Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21933 articles
Browse latest View live

MAN U YAKUBALI KICHAPO CHA MAGOLI 3 KWA 0 KUTOKA LIVERPOOL

$
0
0



Steven Gerard alifunga mikwaju miwili ya penalty na kukosa wa tatu huku timu Liverpool ikiendelea kuimarisha matokeo yake baada ya kuwacharaza mabingwa wateteza wa ligi ya uingereza Machester United tatu bila katika uga wa nyumbani Old Trafford.
Katika kile kilichoonekana kama harakati za kushinda taji lao la kwanza tangia mwaka 1990,Liverpool ilipita mtihani wao kwa kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya timu ya Manchester United ambayo haikuweza kuwadhibiti wapinzani wao na hivyobasi kusogea hadi nafasi ya pili na pointi nne nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.

Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.

Kutokana na mechi hizo za leo Chelsea iko katika nafasi nzuri ya kushinda taji hilo kwa alama 66 ikiwa imecheza mechi 30 huku timu za liverpool na Arsenal zikiwa na pointi 62 kila mmoja, lakini liverpool inashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.

Arsenal ni ya tatu huku Manchester City iliocheza mechi 27 ikiwa na pointi 60 na hivyobasi ikifunga udhia wa time nne bora.

Viongozi wa Barclays Africa Group walivyotembelea nchini.

$
0
0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Malawi nchini, Bi.  Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga wakati wa mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa Kundi la Barclays  Afrika (the Group),  wakitembelea nchini, jijini  Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Ofisa Mkuu Vihatarishi (Risk) wa Barclays Afrika, Anil Hinduja.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kulia) akisalimiana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi & Cotex, Lakshmi Narayan wakati wa  mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa Barclays  Afrika, wakitembelea jijini  Dar es Salaam. Katikati ni baadhi ya maofisa wa NBC, Daniel Kaila (wa pili kushoto) na Azza Ernest Mnzava.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Huduma  Rejareja za Kibenki wa NBC, Mussa Jallow  katika mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa  Barclays  Afrika, wakitembelea nchini.. Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr Hussein Kassim na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi & Cotex, Lakshmi Narayan.   
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu (kushoto) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika mkutano huo jijini Dar esd Salaam.
 Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC Tanzania, Maharage Chande (kulia), akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nyanza Mines, Mukesh Mamlani  wakati wa mkutano huo  jijini  Dar es Salaam.  Katikati ni baadhi ya maofisa wa NBC, Godfrey Nderingo (wa pili kushoto) na Cletus Shirima. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) akiwa na wageni wengine katika mkutano huo. Kundi la Barclays Afrika ‘the Group’, limetokana na kuunganishwa kwa Kundi la ABSA ya Afrika Kusini (ABSA Group Ltd) na sehemu kubwa ya shughuli za Benki ya Barclays barani Afrika hapo Juni 31, 2013. ABSA (sasa the Group) ikimiliki asilimia 55 ya hisa ndani ya NBC, serikali ya Tanzania asilimia 30  zinazobaki zikimilikiwa na mashirika ya fedha ya kimataifa.

Mtandao wa Wanawake na Katiba Walipongeza Bunge la Katiba Kuonesha Usawa wa Jinsia

$
0
0


MTANDAO wa Wanawake na Katiba wenye mashirika zaidi ya 50 yanayotetea haki za wanawake katika Katiba mpya, umelipongeza mchakato na matokeo ya  uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Bunge Maalum la Katiba (Mwenyekiti na Makamu wake) ambao umezingatia usawa wa jinsia.

Kauli hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao kwa niaba ya Mtandao wa Wanawake na Katiba jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa licha ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Mwaka 2012 haikuanisha kuwa uchaguzi wa uongozi wa Bunge hili uzingatie usawa wa jinsia bunge hilo limeona umuhimu huo.

“…Tumetambua busara na hekima za wajumbe za kuonyesha nia ya kujenga msingi wa usawa wa jinsia katika uongozi na vyombo vya maamuzi nchini. Kwetu sisi, hili si suala la uwepo wa mwanamume na mwanamke katika uenyeketi  wa Bunge Maalumu tu, bali pia ni ukomavu wa kipekee wa wajumbe katika kuuona ukweli kuwa suala la kuimarisha sauti za wanawake na wanaume ni nyeti sana, haswa wakati wa ujenzi wa maridhiano muhimu kikatiba,” alisema Liundi.

Tunawapongeza waliochaguliwa ambao ni Mhe. Samweli Sitta (Mwenyekiti) na Mhe.  Samia Hassan Suluhu (Makamu Mwenyekiti) kwa kuaminiwa katika nyadhifa hizo muhimu.  Mtandao wa Wanawake na Katiba  unatambua uwezo wao katika utendaji na una matumaini makubwa kuwa pamoja na mengine mengi watakayoyasimamia, watatoa uongozi ulio imara na wenye weledi wakati wakiongoza Bunge hili katika kujadili na kupitisha misingi muhimu itakoyopelekea katika ujenzi wa usawa wa kijinsia nchini.

Alisema mtandao huo unategemea kuona usawa wa jinsia ndani ya Katiba mpya, ambao sio ule tu wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika  ngazi mbalimbali, lakini pia usawa ulio na nia ya kujenga misingi ya kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi walio wengi na haswa wanawake nchini.

“…Kwa mtazamo huu, tunatarajia kuwa busara za Wenyeviti hawa na washauri wao zitatumika pia kuzingatia usawa wa kijinsia  katika Kamati zitakozoundwa pamoja na kuwa kuzingatia ustadi na uzoefu wa wanakamati unahitajika. Nia kubwa ikiwa kuona wanawake kwa wanaume watatoa sauti zao kuhakikisha na kulinda, pamoja na mengine, uzingatiwaji wa usawa wa jjinsia katika vifungu vyote vya Katiba mpya.

Aidha alifafanua kuwa Mtandao wa Wanawake na Katiba, unawapongeza wajumbe wote wanawake kwa umoja wao, mshikamano na ushirikiano imara, ambao umeleta mafanikio makubwa katika michakato inayoendelea huko Dodoma kwenye Bunge Maalumu.
“…Huu ni mwanzo wenye kuonyesha mifano mizuri, na ambao tunapenda  kuuona ukiendelezwa na kusimamiwa imara wakati wote Bunge Maalumu litakapokuwa likifanya kazi yake ya kuchambua na kupitisha vifungu mbalimbali vya Katiba,” alimalizia Bi. Liundi.

RIDHIWANI KIKWETE ADHAMIRIA KUWAKOMBOA WANA CHALINZE

$
0
0

Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Kwamsanja,wakati alipofika kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwaomba kura katika Uchaguzi huo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa Wanachalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang'ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 16,2014.

Wananchi Rukwa Waunga mkono Serikali Kutenga Bajeti Maalum Kukabiliana Vifo vya Uzazi

$
0
0

Daktari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, John William Gurisha akitoa takwimu za afya ya Uzazi Mkoani Rukwa katika maadhimisho hayo. Daktari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, John William Gurisha akitoa takwimu za afya ya Uzazi Mkoani Rukwa katika maadhimisho hayo.Washiriki anuai kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha za matukio. Washiriki anuai kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha za matukioBaadhi ya washiriki wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya Utepe Mweupe. Baadhi ya washiriki wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya Utepe MweupeMkurugenzi Mkazi wa Shirika la Evidence for Action Tanzania, Craig John Ferla, kupitia kampeni ya Mama Ye akichangia damu.Zaidi ya chupa 970 za damu zilipatikana katika maadhimisho ya wiki ya utepe mweupe. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Evidence for Action Tanzania, Craig John Ferla, kupitia kampeni ya Mama Ye akichangia damu.Zaidi ya chupa 970 za damu zilipatikana katika maadhimisho ya wiki ya utepe mweupe.

  ZAIDI ya wananchi 16,828 wa Mkoa wa Rukwa wamesaini ombi la haki (petition), wakiiomba Serikali kutenga bajeti mahususi ili kuviinua vituo vya afya nchini viweze kutoa huduma za dharura kwa za uzazi ikiwemo upasuaji, damu salama, vifaa vya kutosha na wafanyakazi wenye ujuzi. Taarifa hiyo imetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay jana mjini hapa mbele ya mgeni rasmi wa siku ya Utepe Mweupe ambaye ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda. 

 “Lengo ni kuhakikisha bajeti ya kutosha inatengwa na Serikali Kuu pamoja halmashauri ili kuhakikisha kuwa angalau asilimia 50 ya vituo vya afya nchini vinatoa huduma za dharura za uzazi,” alisema Mlay. Kwa Upande wake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika ujumbe wake ameziagiza mara moja halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya kutosha ili kuimarisha vituo vya afya viweze kutoa huduma za dharura za uzazi ikiwamo upasuaji lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

 Tamko hilo lipo katika hotuba ya Waziri Pinda iliyosomwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akimwakilisha Waziri Mkuu. Katika maelezo yake Waziri Pinda alisema vifo vya mama na mtoto baado ni changamoto nchini hivyo Serikali ina kila sababu ya kukabiliana na changamoto hiyo. 

 Aliongeza kuwepo kwa huduma hizo na watalaamu kwenye vituo vya afya na hospitali nchini, ni njia pekee itakayosaidia kupunguza vifo hivyo. “Kila mwaka karibu wanawake milioni sita hupoteza maisha ulimwenguni kote wakati wa kujifungua, asilimia 50 ya wanawake hawa wanatoka kusini mwa Jangwa la Sahara na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizo kwenye ukanda huu."

UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA:Matokeo ya Awali yasiyo rasmi kutoka vituo mbalimbali yaonesha ccm kuongoza

$
0
0

  
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wafuasi wa chama hicho usiku huu,kwenye Ofisi za CCM mkoa,huku wakisubiri matokeo rasmi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda wowote kuanzia sasa.
TOSA no.1 
CCM 98 ,Chadema 20, CHAUSTA 0
Ipamba no2. CCM 104, Chadema 10,CHAUSTA 0
Isakulilo CCM 83,Chadema 8,CHAUSTA 0

Kilindi A CCM 69 ,Chadema 23, CHAUSTA 0
Ofisi ya Kijiji(Kilindi) CCM 117, Chadema 53, CHAUSTA0
Zahanati  CCM 117,Chadema 67, CHAUSTA 1
Ifunda
Kivalali A CCM 99 Chadema 19 CHAUSTA 0
Kivalali B CCM 109 Chadema 14, CHAUSTA 1
Muwimbi CCM164, Chadema 22 CHAUSTA 0

Mahanzi CCM 130 Chadema 46 CHAUSTA 0
Ikungwe A CCM 131 Chadema 23 CHAUSTA 0
Ikungwe B CCM 216 Chadema 13 CHAUSTA 0
Magunga CCM 184 ,Chadema 4 CHAUSTA1
Wasa CCM 149,Chadema 15 CHAUSTA 0
Usengelidete CCM 260,Chadema 46,CHAUSTA O
 KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA  SALIM ASAS AKICHEZA  KWA SHANGWE  VIWANJA  VYA CCM MKOA KUSHEREKEA  USHINDI  WA  CCM KALENGA

Matokeo ya Awali yasiyo rasmi baadhi ya vituo  inaongoza kwa mbali.

POLISI NCHINI MALYSIA WAFANYA UPEKUZI KATIKA NYUMBA YA RUBANI WA NDEGE YA MALYSIA ILIYOPOTEA JUMA MOJA LILILOPITA

$
0
0

Compound: A view of the entrance to Zaharie Ahmad's residence. Police have been stationed outside for the last week
Compound: A view of the entrance to Zaharie Ahmad's residence. Police have been stationed outside for the last week
Officers are said to have spent two hours searching the pilot's home today inside the luxury compound
Officers are said to have spent two hours searching the pilot's home today inside the luxury compound
Luxury: Shah is said to live at the property with his wife Faisa
Luxury: Shah is said to live at the property with his wife Faisa
In Shah's house a flight simulator has been set up and is understood to have interested police following up one line of investigation - that he had used the equipment to practice making his real-life Boeing 777 ‘invisible’ by turning off all communications.
Despite the investigation, Malaysian officials and friends of the pilots have told MailOnline this week that there are no reasons to suspect either the Captain or co-pilot of having personal problems that would have resulted in them taking control of the aircraft.

Mr Razak added authorities have not ruled out any possibilities in the international search for the plane, which now involves 14 countries, 43 ships and 58 aircraft.

'Clearly the search has entered a new phase. Over the last seven days, we have followed every lead and looked into every possibility,' Mr Razak said. 'For family and friends (of the passengers), we hope this new information brings us one step closer to finding the plane.'
Entrance: The gates outside the home of co-pilot Fariq Abdul Hamid who is also under police investigation
Entrance: The gates outside the home of co-pilot Fariq Abdul Hamid who is also under police investigation
Journalists gathered outside Hamid's home in Shah Alam as police turned their attention to those on board as part of the wide-ranging probe
Journalists gathered outside Hamid's home in Shah Alam as police turned their attention to those on board as part of the wide-ranging probe
Suspicions: Jonti Roos (centre) claims she and her friend were entertained by Fariq Abdul Hamid, 27, who is one of the pilots of the missing Malaysia Airlines flight (right). He is now part of an investigation by police in Kuala Lumpur
Suspicions: Jonti Roos (centre) claims she and her friend were entertained by Fariq Abdul Hamid, 27, who is one of the pilots of the missing Malaysia Airlines flight (right). He is now part of an investigation by police in Kuala Lumpur.

Today, a police van with a large contingent of officers inside passed through a security gate at the entrance to the wealthy compound where  father-of-three Captain Zaharie Ahmad Shah lives with his wife Faisa.

Four plain-clothed police officers were also, reportedly, seen at the home of the other pilot Fariq Abdul Hamid, 27.

Both pilots live in the upmarket Kuala Lumpur district of Laman Seri, about an hour's drive from the city centre - and each was visited today by a team of detectives who arrived in a white 'people mover' vehicle.
The homes are substantial and are, said one resident, typical of high income earners.

It is believed a team of search specialists entered Shah's house and spent two hours searching for signs of foul play, before moving into search the co-pilot's home a short distance away.

The New Straits Times reported last night that before police turned up at Hamid's home, his two brothers arrived there in a Mini Cooper, believed to belong to a friend.

They hurried into the house and remained there for a short time before hurrying away in the same car, taking with them transparent blue plastic bags containing clothes and toiletries.

Fariq's father, Abdul Hamid left with them. An hour later, the plain clothed officers left the house carrying two brown bags.

The concentration by police on the homes of the Captain and the co-pilot adds to suspicion that one - or both - of them might have had been  responsible for the plight of the aircraft.

WAANDISHI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI KWENYE KURIPOTI BUNGE LA KATIBA

$
0
0

DSC_0641
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan akifungua warsha ya siku moja kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya nafasi ya watetezi wa Haki za Binadamu katika Katiba mpya.

.waambiwa waache kamari ya majongoo kuhusu serikali mbili ama tatu
.watetezi wa haki za binadamu, waandishi watoswa kwenye rasimu ya Katiba

Na Damas Makangale, Dodoma, MOblog
WAANDISHI na Wahariri wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kuweka mbele maslahi ya taifa wakati wa kuripoti Bunge maalum la katiba. MOblog inaripoti.

Akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya watetezi wa haki za binadamu na asasi za kirai katika katiba mpya jijini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa kuzingatia weledi wa fani yao na maadili ya uandishi.

“waandishi wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa kuweka mbele maslahi ya taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta suluhu, amani, mshikamano na utulivu,” amesema.
DSC_0650
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Ndg. Onesmo Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la wabunge wa katiba na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa haki za binadamu katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku moja uliofanyika mjini Dodoma.

Amesema waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao wanaweza kushauri na kushirikiana na serikali na mamlaka zingine kupatikana kwa katiba mpya yenye tunu za taifa, Sululu aliongeza kwa kuweka hoja zao kwa ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta mshikamano na ushirikiano wa kitaifa katika kudumisha amani na haki za binadamu nchini. Amesema kwamba kupitia bunge la katiba wanahabari ni kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi na kuelimisha umma jinsi sheria na haki za binadamu zinavyoweza kulinda na katiba ya nchi.
DSC_0627
Mwezeshaji, Mwandishi wa Habari, Mwanasheria, msomi na mjumbe wa Bunge la Katiba Ali Uki akizungumza kwenye warsha hiyo.

“waandishi kwa kutumia nafasi yao wanaweza kushauri kwa kurekebishwa baadhi ya sheria, vifungu ili kuweza kulinda haki za binadamu nchini kwa kupitia bunge maalum la katiba,” aliongeza. Alisisitiza Mhe Sululu kwamba bunge la katiba halijadili kuhusu ama serikali mbili au tatu kwa sababu kuna mambo mengi kwenye rasimu ya katiba yakujadiliwa.

“kwa jinsi mnavyoripoti kuhusu serikali mbili ama tatu ni kama mchezo wa kamari ya majongoo jamani katiba siyo muungano tu,” amesema. Kwa upande, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo olengurumwa amesema ingawaje kwenye rasimu ya katiba hawajatambua watetezi wa haki za binadamu bali wataendelea kushauriana na wajumbe kupata mwafaka wa jambo hilo.
DSC_0629
Meza kuu, Ndg. Onesmo Olengurumwa akiwa na Mgeni rasmi Samia Suluhu Hassani kwenye warsha hiyo.

“Rasimu ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama zilivyoanishwa kikatiba,” amesema

Olengurumwa aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia haijatambua wasaidizi wa kisheria wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa msaada mkubwa kisheria kwenye ngazi za vijijini. Amesema ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua mjadala wa katiba ili misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya utetezi wa haki za binadamu nchini.

Olengurumwa amesema waandishi wa habari kama vile watetezi wa haki za binadamu maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na katiba ya nchi ili kujenga mazingira mazuri ya haki za binadamu nchini. Hivi karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa Serikali tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika. Mjadala wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma.

wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten hivi karibuni.
DSC_0637
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Nyamsenda amesema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume hiyo, ambayo haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu rasimu ambayo haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya wananchi na maoni yao.

Takwimu zinaonyesha kwamba kwa sasa asilimia 36% (kutoka asilimia 10% ya mwaka 2005)kwa Tanzania Bara wanaopata umeme ni asilimia 36% na asilimia 21% ya wanavijiji wa Bara wanatumia umeme hivi kutoka asilimia 2% ya mwaka 2005.Tayari tumevuka malengo ya CCM na ya Serikali

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
 Takwimu zinaonyesha kwamba  kwa sasa asilimia 36% (kutoka asilimia ile 10% ya mwaka 2005)kwa Tanzania Bara wanaopata umeme ni asilimia 36%  na asilimia 21% ya wanavijiji wa Bara wanatumia umeme kutoka hivi sasa kutoka asilimia 2% mwaka 2005.Tayari imevuka malengo ya CCM na ya Serikali ya asilimia 24% wameunganishwa.
Tuendelee kuchapa kazi kwa kasi na ubunifu mkubwa.
Waziri wa Nishati na Madini 
Profesa Sospeter Muhongo

KUTOKA VODACOM: VODACOM TANZANIA YATOA MSAADA YA MIAVULI 20 KWA JESHI LA USALAMA BARABARANI

$
0
0


Askari wa usalama barabarani Tumaini Kimambo akiambatana na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu,kuhifadhi miamvuli 20 iliyotolewa msaada na Vodacom Tanzania kwaajili ya kuwawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi,Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
  Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akifungua mmoja ya miamvuli(20)kabla ya kuikabidhi rasmi kwa Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa(kulia) msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa  akipokea msaada wa miamvuli(20)kutoka kwa Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi,wanaoshuhudia wa pili kutoka kulia ni Tumaini  Kimaro, Simoni Lugangila na Emmanuel David. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania,Bw. Matina Nkurlu(kushoto)akiongea mara baada ya kukabidhi msaada ya miamvuli(20)kwa Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa(kulia) msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa  akipokea msaada wa miamvuli(20)kutoka kwa Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi,wanaoshuhudia wa pili kutoka kulia ni Tumaini  Kimaro, Simoni Lugangila na Emmanuel David. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akimjulia hali na Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili Hospitali ya Mkoa wa Iringa Leo baada ya Kudai Kutekwa na Kuteswa, Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvandana Kampeni Meneja Wake ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Wakagua Vituo vya Kupigia Kura Kwa Helikopta

$
0
0

 Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili akiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo mbunge huyo alimwelezea  Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe(hayupo Pichani)namna alivyotekwa, kuteswa na watu aliodai kuwa ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha Chama Ch Mapinduzi (CCM), Green Guard.
 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akimjulia hali na kumsikiliza Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili akiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo mbunge huyo alimwelezea kiongozi huyo namna alivyotekwa, kuteswa na watu aliodai kuwa ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha Chama Ch Mapinduzi (CCM), Green Guard.

 Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee, namna ambavyo Mbunge Rose Kamili alikuwa akiendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.
 Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili lililotokea jana usiku katika Kijiji cha Kitawaya, Kaa ya Luhota, jimboni Kalenga, wakati alipokuwa akizungumza na mawakala wa CHADEMA, ambapo imedaiwa kitendo hicho kilifanywa na vijana wa ulinzi wa CCM.
 Helikopya ya Chadema iliyowabeba Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvanda akiwa na Kampeni Meneja wake, Godbless Lema akitua ambapo Godbless Lema na Grace Tendega walikua wakizunguka katika maeneo mbalimbali kuangalia shughuli ya upigaji kura vituoni ilivyokuwa ikiendelea leo
 Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvanda akiwa na Kampeni Meneja wake, Godbless Lema muda mfupi baada ya kushuka kwenye helikopta yao walipokuwa wakizunguka katika ameneo mbalimbali kuangalia shughuli ya upigaji kura vituoni ilivyokuwa ikiendelea leo
 Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvanda akibadilishana mawazo na muda mfupi baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kuangalia shughuli ya upigaji kura vituoni ilivyokuwa ikiendelea leo.Picha Zote na Chadema

Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzanzia(BoT)

$
0
0



Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.



Kamati imeamua kwamba;


1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya tegeta escrow.


2) TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.



Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.


PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.


PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.


Imetolewa na 


Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014

MSANII WA JAMAICA ‘VYBZ KARTEL’ AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 KWA KESI YA MAUAJI.

$
0
0
Mkali wa miondoko ya DanceHall kutoka nchini Jamaica, Vybz Kartel(38) amekutwa  na hatia  ya mauaji ya promota Clive “Lizard” Williams yaliyotokea Agosti 2011 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani.
Kwa mujibu wa mtandao wa Jamaica Observer ulidai kwamba Kartel aliyekuwa amefungwa kwa takribani miaka 3 akisubiria hukumu ya kesi ya hiyo, alionekana aliyekata tamaa na kuonyesha uso wa huzuni kufuatia uamuzi wa mwisho walioutoa  majaji katika kesi yake iliyokuwa inamkabili .
Baada ya Kujadiliana mapendekezo  kwa muda wa masaa mawili,  jopo la majaii lilipiga  kura 10 – 1 zilizomtia hatiani Kartel na washtakiwa wenzake watatu, Andre “Mad Suss” St. John, Kahira Jones na Shawn “Shawn Storm” Campbell kwa kuhusika katika mauaji ya Williams(27)  huku mshtakiwa wa  nne, Shane Williams akiachiwa huru na mahakama baada ya kuonekana kuwa hana hatia.
Waendesha mashitaka walisema kuwa marehemu ‘Clive Williams’ alipelekwa St Andrew nyumba kwa mwanamuziki  Kartel ambako  alipigwa hadi kufa sambamba na kupatikana kwa risasi mbili eneo la tukio.
Kwa mujibu wa taarifa unadai kwamba hakuna ushahidi wa wazi uliopatikana ila mahakama ilitumia ushahidi wa kimazingira kuweza kujiridhisha ikiwemo ujumbe wa sauti(Voicemail) na meseji za vitisho alizokuwa akitolewa Williams.
Mashabiki Duniani watammisi Kartel, ambaye anajulikana kwa hits zake zilizokuwa zilizokuwa zikiwabamba  ikiwa ni pamoja na “romping Shop,” “Dollar Sign,” “Clarks” na “Pon De Floor,”  na baadhi ya nyimbo alizoshirikiana na wanawamuziki wa kimataifa kama vile  MIA, Eminem, Busta Rhymes, Lil Wayne, Jay Z na Rihanna.
Hata hivyo Wanasheria wa Kartel wanampango wa kukata rufaa juu ya uamuzi uliotoa mahakama katika kesi hiyo, ndani ya siku 65 kwani wanaamini hukumu iyo ni ya kihistoria, ingawa watuhumiwa wanaweza kupunguziwa adhabu na kufikia miak15 au chini ya hapo.

MSANII WA JAMAICA ‘VYBZ KARTEL’ AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 KWA KESI YA MAUAJI.

$
0
0
Mkali wa miondoko ya DanceHall kutoka nchini Jamaica, Vybz Kartel(38) amekutwa  na hatia  ya mauaji ya promota Clive “Lizard” Williams yaliyotokea Agosti 2011 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani.
Kwa mujibu wa mtandao wa Jamaica Observer ulidai kwamba Kartel aliyekuwa amefungwa kwa takribani miaka 3 akisubiria hukumu ya kesi ya hiyo, alionekana aliyekata tamaa na kuonyesha uso wa huzuni kufuatia uamuzi wa mwisho walioutoa  majaji katika kesi yake iliyokuwa inamkabili .
Baada ya Kujadiliana mapendekezo  kwa muda wa masaa mawili,  jopo la majaii lilipiga  kura 10 – 1 zilizomtia hatiani Kartel na washtakiwa wenzake watatu, Andre “Mad Suss” St. John, Kahira Jones na Shawn “Shawn Storm” Campbell kwa kuhusika katika mauaji ya Williams(27)  huku mshtakiwa wa  nne, Shane Williams akiachiwa huru na mahakama baada ya kuonekana kuwa hana hatia.
Waendesha mashitaka walisema kuwa marehemu ‘Clive Williams’ alipelekwa St Andrew nyumba kwa mwanamuziki  Kartel ambako  alipigwa hadi kufa sambamba na kupatikana kwa risasi mbili eneo la tukio.
Kwa mujibu wa taarifa unadai kwamba hakuna ushahidi wa wazi uliopatikana ila mahakama ilitumia ushahidi wa kimazingira kuweza kujiridhisha ikiwemo ujumbe wa sauti(Voicemail) na meseji za vitisho alizokuwa akitolewa Williams.
Mashabiki Duniani watammisi Kartel, ambaye anajulikana kwa hits zake zilizokuwa zilizokuwa zikiwabamba  ikiwa ni pamoja na “romping Shop,” “Dollar Sign,” “Clarks” na “Pon De Floor,”  na baadhi ya nyimbo alizoshirikiana na wanawamuziki wa kimataifa kama vile  MIA, Eminem, Busta Rhymes, Lil Wayne, Jay Z na Rihanna.
Hata hivyo Wanasheria wa Kartel wanampango wa kukata rufaa juu ya uamuzi uliotoa mahakama katika kesi hiyo, ndani ya siku 65 kwani wanaamini hukumu iyo ni ya kihistoria, ingawa watuhumiwa wanaweza kupunguziwa adhabu na kufikia miak15 au chini ya hapo.

MATOKEO YA JUMLA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA:CCM YASHINDA KWA KISHINDO

$
0
0


Mgombea Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa  akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho jana usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko kwenye jimbo hilo la Kalenga. 
=======  =====  =======
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga Iringa vijijini yametangazwa rasmi jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha CCM kilipata jumla ya kura 22962,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5853 na chama cha CHAUSTA kilipata kura 150.Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia 79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo.

FAIDIKA: Kuchukua mikopo ya biashara bila elimu ya ujasiriamali ni hatari

$
0
0

 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate to Margaret Yohana, an entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days " NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam end of the week. Left is co-author and project coordinator, Dr Ellen Otaru Okoedion.
 An entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam end of the week, Helen Makuru (left) is congratulated by VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi shortly before receiving her certificate from FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore.
 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate to Famasa Disabled Group Chairperson, Lillian Kabaliki, who was part of entrepreneurs  who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Center is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi.
 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate to an entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days "NAWEZA, a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend, Fatuma Miringa. Center is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi.
 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (center) speaks to a group of entrepreneurs from marginalized groups and local Tanzanians from the streets, who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Left is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi and right is Andrew Okallo, Project designer. 
  Director for Small Industries and Small and Medium Enterprises (SMEs) at the Ministry of Industry and Trade, Consolata Ishebabi, speaks to a group of entrepreneurs from marginalized groups and local Tanzanians from the streets, who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Left is VIBINDO Society Chairman Graston Kikuwi and right Emanuel Mwakyusa co-author of the training manual and moderator. 
One of the entrepreneurs (fourth right) who attended a two days"NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend, being congratulated by the seminar moderators, organizers and sponsors.   
======  ======  ======

FAIDIKA: Kuchukua mikopo ya biashara bila elimu ya ujasiriamali ni hatari   
Na Mwandishi Wetu.
Wajasiriamali wakitanzania wameonywa dhidi ya tabia ya kuchukua mikopo bila kuwa na elimu sahihi ya kuziendesha biashara zao, lakini badala yake wanapaswa pia kupata elimu ya ujasiriamali kama wanahitaji kuziendeleza biashara zao.
Wataalam wameonya kuwa mikopo bila ya kuwa na ujuzi wa uendesheji biashara unaweza sababisha biashara kufanya vibaya, mtaji kufa kabisa na kupelekea mkopaji kubaki na madeni makubwa.
Akizungumza wakati wa warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na FAIDIKA kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupata mafunzo ya usimamizi wa biashara na fedha iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na wa kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi alisema biashara za kitanzania zinashindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa elimu ya usimamizi bora na uongozi wa biashara.
“Watanzania wengi wajasiriamali wanadhani kuwa na mtaji wa kutosha ni njia pekee ya kufanikiwa katika biashara. Hili ni wazo potofu. Wengi uchukua mikopo baada ya hapo biashara zao ushindwa kukua na wanajikuta katika madeni makubwa,” alisema.
Aliwaasa wajasiriamali kujenga utamaduni wa kutafuta mafunzo fasaha kabla ya kuwekeza sana katika biashara ambazo hawazifahamu kiundani.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore alisema ikiwa ni kama mchango wa kampuni yake kwenye ustawi wa jamii ya kitanzania, FAIDIKA imetanua wigo wa elimu ya ujasiriamali mpaka kwa jamii ya kitanzania isiyokuwa na uwezo, kupitia warsha ya mafunzo ya usimamizi wa biashara na uhamasishaji ijulikanayo kama ‘FAIDIKA FREE Financial Empowerment, ikiwa na kauli mbiu ya ‘NAWEZA’.
Warsha hiyo pia iliyoambatana na uzinduzi wa kitabu cha mafunzo kilichoandikwa na wataalam watatu wa mafunzo ya biashara, imeanzia jijini Dar es Salaam na itaendelea katika mikoa mingine.   
“Mpango huu umelenga katika kukuza na kutekeleza mbinu za ukuzaji uchumi kwa watu wa hali ya chini kama walemavu na watu waishio katika mazingira magumu kupitia mikopo midogo midogo na elimu ya ujasiriamali na itafanyika kama warsha ya siku mbili itakayojumuisha masuala yote ya jinsi gani ya kuanzisha, kuendesha biashara na pia jinsi ya kutumia teknolojia hususani ya simu za mokoni ili kuboresha biashara,” alisema.
Bi Moore alisema kuwa mwishoni mwa warsha, washiriki wataweza kutambua ni biashara ya aina gani wanataka kuifanya, kuandika mchanganuo wa biashara, kufanya mahesabu ya awali na kuweza kubadilisha maisha yao. 
"Haya ni majaribio ya awali ya elimu kwa umma na utafanyika katika mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha, ikilenga jumla ya washiriki 300 kutoka katika makundi matatu: Wanawake wa Tanzania asilimia 34, watu wenye ulemavu asilimia 32 na watu wa kawaida mitaani asilimia 34," alisema.
Kwa hatua nyingine, Ofisa mtendaji mkuu huyo wa FAIDIKA alidokeza kuwa, mbali na kuwakopesha waajiriwa kama ilivyokuwa desturi yao, taasisi yake ya fedha hivi karibuni itaanza kutoa mikopo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati, taasisi ndogo za fedha, kukopesha kwenye biashara, na itakuwa ikifanyakazi kwa ukaribu na watu wanaojituma, waaminifu na kujiamini kuwa wanaweza kama ilivyo kauli mbiu yao ya ‘NAWEZA’.
Bi Moore alibainisha kuwa wajasiriamali watakaopata mafunzo hayo pia wataingia katika shindano la uandishi wa mchanganuo wa biashara, ambapo mshindi atapokea zawadi ya pesa taslim itakayokuwa kama mtaji kwa mchanganuo huo wa biashara ulioshinda.
Kwa niaba ya washiriki wote wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kundi la wajasiriamali walemavu (FAMASA disabled group), Lillian Kabalika, aliipongeza FAIDIKA kwa kutambua umuhimu wa kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali bure.
“Tunatoa pongezi kwa wazo hili. Tunawaomba FAIDIKA wasiishie kuwapatia mafunzo watu wasiojiweza peke yake, lakini pia wawasaidia katika kuyafanyia kazi yale waliojifunza. Na pia nawaomba waendelee na elimu hii ili watu wengi walio na ulemavu watambue kuwa ulemavu si kushindwa na kila kitu na wanaweza kuondoka mitaani na kuacha kuomba omba na kuanza kujitegemea na hata kuweza kutengeneza ajira zaidi na kuwaajiri wale wasiokuwa na ajira,” alisema.

MATOKEO YA JUMLA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA:CCM YASHINDA KWA KISHINDO

$
0
0


Mgombea Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa  akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho jana usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko kwenye jimbo hilo la Kalenga. 
=======  =====  =======
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga Iringa vijijini yametangazwa rasmi jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha CCM kilipata jumla ya kura 22962,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5853 na chama cha CHAUSTA kilipata kura 150.Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia 79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo.

Article 8

$
0
0

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watumishi Bw. George D. Yambesi, katikati, akiendesha mkutano wa Baraza, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAB Mkwizu na kushoto ni Katibu Bi. Lilian Denis.
 Sehemu yaWajumbe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba akitoa mchango wake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
 Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu Bw. Emmanuel Mlaya akitoa mchano wake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Utumishi.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watumishi akisikiliza hoja wakati wa mkutano, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAb Mkwizu
Mmoja wa wajumbe Suleiman Mafele anayetarajia kustaafu, kulia, akimuaga Katibu wa Baraza la Watumishi wa Ofisi ya Rais , menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Lily Denis, katikati, kushoto ni Bw. Festus Mbwiro.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL A AFUNGUA MKUTANO WA WAWEKEZAJI KATI YA ISRAEL NA TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


1 (9)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014.
3 (5) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo. 4. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya, wakati alipotembelea banda la Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi  mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kulia ni Mkuu wa Maendeleo ya Biasara na Habari, Linda Byaba. 5 (1) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kushoto ni Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya (kulia) ni Mkuu wa Maendeleo ya Biasara na Habari, Linda Byaba.6 (2)8 (1) Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia ukumbini humo.9 (1) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.11Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka ukumbini baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Picha na OMR

AIRTEL yakabidhi shilingi million Tano kwa wanawake kwa ajili ya Tuzo ya Mwanamakuka 2014

$
0
0



Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mfano wa hundimwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo wakati wa halfa ya Tuzo za Mwanamakuka 2014 ambapo Airtel Tanzania ni moja kati ya Wadhamini wa tuzo hizo,  Bi Leil Mwambungu aliibuka na kutangazwa mshindi wa mwanamakuka 2014. Akishuhudia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha (wakwanza kulia), Hafla ya mwanamakuka ilifanyika jana katika ukumbi wa Escape 1 mikocheni Dar es salaam. 



 Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kulia) akimpongeza mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika halfa ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam
mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika hafla ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam, pichani kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha


========  ========  =========
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imekabithi waandaaji wa Tuzo za mwanamakuka The Unity of Women Friends kiasi cha million tano pesa taslimu wakati wa halfa ya  tuzo za mwanamakuka 2014 zilizofanyika jijini Dar es saalam mwisho wa wiki
Tuzo hizi za mwanamakuka 2014 ziliwashirikiasha washindi 10 wa mwaka 2012 na mwaka 2013 ambapo washindi hawa walifatiliwa biashara zao na kuchaguliwa mshindi mmoja aliyefanya vizuri na kutumia vyema zawadi aliyoshinda katika kuendeleza biashara zao ambapo bi Leila Mwambungu aliyekuwa mshindi wa pili mwaka Jana kuibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema”  Tunayofuraha kuwa  wadhamini  wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa miaka mitatu mfululizo kwa sasa na kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa wanawake kupitia tuzo hizi. tunafurahi kuona jinsi kina mama hawa wajasiriamali walioshinda miaka iliyopita wakifanya vizuri katika biashara zao.
Na sisi Airtel leo tunakabithi kiasi cha kiasi cha shilingi milioni tano kama mchango wetu kwa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka 2014. Tunaamini kiasi hichi cha fedha kitaweza kuwawezesha waaandawaji wa tuzo hizi kufanikisha halfa hii na kuwafikia wanawake na kuwawezesha  kutanua mitaji yao na hatimae kuongeza kipato na faida zaidi na kujikwamua kiuchumi”.
“Tutaendelea kushirikiana na The unity of Women Friends ili kuhakikisha tunaweza kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini” aliongeza Matinde.
Kwa upande wake mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu Alisema “naona fahari na furaha kuwa mshindi wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka huu, napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi kwa kuniona kupitia juhudi ninazoziweka katika kazi zangu na biashara zangu. Mpaka sasa nimeweza kuajiri watanzania kupitia biashara zangu na  Kiasi hii nilichozawadiwa leo kitanisaidia sana kukuza mtaji. 
Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza  katika biashara zao,  haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
Naye mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema Tuzo hizi za Mwanamakuka zinaendelea kukua na kuziboresha zaidi,   kwa mwaka huu lengo letu lilikuwa ni kuwawezesha wachache kwa kuwafatilia washindi wetu 10 wamiaka iliyopita na kuona jinsi gani biashara zao zinavyoenda na kumzawadia anayefanya vizuri zaidi. Lengo ni kuendelea kuwahamasisha na kufatilia mafanikio yao kwa karibu.
vilevule tukiangalia miaka iliyopita tuliweza kuwashirikisha wanawake tu katika sherehe za tuzo hizi lakini kwa mwaka huu tumeamua kushirikisha familia kwa kuandaa bonanza ambapo wakinababa na watoto kwa pamoja tunasherehekea mafanikio haya, na kusherehekea siku ya wanawake duaniani huku tukienzi juhudi za wanawake jasiri nchini na kuwazawadia
Tunashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi miaka mitatu kwa sasa na tunaamini kuwa bado wataendelea kutoa mchango wao na kushirikiana nasi na kutuunga mkono kwa miaka mengine ijayo na kuhakikisha lengo letu la kumwinua mwanamke wa kitanzania linafikiwa. Alisema Shamo

Kwa mwaka huu Tuzo hizi zilishirikisha washindi waliopatikana miaka iliyopita ambapo kati yao pamoja na Tatu  Ngao, Mwananne Msekalile, Sikudhani Daudi, Nasra, Aziz, Khalid, Leila Mwambungu, Selestina Renatus, Maajab Yusufu na Agnes Daudi  ambapo Bi Leila Mwambungu Ameibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
Viewing all 21933 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>