Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21888 articles
Browse latest View live

TFF YAKUBALI UENYEJI KAGAME CUP

$
0
0
TAREHE 10 MEI 2015

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, leo hii imekubali kuwa wenyeji wa  michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya Vilabu maarufu kama CECAFA Kagame Cup.

CECAFA ambao ndio wamiliki wa mashindano haya watatoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki na wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo.

Michuano hii inatarajiwa kuafanyika nchini kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

-- 
Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
T: +255 22-2861815  I F: +255 22-2861815  I C: +255 713 455970 
A:I P.Oa.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania  
 


STARTIMES YATEMBELEA NA KUTOA MSAADA WANAFUNZI UHURU MCHANGANYIKO

$
0
0


Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi msaada wa vyakula mbalimbali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam, Bi. Anna Mshana (kushoto). Kampuni hiyo ilitembelea na kutoa msaada wa vyakula kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo ina kitengo kinachofundisha wanafunzi wenye ulemavu.




Msanii wa Bongo Flava na balozi mpya wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Nurdin Bilal au maarufu kama Shetta (kulia) akimkabidhi msaada wa vyakula mbalimbali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam, Bi. Anna Mshana (kushoto). Kampuni hiyo ilitembelea na kutoa msaada wa vyakula kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo ina kitengo kinachofundisha wanafunzi wenye ulemavu. Pamoja naye kutoka kushoto ni wafanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Elena Liu na Bw. Richard Yan.


Msanii wa Bongo Flava na balozi mpya wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Nurdin Bilal au maarufu kama Shetta akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo ilipotembelea na kutoa msaada wa vaykula kwa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam.




<!--[if gte mso 9]>

CHAMA CHA WANAWAKE WANASHERIA TANZANIA (TAWLA) CHAZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 TANGU KIANZISHWE

$
0
0

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chama cha Wanawake Wanasheria  Tanzania (TAWLA),  Margareth Ringo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa, katika  maadhimisho ya miaka 25 ya kujengea uwezo na kufanya uchechemuzi juu ya haki ya wanawake. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile na Mjumbe wa Baraza la TAWLA, Annmarie Mavenjina.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile (kulia), akizungumza katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Mweka Hazina wa TAWLA, Asina Omari, Mjumbe wa Baraza la TAWLA, Annmarie Mavenjina na  Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chama cha Wanawake Wanasheria  Tanzania (TAWLA),  Margareth Ringo.
 Mkutano ukiendelea.
 Maofisa wa TAWLA wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Mratibu wa maswala ya Wanachama wa TAWLA, Josephiner Arnold (kushoto), akumuelekeza jambo Ofisa Habari wa TAWLA, Goodness Mrema wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Ukumbi wa YWCA Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
 Wanahabari wakichukua taarifa ya maadhimisho hayo.
  Wanahabari wakichukua taarifa ya maadhimisho hayo.
Wanahabari wakichukua taarifa ya maadhimisho hayo.

 Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wanawake Wanasheria  Tanzania (TAWLA) kwa kipindi cha miaka 25 kimetoa msaada wa kisheria kwa wanawake milioni tano katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Dodoma.

Hayo yalielezwa na Makamu Mwenyekiti wa Balaza la TAWLA, Margareth Ringo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika maadhimisho ya miaka 25 ya kujengea uwezo na kufanya uchechemuzi juu ya haki ya wanawake.

"TAWLA inajivunia mafanikio makubwa iliyopata ndani ya kipindi cha miaka 25 kimeweza kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake wasiopungua milioni tano kupitia vituo vilivyopo Dar  es Salaam, Tanga,Arusha na Dodoma" alisema Ringo.

Alisema pia wameweza kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa kutumia simu bila malipo kupitia namba 08007510101/0800110017.

Ringo aliongeza kuwa katika kuhakikisha jamii za pembezoni zinaweza kuifikia haki TAWLA imetoa mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria 402 katika wilaya 18 Tanzania ambazo ni Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Chamwino, Mpanda vijijini, Mpanda Mjini, Arumeru, Longido, Monduli, Arusha, Karatu, Muheza, Tanga, Kisarawe, Mvomero, Ilemela Magu na Ilala.

Alisema wasaidizi hao wamesaidia kuwafikia zaidi ya watu 10,500 waliokuwa na matatizo ya kisheria na pia namba kubwa zaidi wameweza kupata elimu ya maswala ya kisheria.

Aliongeza kuwa pamoja na kutoa msaada wa kisheri  wameweza kuihamasisha jamii juu ya masuala ya kisheria kupitia machapisho mbalimbali na vyombo vya habari na michezo ya kuigiza ambapo watu zaidi ya milioni 15 wamefikiwa.

Alisema chama hicho kimekuwa kikishiriki kutetea mabadiliko ya sheria kandamizi kwa wanawake na za kuwalinda, mchakato wa kupitisha kwa sheria ya mtoto na sheria ya makosa ya kujamiana, kuchangia uteuzi na ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi na kuwa chama hicho kina mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wakiwemo asasi zisizo za kiserikali, serikali kuu na za mitaa.

Ringo alisema katika kusherehekea mafanikio ya miaka 25 TAWLA kuanzia Mei 10 hadi 29 wanatakuwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji wa kuandika wosia na utaenda pamoja na uandikishaji wosia bila gharama kwa wale ambao watakuwa tayari katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Dodoma pamoja na kutoa msaada wa kisheria katika baadhi ya mikoa.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habari za jamii.com/)

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

MAGAZETI YA UDAKU LEO

MAGAZETI LEO JUMATATU TAREHE 11.5.2O15

LIVERPOOL YAIFANYIA CHELSEA KAMA AZAM ILIVYOWAFANYIA YANGA

$
0
0

liver chelsea
Na Richard Bakana-shaffihdauda.com.
Wachezaji wa klabu ya Liverpool jana katika mchezo wa ligi kuu ya England (EPL) walipokutana na mabingwa wapya wa ligi hiyo Chelsea waliwaonyesha heshima yao ya kubeba ubingwa, kitendo ambacho hata hapa Nyumbani Tanzania kwa mara ya kwanza kilionyesha na klabu ya Azam FC ambao waliwapigia makofi Yanga siku ya Jumatano timu hizo zilipokutana katika Uwanja wa Taifa.
YANGABINGWA4
Mchezo huo ambao ulipigwa Nyumbani kwa Chelsea ‘Stamford Bridge’ ulimalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kufungana bao moja moja.
Chelsea ndio walianza kupata bao kupitia kwa nahodha wake John Terry kunako dakika ya tano (5) lakini mkongwe wa Liverpool ambaye anataka kuikimbia timu hiyo Steven Gerrard akasawazisha bao hilo katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na kufanya timu hizo kugawana pointi moja moja na goli 1-1.
chelsea
Gerrard alitumia mchezo huo kuwaaga mashabiki wake ambapo alipotoka Uwanjani dakika za mwisho mwisho za mchezo huo, alienda katika upande wa mashabiki wa Chelsea na kuwapungia mkono na wao wakaonyesha heshima kwa kusimama na kumpigia makofi hari kadharika kwa mashabiki wa Liverpool.
gertard fans
Nguli huyo ambaye maisha yake ya soka yalianzia hapo hapo Liverpool akiwa na miaka nane sasa baada ya msimu huu kumalizika anatarajia kutimkia nchini marekani kumalizia soka lake la uzeeni.
gerard liver

Tuma Maoni


RAIS KIKWETE KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA YAKE RASMI NCHINI ALGERIA

$
0
0

3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.

5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah akiwasili katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers kwa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na kikundi cha utamaduni katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mabalozi wa nchi za Kiafrika katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. PICHA NA IKULU


MANCHESTER CITY YAICHAPA QPR BAO 6 NA KUITEREMSHA DARAJA

$
0
0

Man City imeitwanga QPR kwa mabao 6-0 na kuiteremsha daraja rasmi.
QPR ina pointi 27, imebakiza mechi mbili, iwapo itashinda zote itafikisha pointi 33.
Maana yake itakuwa imeshindwa kujiondoa katika nafasi mbili za kuteremka daraja kwa kuwa Hull City ina pointi 34 na iko katika nafasi ya 18 ambayo pia ni ‘denja’.
Man City XI: Hart 6, Zabaleta 6.5, Demichelis 6, Mangala 7, Kolarov 7, Fernando 6.5, Milner 7 (Navas), Fernandinho 6.5 (Toure 6), Lampard 6.5 (Bony 6.5), Silva 7.5, Aguero 8
Subs not used: Caballero, Sagna, Kompany, Dzeko
Manager: Manuel Pellegrini 7 
QPR XI: Green 5.5, Caulker 4.5, Dunne 5, Hill, Phillips 5, Barton 5, Henry 5.5, Suk-Young 4.5 (Wright-Phillips), Fer 5 (Kranjcar 6), Zamora 4 (Hoilett 6), Austin 6
Subs: McCarthy, Furlong, Grego-Cox, Comley
Manager: Chris Ramsey 4
Referee: Mike Dean - 6
10May2015

CHELSEA WATOKA SARE NA LIVERPOOL,GERRAD AAGA RASMI

$
0
0

STEVEN GERRARD AMEIFUNGIA LIVERPOOL BAO LA KUSAWAZISHA NA KUFANYA MATOKEO YAWE 1-1 DHIDI YA CHELSEA. NDIYO BAO LAKE LA MWISHO AKIICHEZEA TIMU YAKE, PIA BAO LAKE LA MWISHO KATIKA UWANJA WA STAMFORD BRIDGE MAARUFU KAMA DARAJANI.GERRARD ANAONDOKA LIVERPOOL MWISHONI MWA MSIMU HUU KWENDA ZAKE LA GALAXY YA MAREKANI.HATA HIVYO BAO HILO HALIJAISAIDIA LIVERPOOL, KWANI INAONEKANA IMEKOSA NAFASI YA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA ULAYA, MWAKANI.










Article 2

$
0
0

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU JOHN NYERERE DAR



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John  Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati alipowasili  nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. 
Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati  alipowasili nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere.  Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo cha msiba wa marehemu John Nyerere, wakati  wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John anatarajia kuzikwa  keshokutwa nyumbani kwao Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waombolezaji nyumbani kwa Mama Maria  Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani 
kwao Butiama. Picha na OMR

SHIGONGO AZINDUA VITABU VYAKE VITATU VIPYA KATIKA OFISI ZA GLOBAL

$
0
0



MHAMASISHAJI na mjasiriamali wa kimataifa, Eric James Shigongo, amewaasa Watanzania kutokata tamaa katika kufuatilia ndoto zao huku wakiamini kuwa wao ni watu muhimu katika maisha yao na ya jamii.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo ndani ya ofisi za Global Publishers zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar katika uzunduzi maalumu wa vitabu vyake vitatu, Shigongo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kusoma vitabu ili kupata maarifa mengi ya juu ya mafanikio maishani.

 “Kila mmoja ana ndoto za kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kuondoka mahali alipo. Wengi hushindwa kupiga hatua za mafanikio maishani kwa sababu nyingi yakiwemo mazingira waliyokulia wakiaminishwa kuwa hawawezi kufanya chochote maishani,  jambo ambalo si la kweli kwani kila mmoja anaweza kufikia ndoto zake akiamua tu kubadili fikra na namna ya kutenda mambo maishani,” alisema Shigongo.

Vitabu vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni  ’26 Secrets – How to Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.

Uzinduzi wa vitabu hivyo ni kuashiria kwake kuingia rasmi mitaani na kusambazwa kwenye kona mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo vinatarajiwa kubadilisha maisha ya maelfu ya wasomaji watakaofanikiwa kupata siri za mafanikio.
Mkurugenzi wa Global Publishers LTD, Shigongo Eric James (kulia), akishikilia vitabu vyake baada ya kumpatia jukumu la uzinduzi huo Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Kampuni hiyo, Oscar Ndauka. Tukio hilo limefanyika mapema leo ndani ya jengo la ofisi za GlobalPublishers zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia), akiwa amenyanyua moja ya vitabu hivyo baada ya zoezi la kukata utepe wa uzinduzi kukamilika.  Katikati ni mtunzi wa kitabu hicho, Shigongo Eric James na Oscar Ndauka, wote wakiwa wamenyanyua vitabu hivyo. Vitabu vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni  ’26 Secrets – How to Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Shigongo akimkabidhi jukumu la kukata utepe Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa Oscar Ndauka (wa kwanza kushoto) huku Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Abdallah Mrisho anashuhudia zoezi hilo.

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYANI HAI.

$
0
0



Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni ukanda wa chini wilayani Hai.
Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani Hai.
Meneaja wa NMB kanda ya kasakazini Vicky Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa wilya ya Hai,Anthony Mtaka huku zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe.
DC Mtaka,Mbunge Mbowe na Meneaja wa NMB ,Bishubo wakifurahia msaada huo.

ANGALIA PICHA YA SHOW YA YAMOTO BAND ILIYOFANYIKA DODOMA UKUMBI WA MATHEI LOUNGE

THE GOVERNMENT OF TANZANIA EXPANDS ITS NEW BIRTH REGISTRATION SYSTEM TO MWANZA

$
0
0

 
Baby Veronica being registered
Baby Veronica being registered.
The new system is set to drastically increase the number of children under 5 with birth certificates.

The Deputy Minister of the Ministry of Constitutional and Legal Affairs of the United Republic of Tanzania, Honorable Ummy Ali Mwalimu, launched today in Mwanza the new simplified birth registration initiative for children under-five in Tanzania. The event took place in Mwanza, the second largest city in mainland Tanzania. Mwanza will be the second region, after Mbeya, to benefit from the new, easily accessible and free birth registration system which is set to register over 400,000 children under-five by December 2015.

This new birth registration system, which is being supported by a generous contribution from the Government of Canada through the Department of Foreign Affairs, Trade, and Development, was first field tested in 2012 in Temeke, the largest district of the city of Dar es salaam and in 2014 was officially launched in Mbeya. According to the Acting Chief Executive Officer of RITA, Ms. Emmy Hudson, this simplified system marks a significant shift in accelerating birth registration in Tanzania after years of stagnation.

“RITA has embarked on several initiatives to improve birth registration in Mainland Tanzania, especially to newborn babies to ensure that each baby is captured and registered shortly after birth and closest to home. Through this initiative we see this dream realized and thank our development partners for unwavering support. Temeke and Mbeya have set good examples and we hope to register even better results in Mwanza.”


The 2010 Tanzania Demographic and Health Survey showed that only 16 per cent of children in Tanzania under the age of five were registered with civil authorities, and only about 8 per cent have a birth certificate.[1] Registration in Zanzibar is much more widespread than on the mainland with 78.7 per cent of under-fives registered (63 per cent with a certificate) versus 14.6 per cent registered (6.2 per cent with a certificate) on the mainland.
Prior to the roll-out of the Birth Registration Initiative in Mbeya it was estimated that only 8.7 per cent of the under-five population had a birth certificate. In less than two years after the roll-out, Mbeya saw approximately a 48 per cent increase and now it is estimated that nearly 56 per cent of under-fives in Mbeya have a certificate.

[1] See Tanzania Demographic and Health Survey (2010), pg. 27.
[2] Ibid. and See p.28, Table 2.11 Birth Registration for Children Under Five
Baby Veronica and her Birth Certificate
Baby Veronica and her Birth Certificate.
The new decentralized birth registration and certification system capitalizes on the existing health infrastructure and personnel to register newborn babies soon after birth or within 12 months when visiting health facilities for vaccinations. Registration information is uploaded using mobile phone technology to a centralized data-base resulting in real-time data availability, and a certificate is issued the same day.
This new birth registration and certification system will be operational in Mwanza soon after today’s launch. With financial support from the Canadian Government, this new system will also be rolled out over the next five years to ten additional regions, namely, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera, Kigoma and Dodoma.
Paul Speech
UNICEF Tanzania Deputy Representative, Paul Edwards.
UNICEF Tanzania Deputy Representative, Paul Edwards, commended the Government of Tanzania for its commitment to prioritizing child rights and reaffirmed UNICEF’s commitment and support towards making birth registration and certification a reality for all children.
“With this initiative RITA has taken an important step towards facilitating birth registration. Registration Assistants are now able to upload information instantly over mobile phones, making data available in ‘real time.’ This type of information is crucial in planning for Tanzania’s future. And it goes without saying that the certificate itself provides protection for children - proof of age informs the State as to who is a child, and provides protection against the exploitation of children and child marriage.”
Tigo Lake Zone Director, Ally Maswanya said: “The support provided by Tigo towards this initiative is in line with the company’s corporate social responsibility strategy which aims at empowering community with information and communication technology tools such as mobile phones. The under-five birth registration initiative demonstrates our commitment as telecommunication experts and attests the potential of mobile technology in development programs.”
The VSO Country Director Jean Van Wetter praised the strong partnership between Government, UN, private sector and civil society: “Birth registration is fundamental to guarantee child rights and further improve the social services delivery system in the country.”

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYANI HAI.

$
0
0

 
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni ukanda wa chini wilayani Hai.
Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani Hai.
Meneaja wa NMB kanda ya kasakazini Vicky Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa wilya ya Hai,Anthony Mtaka huku zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe.
DC Mtaka,Mbunge Mbowe na Meneaja wa NMB ,Bishubo wakifurahia msaada huo.
Msaada mwingine uliotolewa ulikuwa ni wa Blankets.
Chakula pia kilitolewa kwa wahnga hao.
Meneaja wa NMB,Vicky Bishubo akiwa na wahanga wa mafuriko .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Benki ya NMB imetoa msaada  wa kibinadamu wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 baada ya kutembelea  eneo la tukio na kujionea athari kubwa zilizosababishwa na mafuriko hayo.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo,alitoa pole kwa familia zilizofikwa na kadhia hiyo huku akisema NMB imeguswa na tukio hilo na kwamba inatoa msaada
katika maeneo matatu.

Alisema eneo la kwanza la msaada ni chakula ambapo imetoa unga kilo 
2,000,Maharage Kilo 500,Sukari Kilo 500 na mafuta ya kula lita 1,000.

Eneo jingine ni eneo la malazi ambapo yametolewa Magondoro 70,Mablangeti 100,pamoja na marobota ya nguo huku pia Benki hiyo ikichangia mifuko 50 ya Sementi kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Elerai iliyofikwa pia na mafuriko.

“Tumesikitishwa na majanga yaliowakuta,NMB tumekuwa na desturi ya kurudisha faida yetu katika jamii kwa kusaidia majanga mbalimbali hivyo tumetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi
milioni 10”alisema Bishubo

Nao baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo waliishukuru NMB kwa msaada huo na kutoa rai kwa watu,mashirika na taasisi mbalimbali zilizo za kiserikali na zisizo za serikali kuona umuhimu wa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kutoka na adhari ziliwakumba.

Mwisho.

MAGAZETI LEO JUMANNE

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUEPUKA LUGHA ZA CHUKI

$
0
0
       

Meza kuu.
(Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog).
Mshehereshaji wa Semina Bi. Rose Mwalongo akiwakaribisha washiriki wote waliofika kwenye semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of women in radio and television (AWRTT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika.
Bi. Rose Haji Mwalimu kutoka IAWRT Tanzania akifungua semina kwa kwa washiriki ambao walikuwa ni wanahabari (hawapo pichani) mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika wa pili kutoka kushoto ni Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare, wa pili kutoka kulia ni Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen pamoja na Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN).
Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare akitoa semina kwa wanahabari namna ya kusimama katika ukweli na uwazi na pia kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii, na baadae kusababisha machafuko kwenye Uchaguzi mkuu wa 2015.
Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen kutoka ubalozi wa Norway akiwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa makini kipindi chote wanapochukua au kutafuta taarifa ili kuondoa vurugu kwa nchi hasa Tanzania inayotegemea kufanya uchaguzi mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN), Aidan White akitoa semina kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi mazuri ya uandishi hasa kwenye hiki kipindi cha Uchaguzi.
Baadhi ya washiriki wa semina.
Rais wa Shirikisho la waandishi wa Habari Afrika (FAJ), Mohamed Garba.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Bi. Imelda Lulu Urio akielezea kuhusu vyombo vya habari vya Tanzania vilivyoanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia maana zinaleta chuki kwa taifa hasa suala la udini ambalo limeonekana kushika kasi hapa chini Tanzania.
Bi. Irene Burungi Mugisha kutoka IAWRT nchini Uganda akizungumza jambo.
Wadau wakifuatilia mada kwa umakini.
Mhariri mkuu wa gazeti la The New Times la nchini Rwanda, Bw. Kennedy Ndahiro akitoa mada kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari waliohudhuria kwenye semina ya matumizi mazuri ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu.
Rais wa Umoja wa waandishi nchini Uganda, Bi. Lucy Ekadu akiwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika utoaji wa habari katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu na pia kutoa elimu ya msingi kwa wanahabari ili kutochochea vurugu.
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Ayoub Rioba akitoa semina kwa washiriki (hawapo pichani) akiwasilisha mada yake kwenye semina iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar.
Mshiriki Borry Mbaraka akiuliza swali kwa watoa mada.
Rais wa IAWRT, Bi. Rachael Nakitare (wa tatu kutoka kushoto) akiuliza swali kwa mtoa mada (hayupo pichani).
Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe akiwasilisha mada yake kwa wanahabari(hawapo pichani).
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa mmoja wa watoa mada wakati wa semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Peacock jijini Dar.
Mweka hazina kutoka IAWRT Tanzania, Razia Mwawanga akikazia jambo kwenye semina ya wanahabari.

Wadau wakifuatilia kwa umakini mada.
Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu
Ikiwa Tanzania inajiandaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, waandishi wa habari nchini wameaswa kujiepusha na lugha za chuki pamoja na uchochezi kipindi chote cha uchaguzi jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko kama inavyoonekana katika nchi mbalimbali barani Africa na duniani.
Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network (EJN) ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika mashariki kwa lengo la kujadili masuala yanayohusiana na lugha za chuki kwa vyombo vya habari vya Afrika pamoja na madhara yake kwa wananchi.
Akifungua warsha hiyo mgeni rasmi ambaye ni Raisi wa shirikisho la wanahabari Africa (FAJ) Bw. Mohamed Gabra amesema kuwa moja ya mambo ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko makubwa katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla ni lugha zinazotumika na wanahabari wakati wakiripori baadhi ya habari lugha ambazo amesema kuwa zimekuwa zikileta chuki baina ya watu na mwisho wake kusababisha madhara makubwa ambayo yangeweza kuepukika kama hatua zingechukuliwa mapema.
Ametolea mifano kwa nchi kama Rwanda, Kenya, na nchi nyingine za ulaya ambazo zimewahi kuingia katika machafuko ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi kutokana na vyombo vya habari pamoja na wanahabari wenyewe kutumia kalamu zao kuwajengea chuki wananchi na mwisho kusababisha kuibuka kwa machafuko makubwa.
Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya uchaguzi mkuu kwa mafanikio na amani ni lazima wanahabari wahakikishe kuwa wanasimama kwenye ukweli na kuhakikisha kuwa wanawaambia wananchi kile ambacho kinatokea na sio kujenga na kutengezeza maneno ambayo mwisho yatasababisha chuki kwa watanzania.
Awali akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Rais wa (IAWRT) Bi. Rachael Nakitare amesema kuwa ni lazima kipindi hiki cha Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu ni kipindi cha wanahabari kusimama katika ukweli,uwazi na kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii,na baadae kusababisha machafuko.
Baadhi ya watu waliotoa mada katika warsha hiyo ni pamoja na wakili na Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi. Imelda Lulu Urio ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea jinsi vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia mambo hayo ili kuepuka mambo makubwa ambayo yanaweza kujitokeza hapo baadae.
Wengine waliopata nafasi ya kuchangia katika warsha hiyo ni mwandishi mkongwe nchini ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk. Ayoub Rioba ambapo amesema kuwa katika chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika kwa sasa wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wanahabari kutaka kujinufaisha wao kisiasa bila kujali madhara ambayo yanaweze kutokea endapo wanahabari watakiuka maadili ya taaluma zao.
Baadhi ya wanahabari kutoka mataifa ya nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda,wamesema kuwa hakuna tofauti kubwa sana kati ya ufanyaji wa kazi za wanahabari zinazofanywa nchini Tanzania na mataifa yao bali tofauti iliyopo ni sheria zinazowaongoza wanahari katika mataifa hayo.

Serikali yatakiwa kuhimiza wananchi kushiriki upigaji kura Uchaguzi Mkuu

$
0
0
              

Kulia mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
Kulia mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa.
Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa.
Kushoto mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers).
Kushoto mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) wakiwa katika semina hiyo.
washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
Na Joachim Mushi,
WANAHARAKATI Ngazi ya Jamii nchini wametoa madai kuelekea Uchaguzi Mkuu huku wakiiomba Serikali iharakishe mchakato wa uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura ili vijana wengi wanaostahili waweze kuitumia haki yao ya msingi ya kushiriki mchakato wa uchaguzi na ule wa kura ya maoni.
Madai hayo yametolewa katika tamko lao lililotolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) kwenye warsha ya majadiliano kati ya waandishi wa habari, wachora katuni na waandishi wa habari za mitandao ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Katika madai hayo wanaharakati ngazi ya jamii pia wameomba elimu ya uraia na ya mpiga kura itolewe kwa wingi ili iwafikie vijana wapate hamasa ya kujitokeza kugombea na kupiga kura, ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waweze kupata nafasi sawa kama wagombea kwenye uchaguzi bila upendeleo wala woga.
Aidha imetaka vijana wanaojitokeza kama wagombea wawekewe mazingira rafiki ikiwezekana wapewe ruzuku ya kuwasaidia kushindana kwenye uwanja wa demokrasia, pamoja na kushauri Sera ya Taifa ya Vijana pamoja na Mkataba wa Vijana wa Afrika unalitambua kundi la vijana kama rasilimali mojawapo muhimu sana kwenye maendeleo na pia katika kulinda amani na utulivu kwenye Bara la Afrika.
“…Hata hivyo pamoja na kwamba vijana ni zaidi ya 60% bado mchango na thamani ya vijana haujatumika ipasavyo kwenye demokrasia ya Tanzania, huku thamani yao ikionekana tu nyakati za uchaguzi kwa kutumiwa kama walinzi au wapambe wa wagombea,” imeeleza sehemu ya tamko hilo.
Limebainisha kuwa pamoja na uanzishwaji wa Mabaraza ya Vijana kwa vyama vingi, mengi hayana nguvu ya maamuzi kwa kuingiliwa na vyombo vya juu vya Chama, ikiwa ni pamoja na kukumbusha kuwa mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka ambao vijana wengi waliingia Bungeni na wamekuwa chachu kubwa ya kuchangia na kuibua mijadala yenye tija Bungeni.
Hata hivyo imeeleza kuwa bado idadi ya vijana wanaojitokeza kupiga kura hasa wasichana bado ni ndogo ukilinganisha na ile ya wanaojiandikisha na wanaoshiriki kwenye kampeni, vijana wengi wanaojitokeza kwa kuweka nia ya kugombea wamekumbana na kigingi cha uteuzi kwa kutokubalika ndani ya vyama kwa mawazo mgando kwamba umri wao hauwawezeshi kufanya uchambuzi wa masuala makubwa ya kitaifa, kadhalika changamoto ya nguvu yao ndogo kiuchumi ajira ambayo inawafanya wasiweze kushindana kikamilifu katika uwanja usio na usawa wa siasa.
Kwa upande wa vyama vya siasa tamko hilo limetaka watu wenye ulemavu waingizwe kwenye sera na mipango ya nchi kwa vitendo kwani bado ushiriki wao kwenye masuala ya uchaguzi na uongozi uko chini.
Madai mengine ni pamoja na Vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kuhakikisha zinazingatia ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye uchaguzi kama wagombea na wapiga kura, Serikali kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu ili washiriki kikamilifu kwenye michakato yote ya maendeleo, hii ni pamoja na uchapishaji wa sheria na kanuni kwa lugha rahisi ikiwemo maandishi ya nukta nundu, vituo rafiki vya kampeni na kupiga kura kwa watu wenye ulemavu.
Mengine ni pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi, kudai ulinzi na usalama wa maisha yao, kama raia wa taifa hili, uwepo wa mikakati ya kuelimisha umma uondokane na mawazo potofu yanayoashiria kutishia uhai na usalama wa kundi hili na hasa wenye ulemavu wa ngozi. Hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaohusika.
“…Serikali ihakikishe upatikanaji wa taarifa na maarifa kwa njia rahisi ikiwemo lugha ya alama na maandishi ya nukta nundu kutoa elimu ya mpiga kura na pia vyombo vya habari kama vile TV ziweke wakalimani hasa katika vipindi vya taarifa ya habari na vipindi vyote vyenye mijadala ya kitaifa. Mgombea tutakayempa kura ni Yule ambaye miongoni mwa sera zake itakua ni kupinga ukatili wa kijinsia kwa hali zote bila woga wala upendeleo
Aidha mengine ni pamoja na Serikali itakayoingia madarakani kuhakikisha inaunda Tume ya Kughulikia Ukatiki wa Kijinsia kama zilivyo Tume nyingine, kuunda mahakama maalum ya kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia ngazi ya familia na kuweka mikakati halisi ya kuhakikisha kwamba kila mwanamke ana haki ya uchumi na haki ya maisha endelevu/ajira akiwa kijijini au mjini, mwenye ulemavu, mzee au kijana, wanawake na wanaume wote wapate kipato kinachotosheleza kuishi maisha bora kama binadamu.
Warsha hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) imejumuisha makundi mbalimbali ya wanahabari ikiwa ni lengo la kuwajengea uwezo kuandika masuala ya kijinsia kwa kina.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai

$
0
0
      

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015
Viewing all 21888 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>