wa serikali umezingatia suala la matumizi mazuri ya rasilimali watu.
Amesema kutokana na wingi wa walimu wa sanaa katika shule za sekondari mwalimu mmoja wa sanaa alikuwa akifundisha chini ya vipindi 10 kulinganisha na mwalimu wa sekondari ambaye alikuwa akifundisha vipindi 20.
Aidha Waziri Jafo pamoja na kutambua kuwepo kwa upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo kwa upande wa msingi na sekondari, ameziagiza halmashauri zote 185 kuweka nguvu katika kukamilisha miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari pamoja na maabara.
Pia Waziri Jafo amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza agizo la kununua magari na kutenga fedha za ununuzi wa magari kupitia bajeti za Mikoa na Halmashauri.
Kuhusu wahitimu wa Darasa la saba wa mwaka 2018 kupata vyeti vyao, Waziri Jafo amesema kuwa serikali imelichukua ombi hilo kwa uzito unaostahili.
Katika risala yake, Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya Bibi Mayasa Hashimu ameiomba serikali iwasisitize wakurugenzi wa halmashauri kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya.
Pia ameiomba serikali kuweka msisitizo wa pamoja katika usimamizi wa ujenzi na ukarabati wa Matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa, maabara na hosteli shuleni.
↧
Mahakama kutoa hukumu kesi ya Nguza Viking na mwanaye Papii Kocha Tanzania
Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) inatoa hukumu katika kesi iliyowasilishwa na wanamuziki Nguza Viking maarufu Babu Seya na mwanaye, Johnson Nguza 'Papii Kocha' dhidi ya serikali ya Tanzania katika mahakama hiyo.
Wawili hao waliwasilisha rufaa katika mahakama hiyo mwaka 2015 kupinga hukumu ya kifungo cha maisha iliyokuwa imetolewa dhidi yao.Walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule waliokuwa na kati ya umri wa miaka 6 na 8 mwaka 2003.
Walikuwa wametumikia kifungo cha miaka 13 kufikia wakati wa kupewa msamaha
Babu Seya ambaye ni miongoni mwa wafungwa 1,821 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya Uhuru wa Tanganyika mnamo 9 Desemba, 2017.
Wengine 8157 walipunguziwa adhabu zao.
Wawili hao ndio walioimba kibao maarufu cha 'Seya' na walikuwa kati ya wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kufungwa maisha au kunyonga ambao walinufaika kutokana na msamaha wa rais.
- Wafungwa waliosamehewa wamshukuru Magufuli kwa kumwimbia
- Babu Seya na wanawe waachiwa huru kwa msamaha wa rais
Hatua ya Dkt Magufuli kuwasamehea wawili hao ilishutumiwa na watetezi wa haki za watoto na wanawake.
Kate McAlpine, mkurugenzi wa shirika la Community for Children Rights lenye makao yake Arusha aliambia BBC wakati huo kwamba alikuwa "ameshtushwa lakini hakushangazwa" na hatua ya rais huyo. Alisema hatua hiyo ilionesha 'uelewa mdogo' wa kiongozi huyo kuhusu masuala ya udhalilishaji wa watoto.
Alilinganisha hatua hiyo na tamko la Rais Magufuli kwamba wasichana wanaoshika mimba hawafai kuwa shuleni.
"Huwa hafahamu vyema mambo, hasa yanayohusu watoto kama waathiriwa. Wasichana wanaoenda shule hushika mimba kwa sababu mara nyingi ni waathiriwa wa udhalilishaji," alisema Bi McAlpine.
Wakishinda watadai fidia?
Kwa kuwa wawili hao walishasamehewa na rais, uwezekano wao kuchukuliwa hatua iwapo hukumu ya kifungo dhidi yao itadumishwa ni mdogo sana.Hata hivyo, iwapo watapatikana bila hatia, kuna uwezekano huenda wakawasilisha kesi wakitaka walipwe fidia kwa kipindi ambacho walikaa gerezani.
Ilikuwaje hadi tukafika hapa?
Nguza Viking na wanawe watatu walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kuwabaka na kulawiti watoto.Mwaka 2010 rufaa yao ilisikilizwa na 30 Oktoba Majaji Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati katika Mahakama ya Rufaa wakawaachilia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwapata bila hatia.
Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.
Kesi hiyo iliwashtua mashabiki wa mwanamuziki Viking nchini Tanzania, na kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.
↧
ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI
Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Zakia Meghji akitoa maneno ya hamasa kwa vijana wa Girl Guides katika semina iliyofanyika Makao Makuu ya TGGA, Mtaa wa Kibasila, Upanga Dar es Salaam.
Meghji ambaye aliwaelezea historia ya maisha yake tokea utotoni, shuleni, chuoni na ya kisiasa, aliwataka Girl Guides kuwa jasiri, waadilifu, wazalendo na wachapakazi pamoja na kuwa na vision..
Aliwafundisha jinsi ya kupambana na wanaume walaghai wanaowataka kimapenzi na kuwaharibia ndoto yao ya kielimu na maisha kwa ujumla.
Pia aliwataka kuheshimu mila nzuri, desturi na utamaduni mzuri pamoja na kuwaheshimu wazazi na jamii bila kusahau kushirikiana nao katika masuala mbalimbali.
Aliwaambia kuwa baadhi ya mambo muhimu ni kuwa na tabia ya kushirikiana na watu mbalimbali kwa lengo la kubadilisha uzoefu, mawasiliano na kwamba unatakiwa kuanza uongozi ukiwa kijana siyo ukiwa mzee.
Anawaeleza kuwa ushupavu wake ulimfanya kwa mara ya kwanza awe mbunge mwaka 1985, amekuwa Mkuu wa wilaya na waziri kwa muda mrefu mpaka alipoamua kustaafu.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203,0689425467
Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akisalimiana na Girl Guides kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na mikoani.
Mkufunzi wa TGGA Makao Makuu ya TGGA, akielezea historia ya chama hicho
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa TGGA, Grace Makenya akitoa maneno ya hamasa kwamba daima hastaafu na kwamba yeye hivi sasa ana miaka 70 lakini bado ni Girl Guides
Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
Yess Girl, Nadine Ratovoson kutoka Madagascar akijitambulisha. Yupo nchini kwa ziara ya mafunzo ya miezi sita ya kubadilishana mafunzo.
Yss Girl kutoka Zambia ambaye yupo nchini kwa ziara yamiezi sita ya kubadilisha mafunzo
Miryam Mjema na Grace Makenya
Kamishna wa TGGA, Temeke, Komba akijitambulisha
Sophia Simon (kulia) Mkufunzi wa TGGA Temeke, akijitambulisha
Kamishna wa TGGA Ilala, Stellah Kasisika akijitambulisha
Girl Guide wakiwa na furaha
Meghji akisisitiza jambo
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kulia) akiwa na Mdau wa TGGA, Asiah Abdul Azizi na Candida Bahame.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Zanaki, Winhope Mgalega, akimmuliza Zakhia Meghji ni nini siri ya mafanikio yake.
Meghji ambaye aliwaelezea historia ya maisha yake tokea utotoni, shuleni, chuoni na ya kisiasa, aliwataka Girl Guides kuwa jasiri, waadilifu, wazalendo na wachapakazi pamoja na kuwa na vision..
Aliwafundisha jinsi ya kupambana na wanaume walaghai wanaowataka kimapenzi na kuwaharibia ndoto yao ya kielimu na maisha kwa ujumla.
Pia aliwataka kuheshimu mila nzuri, desturi na utamaduni mzuri pamoja na kuwaheshimu wazazi na jamii bila kusahau kushirikiana nao katika masuala mbalimbali.
Aliwaambia kuwa baadhi ya mambo muhimu ni kuwa na tabia ya kushirikiana na watu mbalimbali kwa lengo la kubadilisha uzoefu, mawasiliano na kwamba unatakiwa kuanza uongozi ukiwa kijana siyo ukiwa mzee.
Anawaeleza kuwa ushupavu wake ulimfanya kwa mara ya kwanza awe mbunge mwaka 1985, amekuwa Mkuu wa wilaya na waziri kwa muda mrefu mpaka alipoamua kustaafu.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203,0689425467
Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akisalimiana na Girl Guides kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na mikoani.
Mkufunzi wa TGGA Makao Makuu ya TGGA, akielezea historia ya chama hicho
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa TGGA, Grace Makenya akitoa maneno ya hamasa kwamba daima hastaafu na kwamba yeye hivi sasa ana miaka 70 lakini bado ni Girl Guides
Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
Yess Girl, Nadine Ratovoson kutoka Madagascar akijitambulisha. Yupo nchini kwa ziara ya mafunzo ya miezi sita ya kubadilishana mafunzo.
Yss Girl kutoka Zambia ambaye yupo nchini kwa ziara yamiezi sita ya kubadilisha mafunzo
Miryam Mjema na Grace Makenya
Kamishna wa TGGA, Temeke, Komba akijitambulisha
Sophia Simon (kulia) Mkufunzi wa TGGA Temeke, akijitambulisha
Kamishna wa TGGA Ilala, Stellah Kasisika akijitambulisha
Girl Guide wakiwa na furaha
Meghji akisisitiza jambo
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kulia) akiwa na Mdau wa TGGA, Asiah Abdul Azizi na Candida Bahame.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Zanaki, Winhope Mgalega, akimmuliza Zakhia Meghji ni nini siri ya mafanikio yake.
↧
↧
MAFUNZO YA USIMAMIZI WA SHAMBA LA PAPAI SALAMA YAFANA DAR
IMEANDALIWA NA NA RICHARD MWAIKENDA;0715264202,0689425467,0754264203
↧
FEMINA HIP YAKABIDHI TUZO KWA WASHINDI KUMI WA SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI KUTOKA MIKOA KUMI NA TANO NCHINI

Wanafunzi kutoka shule za sekondari walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo.

Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akionyesha jarida la Fema

Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Yassin Haji kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.

Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi.

Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akiwa na baadhi ya washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi na wachama wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip.

Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Humphrey Otedo kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.
.....................
Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya vijana, Femina Hip limetoa tuzo kwa washindi kumi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi, lililoshirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa kumi na tano nchini.
Akizungumza na wanahabari wakati wa utoaji tuzo kwa washindi, Kiongozi wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip ambayo iliendesha shindano hilo, Lydia Charles amesema shindano hilo lililenga kuleta uelewa pamoja na kubaini changamoto kuhusu masuala ya hedhi wanazokabiliana nazo watoto wa kike katika jamii.
Amesema wanafunzi karibu 88 walishiriki shindano hilo, ambapo wavulana walikuwa 27 na wasichana 61. Na kwamba walioibuka washindi ni wasichana 5 na wavulana 5, huku shule ya Sekondari Chang’ombe ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya washindi na washiriki.
“Shindano hili lililenga kupaza sauti za changamoto za wasichana wanazokutana nazo wakiwa katika siku zao.Huu mradi ulilenga kumsaidia mtoto wa kike kuwa shuleni siku zote ambazo ana hedhi, kuhakikisha uwepo wa maji shuleni na vyoo visafi,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Femina Hip, Sauda Simba amesema shindano hilo limebainisha changamoto wanazopata watoto wa kike wakiwa kwenye siku zao, ikiwemo ukosefu wa taulo za kujihifadhi-Pad, na kuitaka serikali pamoja na jamii kuhakikisha watoto wa kike wanapata hedhi salama.
Kwa upande wake, Balozi wa masuala ya hedhi salama, Badru Juma ameitaka serikali na jamii kutatua changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike hasa wa kijijini.
Washindi hao ni pamoja na Veronica Felician kutoka Kondoa Girls High School kutok Dodoma, Jemima Carlos, Yasin Said,, Humphrey Otedo wote kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe, na Latifa Salumu kutoka Shule ya Sekondari Zinga.
↧
SHIRIKA LA AGPAHI LAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE KWA WILAYANI MUHEZA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake (cryotherapy machine). kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala
SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy machine).
Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.
"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema Mwakyusa.
Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze kazi.
Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.
Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
↧
WENGI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA MKIKITA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe (kushoto) akiwachangamsha washiriki kabla ya kuanza kutoa mada kuhusu Ujasiri Kilimo wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Shamba la Papai Salama yaliyoandaliwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) kwenye Ukumbi wa Anatoglou, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Mkikita na Washona Mahema wameunda umoja wa Kilimo Viwanda Tanzania (KIVITA) utakaokuwa unatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima nchini.
Mtaalamu wa Kilimo, John Charles akitoa mada kuhusu mfumo wa umwagiliaji kwenye kilimo cha papai salama wakati wa mafunzo hayo. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda: Kamanda wa Matukio Blog;0715264202,0754264203,0689425467
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akitoa utambulisho kwa baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Sehemu ya washiriki wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo hayo
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo na Malisili cha Canre, Dar es Salaam, Kogea Levi (kulia) na Frank Godson wakiwa makini kusikiliza mada kuhusu kilimo cha papai salama
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mkikita, Deo Liganga (kulia) akiwa na Mtaalamu wa Kilimo wa Mkikita, Samweli pamoja na Simeo aliyetoa mada kuhusu usimamizi wa kilimo cha Papai Salama.
Wafanyakazi wa Mkikita wakijadiliana jambo wakati wa mafunzo hayo. Kutoka Kushoto ni Meneja Uhusiano, Neema Ngowi, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Elizabeth Ndamgoba na Mhasibu Msaidizi, Samson Kalinga.
Adam Ngamange akiwa na badhi ya wadau wakati wa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange, alipokuwa akitoa mada kuhusu Ujasiri Kilimo wakati wa Mafunzo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange, alipokuwa akitoa mada kuhusu Ujasiri Kilimo wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Shamba la Papai Salama kwenye Ukumbi wa Anatoglou, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Mkikita na Washona Mahema wameunda umoja wa Kilimo Viwanda Tanzania (KIVITA) utakaokuwa unatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima nchini.
Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Uundwaji wa Ushirika wa Tanzania Holtculture Iniciative Society (THIS), Abraham Nyantory akielezea muundo wa Rasimu ya Katiba hiyo kwa wanachama watarajiwa wa ushirika huo utakaokuwa chini ya mwamvuli wa Mkikita.
↧
↧
MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MACHI 25 , 2018
↧
ONGEZEKO LA WATU, WATUMIAJI WA SIMU KUKUZA BIASHARA ZA MTANDAONI AFRIKA
Na Jumia Tanzania
Kuendelea kukua kwa ongezeko la idadi ya watu na watumiaji wa simu za mkononi barani Afrika kuna mchango kwenye ukuaji wa biashara kwa njia ya mtandao. Hilo linaenda sambamba na ueneaji wa huduma za mtandao wa intaneti ambao umebadili namna waafrika wanavyotumia simu zao za mkononi hivi sasa.
Hivi karibuni Jumia, mtandao unaojihusisha na uuzaji na manunuzi ya bidhaa mtandaoni, ulizindua ripoti kuhusu sekta ya bidhaa za simu kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Ripoti hiyo imeangazia masuala mbalimbali kwenye setka hii pamoja na mchango wake katika shughuli za kijamii na kiuchumi nchini. Ripoti hiyo pia imeangazia namna watanzania wanavyotumia simu na teknolojia ilizoambatana nazo kama vile huduma za fedha na biashara za mtandaoni.
Akizungumzia juu ya ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott amebainisha kuwa uwasilishwaji huo umekuja katika kipindi ambacho wanaendesha kampeni ya ‘Wiki ya Simu’ itakayohusisha uuzaji wa simu kwenye mtandao wao kwa kushirikiana na makampuni tofauti ya simu nchini.
“Jumia inaamini kwamba soko la simu ni miongoni mwa sekta kubwa kwenye nchi zinazoendelea barani Afrika, na ina mchango mkubwa kwenye kuziwezesha sekta zingine. Wiki ya Simu itafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuanzia Machi 24 mpaka 30, kampeni ambayo ni kubwa kabisa ndani ya mwaka ikiwa imejikita kwenye bidhaa moja pekee. ‘Jumia Mobile Week’ itawawezesha watanzania kujipatia mapunguzo na ofa mbalimbali kwenye bidhaa za kutoka kampuni tofauti za simu,” alisema Prescott.
Sekta ya bidhaa za simu Afrika ina thamani ya bilioni $110
Hivi sasa, idadi ya watu barani Afrika imefikia bilioni 1.27 ambapo takribani watu bilioni 1.04 wanatumia simu za mkononi, sawa na ueneaji kwa asilimia 82. Kuongezeka kwa idadi ya watu na mtandao wa intaneti kwenye maeneo mbalimbali kumeendelea kuifanya sekta hiyo kuwa na tija zaidi. Sekta hii ina mchango mkubwa kwenye maisha ya kila siku ya watu kama vile huduma za fedha kwa njia ya simu. Ambapo nchini Tanzania pekee, zaidi ya watu milioni 40 waliripotiwa kuunganishwa na huduma za simu za mkononi wakati kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 50 zikitumwa kwa njia ya simu.
Mwaka 2016, huduma za teknolojia ya simu zilizalisha kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 110 katika uchumi wa nchi za Kiafrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, sawa na asilimia 7.7 ya pato la ndani la taifa. Mchango wa sekta ya simu kwenye pato la taifa unatarajiwa kukua na kufikia dola za Kimarekani bilioni 142, sawa na asilimia 8.6 ya pato la ndani la taifa, kufikia mwaka 2020, kwani nchi nyingi zitakuwa zikinufaika na maendeleo katika uzalishaji na ufanisi utakaoletwa na kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi.
Ueneaji wa watumiaji wa simu Tanzania unakaribiana na wa Afrika
Hivi karibuni, Tanzania ilitangaza kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa simu na kufikia zaidi ya milioni 40, ambayo ni sawa na ueneaji kwa asilimia 72, asilimia 10 pungufu ya ueneaji wa bara zima la Afrika ambao umefikia asilimia 82.
Uwepo wa ushindani wa bei na motisha kwa wateja kwenye soko la simu umekuwa na mchango mkubwa katika unafuu wa upatikanaji wa bidhaa hizo. Kitu kingine cha muhimu, ni uwepo wa huduma mpya zinazotambulishwa na kampuni tofauti za mitandao ya simu zimekuwa ni kichocheo kikubwa kwa watanzania wengi kumiliki simu za mkononi.
Simu kutoka bara la Asia zatawala kwenye mtandao wa Jumia
Bidhaa za simu kutoka bara la Asia zinaongoza kwa kuwa miongoni mwa simu zinazonunuliwa zaidi kwenye mtandao wa Jumia. Kampuni zinazofanya vizuri ni pamoja na Tecno, Samsung, Lenovo, na Infinix, ukilinganisha na simu kutoka nchi za Magharibi (Ulaya na Marekani). Infinix ni simu inayoongoza kwa mauzo katika nchi 10 ambazo Jumia inaendesha shughuli zake, wakati Tecno ikiwa ni kinara katika mtandao huo nchini Tanzania.
Simu kutoka bara hilo zimefanikiwa kulitawala soko la Afrika kwa sababu zimeweza kuendana na mahitaji yake. Nchi nyingi za Kiafrika bado zinaendelea, ni dhahiri kwamba nguvu ya manunuzi bado ni ndogo. Kikubwa zaidi, simu zao ni za gharama nafuu na zinapatikana kwa urahisi, karibuni kila mji ukilinganisha na simu kama vile iPhone ambazo hupatikana kwenye miji mikubwa na ya kibiashara pekee.
Zaidi ya watu bilioni 4 duniani wanatumia intaneti
Idadi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti duniani imevuka bilioni 4, idadi ambayo ni sawa na zaidi ya nusu ya watu wote duniani.
Tanzania nayo inakua kwa kasi kwa upande wa idadi ya watumiaji wa simu na mtandao wa intaneti katika ukanda wa Mashariki na Afrika kwa ujumla. Mapema mwaka huu, TCRA iliripoti juu ya kuongezeka kwa idadi ya watumiaji na ueneaji wa intaneti kufikia milioni 23 sawa na asilimia 45 mwaka 2017, kutoka watumiaji milioni 7.5 sawa na asilimia 17 mwaka 2012.
Simu ni mkombozi kwa watanzania kiuchumi na kijamii
Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi inatarajiwa kuvuka bilioni 5 kufikia mwaka 2019.
Nchini Tanzania, idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi wameonekana kukitumia kifaa hiki kwa manufaa mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. Ukiachana na kuzungumza, kutumiana jumbe za maandishi au kuingia kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya watanzania wameanza kufanya shughuli zao za manunuzi mtandaoni, tena kwa kutumia simu zao za mkononi.
Mwaka 2017, asilimia 83 ya wateja wa Jumia walifanya manunuzi kwa kutumia simu za mkononi. Hii ni ishara kwamba idadi ya watanzania inazidi kuongezeka katika kutumia simu za mkononi kurahasisha shughuli zao za kila siku.
“Biashara kwa njia ya mtandao bado ni sekta mpya Tanzania, ambayo ipo kwenye hatua za awali za ukuaji. Naamini kwamba ueneaji wa huduma ya mtandao wa intaneti utachochea ukuaji wa sekta hii. Barani Afrika hivi sasa, ni idadi ndogo sana ya manunuzi yanafanyika mtandaoni, yaani kununua bidhaa kwa kutumia intaneti,” alielezea na kuhitimisha, “kuna ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wanaomiliki simu za mkononi, hususani simu janja. Hii ni hatua muhimu kwenye sekta. Lakini bado idadi ya wamilikaji wa simu janja ni ndogo, changamoto ambayo Jumia tumeiona na tungependa kuitatua kwa kuhakikisha kwamba zinapatikana kwa gharama nafuu na urahisi. Na hilo ndilo dhumuni la kampeni ya ‘Wiki ya Simu’.’”
↧
NI KWELI MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAA!!!!
↧
MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MACHI 26,2018
↧
↧
JAFO ATAKA VIPAJI VYA MICHEZO VIIBULIWE NGAZI ZA CHINI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akijiandaa kupiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya shule ya sekondari Makole katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya shule ya sekondari Dodoma katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
...................................................................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akisalimiana na wachezaji wa timu ya shule ya sekondari Makole katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
........................................................................................
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amesema kuendelea kufanya vibaya kwa Timu za Taifa katika michezo mbalimbali kunatokana na kukosekana kwa uwekezaji wa kutosha kwenye kuibua vipaji vya michezo husika.
Akikabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki mashindano ya UMISETA mjini Dodoma, Jafo amesema kuwa hali hiyo inatakiwa kufanyiwa kazi na kwamba kama ukifanyika uwekezaji mdogo kwenye michezo utaweza kuinua nchi kwenye sekta hiyo.
Waziri Jafo amesema uwekezaji kwenye michezo ni muhimu na lazima uanze kwa watoto wa shule za msingi na sekondari.
"Michezo hii haikurupuki imewekwa kwenye mpango wa Taifa upo kwenye ilani ya uchaguzi na sera za michezo ili kuhakikisha michezo inasonga mbele,"amesema.
Ameagiza kubainishwa walimu wa michezo shuleni ili kuweza kukuza kikamilifu vipaji vya michezo.
Naye, Meneja wa Kampuni ya Coca cola wanaodhamini mashindano hayo Siha Shayo amesema watagawa vifaa vya michezo kwa zaidi ya shule 4000 zitakazoshiriki mashindano hayo mwaka huu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma Deogratius Ndejembi amesema uwekezaji katika michezo ngazi za chini ni muhimu.
↧
ESRF wapongezwa kupitia SIDP
Mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5)
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Obadiah Nyagiro akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof Elisante Ole Gabriel uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk. Tausi Kida wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa-CUTS International Bw. Rashid Kaukab akizungumza wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti mshiriki wa ESRF Prof. Samwel Wangwe, akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya vigezo vya kuipitia upya sera ya maendeleo endelevu wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Obadiah Nyagiro wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Peter Nyang’ombe akiwasilisha mada kuhusu juhudi za kutaka kuwepo na maboresho ya SIDP wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi akichangia mada wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa Huru wa masuala ya Jinsia na Maendeleo Prof. Marjorie Mbilinyi akichangia hoja wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano akichangia mawazo wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Obadiah Nyagiro (katikati) na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia).
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akiongoza uwasilishaji na majadiliano ya mada ya:Maendeleo endelevu ya viwanda: Na nini Dhima ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti mshiriki wa ESRF Prof. Samwel Wangwe akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wakati akiwasilisha mada ya Maendeleo endelevu ya viwanda: Na nini Dhima ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara kwenye mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
Mwanadiplomasia Shirika la Biashara la Dunia (WTO), Bi Gloria Kidulile akiwasilisha mada kuhusu mazungumzo ya WTO: yanawezaje kuathiri maisha ya wakulima wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu,
TAASISI ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), imepongezwa kwa kazi zake inazofanya za utafiti na kutoa mwelekeo sahihi wa uanazuoni kwenye masuala mazito yanayotakiwa kutekelezwa na wananchi wa Tanzania kuendeleza ustawi na kuinua uchumi.
Aidha imepongezwa kwa kurejea kuipitia sera ya maendeleo endelevu (SIDP) ya mwaka 1996 ambayo kwa sasa inahitaji kufanyiwa marekebisho kuendena na maizngira ya sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Elisante Ole Gabriel, katika hotuba iliyosomwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara hiyo, Obadiah Nyagiro wakati akifungua mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara?
Alisema kwamba majadiliano hayo yanakwenda sawa na juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kujikita katika maendeleo ya viwanda ambapo uwekezaji na biashara ni vitu muhimu.
Alisema mwaka 1996 serikali ya Tanzania ilizindua sera ya maendeleo endelevu (SIDP) ikiwa imepangwa kuibeba nchi kuanzia mwaka huo hadi mwaka 2020.
Lengo ya sera hiyo ni ilikuwa kuiweka Tanzania katika njia ya viwanda na kufikia malengo ya kitaifa kama ilivyoelezwa katika malengo ya taifa (TDV) kufikia 2025.
Alisema kwa miaka mingi utekelezaji wa SIDP umekuwa ukisaidiwa na sera mbalimbali za kilimo, fedha na biashara na mikakati ya maendeleo.
Kuelekea katika viwanda kunakwenda sanjari na kuangalia mipango ya maendeleo ingawa kuna hisia kwamba suala la usalama wa chakula mabadiliko ya hali ya hewa na usindikaji wa mazao ya kilimo yamekuwa yakiachwa katika kuongeza uimara wa safari ya maendeleo.
Mapungufu yaliyopo ndani ya SIDP yanahitaji kuangaliwa ili kutoa umuhimu wa kuunganisha masuala hayo muhimu ambayo ni mtambuka na maendeleo ya viwanda.
Kwa kuunganisha masuala hayo na kuangalia jinsia taifa litakuwa na sera bora kabisa ya viwanda yenye kubeba kila kitu kinachotakiwa katika kuelekea uchumi unaotegemea viwanda na kujali mazingira.
Amesema kutokana na mazingira hayo ni dhahiri kwamba mkutano huo na maazimio yake yatakuwa chachu kwa watengeneza sera ambao wanatakiwa kuipitia sera hiyo na kuipa uhai mpya.
Naye Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene aliyesoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida akikaribisha wajumbe wa mkutano huo, alisema kwamba mkutano huo mkubwa wa kitaifa umelenga kutoka na maazimio ambayo yatasaidia watunga sera kuihuisha sera iliyopo na mikakati mbalimbali ya kuipeleka Tanzania katika dunia ya viwanda.
Alisema mkutano huo unafanana na ule uliofanyika Agosti 24 mwaka jana ambao uliangalia mambo mbalimbali yanayohusiana na sera hiyo na kuihusisha katika SIDP.
Alisema haja ya kuangalia sera hiyo kunatokana na ukweli kuwa kuna mapengo kadha katika sera yanayosababisha ufanisi mdogo wenye tija katika uchumi na biashara pia katika kilimo.
Upitiaji huo wa SIDP umefanywa na ESRF kwa kufadhiliwa na CUTS International na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Washiriki pia walipata nafasi ya kupewa taarifa ya hali ya kilimo nchini na majadiliano ya masoko kupitia Shirika la Biashara Duniani (WTO) na taasisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia na mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC).
Katika mkutano huo mada mbalimbali ziliwasilishwa zilizoangalia sekta mtambuka zikiwamo za kilimo na viwanda.
↧
WAKAZI WA WILAYA YA MKINGA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI WA SHIRIKA LA KITAIFA LA WATER MISSIONS INTERNATIONAL TANZANIA
Wadau wa mradi wa maji wa Mkinga wakibeba ndoo kwa pamoja wa hafla ya uzinduzi wa mradi.
Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania, Isack Abdiel, akielezea mradi huo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo.
Kisima cha maji kilichokuwa kinatumika kabla ya mradi mpya.
Sehemu ya miuondombinu ya mradi mpya.
Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na kusambaza huduma za maji la Water Missions International Tanzania, mwishoni mwa wiki limezindua mradi mkubwa utakaonufaisha vijiji 7 vya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utaowawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa matumizi yao na matumizi mengineyo na shughuli za kiuchumi. Kwa kipindi cha muda mrefu wilaya ya Mkinga imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji salama, kutokana na kutokuwepo na vyanzo vya uhakika vya maji katika eneo hilo.Vijiji 4 vya Mkinga, Mtenguleni, Mwakihonda and Karoyo vimekuwa vikitegemea kupata maji ya bomba kutoka tanki la zamani la kusambaza maji kutoka kijji jirani cha Parangukasere, ambalo limekuwa halitoshelezi mahitaji ya maji kwa wakazi wa vijiji hivyo. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Gregory Ndunguru,ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Mkinga,kuzinduliwa kwa maradi huu wilayani hapa kutawezesha wananchi kupata maji safi ya uhakika wakati wote,kwa niaba ya serikali nalishukuru shirika la Water Missions International Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini”. Mhandisi Ndunguru, alisema mradi huu utanufaisha maisha ya mamia ya wananchi wakazi wa Mkinga na kupunguza adha kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kifamilia . Alitoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa shirika hilo sambamba na kutunza miundo mbinu itakayowekwa katika maeneo yao ili kuwezesha mradi kuwa endelevu. “Mradi huu muhimu hapa Mkinga pia utaimarisha afya na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa mbalimbali yanayosababisha na ukosefu wa maji na matumizi ya maji yasiyo salama kwa kuwa hivi sasa tuna uhakika wa kupata maji salama,”alisisitiza. Kwa upande wake,Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania ,Isack Abdiel alisema “Tunayo furaha kuzindua mradi wa maji katika wilaya ya Mkinga ,ukiwa ni mwendelezo wetu wa kuunga mkono serikali ya Tanzania kuboresha upatikanaji wa maji ya uhakika na salama kwenye jamii zenye upungufu wa maji nchini,tunayo imani wananchi mmeupokea vizuri na mtaulinda ili uwe mradi endelevu ili unufaishe mpaka vizazi vijavyo”. Aliwashukuru watendaji wa serikali,mashirika yasiyo ya kiserikali inayoshirikiana nayo na wadau wote ambao wamefanikisha jitihada za kuanzisha mradi huu wilayani Mkinga. Shirika la Water Missions International Tanzania,lilianza kufanya kazi nchini mnamo mwaka 2013, likiwa limejikita katika kuendesha miradi ya kuondoa kero ya maji kwenye jamii ,sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu miradi ya maji.Hadi kufikia sasa shirika limefanikisha miradi ya maji katika mikoa zaidi ya 6 nchini,ikiwemo mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Kagera na Tanga. Ofisi za makao makuu ya Water Missions International Tanzania nchini yapo jijini Dar es alaam na ndipo inaporatibiwa miradi yote ya maji inayoendeshwa na shirika nchini .Tanzania ni nchi ya 10 kuwa na miradi ya shirika hili.Baadhi ya nchi nyingine linapoendesha miradi ya maji ni Kenya, Uganda, Malawi, Haiti, Honduras, Mexico, Peru, na Belize.↧