Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21901 articles
Browse latest View live

MAGADI SODA KULIINGIZIA TAIFA SHILINGI BILIONI 480 KWA MWAKA

$
0
0

 Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga, na Mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya habari Frank Mvungi 
 Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda  katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga  
Mhandisi wa mradi wa  magadi soda  Godfrey Mahundi akitoa ufafanuzi kuhusu makadirio ya gharama za mradi huo ambao unakadiriwa kutumia  kiasi cha dola za kimarekani milioni 500. Katikati ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba na wa mwisho ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga.PICHA ZOTE  NA. Georgina Misama-MAELEZO.
========    ==========  ========
Frank Mvungi-MAELEZO.

IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni  mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni  480 kwa mwaka.

Hayo yamesemwa na  Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Ngapemba alisema hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini hayo katika Bonde la Engaruka  Wilayani Monduli mkoani Arusha.

Alizitaja faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na fedha za kigeni kutokana  na mauzo ya madini hayo nje ya nchi. Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.

Ngapemba  alibainisha kuwa madini ya magadi soda yanatumika viwandani  katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza  karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.

Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu  tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda. Alisema kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata ni kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.

“Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo”, alisema Ngapemba na kuongeza:

Alisema kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.

BODI YA UCHUNGUZI WA AJALI YA MV KILIMANJARO 2 YAKABIDHI RIPOTI YAKE KWA WAZIRI WA MIUNDOMBUNU NA MAWASILIANO ZNZ

$
0
0

 Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo wakati wa kumkabidhi  Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Rashid Seif Suleiman (Mwenye Kanzu)Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha na Nafisa M. Ali-WMM
Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Na Nafisa M. Ali –WMM    
      17/03/2014
Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 leo imekabidhi rasmi Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa  Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Akikabidhi Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema kazi hiyo waliyopewa wameweza kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na walikuwa huru bila ya kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi yoyote.

Aidha alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi wa Zanzibar. Hata hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa kuifanya kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi hiyo na majukumu mengine walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi hiyo walitakiwa kuikabidhi kesho na badala yake wameweza kuikabidhi leo.

Aidha mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo. Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi walizingatia uhalisia wa kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu.

Aidha alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia. Hata hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa mujibu wa taratibu zilizopo. Aidha aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala Serikali.

Naye Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki  itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika. Bodi hiyo ya Wajumbe watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Baharini kifungu no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 iliyotokea Miezi miwili iliyopita katika Mkondo wa Nungwi ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

GODFREY MGIMWA AKABIDHIWA HATI YAKE YA KUWA MBUNGE

$
0
0

 mshindi wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa akiwa na mke wake Robby Mgimwa wakifurahia hati aliyokabidhiwa ya kuwa mbunge.
 Godfrey Mgimwa akiwa anafurahia ushindi katikati Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijiji mama Mtavilalo.

(DOWNLOAD NEW AUDIO) B,BaFA ft.Castro Rap game kibiashara mp3.

KAMERA PAMOJA NA WADAU KUAFANYA ULINZI KATIKA NGUMI MARCH 29 PTA SABASABA

$
0
0

ALLY MWAZOA PROMOTA
WADAU wa mchezo wa masumbwi nchini Tanzania wamejitokeza kuwa walinzi wa mapambano yaliyo andaliwa na promota Ally Mwazoa yatakayoanza march 29, april 26 na mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba  akizungumzia mpambano wa Japhert Kaseba na Thomas mashali mpambano ambao umebakiza siku chache tu ili ufanyike

Mwazoa aliwashukulu wadau hawo ambao wamejitokeza kwa ajili ya ulinzi wa ali ya juu utakaofanyika siku hiyo kwa mabondia na wadau wenyewe kukubali kulipa kiingilio na kufanya ulinzi wa kila kona katika ukumbi huo
ambapo klabu mbalimbali za ngumi kutoka Temeke Ilala Kinondoni na Tanga pamoja na mikoa ya jirani na wadau wamejitokeza kuthibiti fujo mbalimbali ambazo zitajitokeza siku hiyo pia wale ambao wamedhamilia kufanya fujo siku hiyo kutakuwa na askari kanzu mbalimbali hivyo watapata kipondo cha ali ya juu pamoja na kutupwa lupango

Mwazoa aliongeza kwa kusema siku hiyo kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa kila upande wa ukumbi huo ili kuona matukio mbalimbali ya nje na ndani yatakayokuwa yakiendelea ili kuthibiti vitendo vya uhuzwaji wa tiketi feki na kuingia kiolela na kusababisha asara kwa promota na washiliki katika tukio zima

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi makali ambapo bondia Haji Juma atavaana na Juma Fundi wakati Fred Sayuni atapambana na Rajabu Mahoja na Zuber Kitandula atamenyana na Issa Omar wakati Bakari Dunda ataoneshana ubabe na Baina Mazola

Mwazoa
aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka  
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

RUBANI FARIQ ABDUL HAMID ASEMEKANA KUITOROSHA NDEGE YA MALAYSIA AIRLINES

$
0
0


Kamera za usalama zikimwonyesha rubani wa ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777, Zaharie Ahmed Shah,  kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.
Michoro inayoonyesha njia ambayo ndege hiyo huenda ilipitia kwenda kusikojulikana.
Mwanafunzi, Firman Siregar, akiwa na wazazi wake, ni mmoja wa abiria 239 waliokuwa katika  ndege hiyo yenye orodha ya safari namba  Flight MH370.
Rubani Zaharie Ahmad Shah.
Nyendo za ndege hizo zinavyokisiwa na wataalam.
Mwandishi wa habari akichukua picha nyumba ya  rubani Fariq Abdul Hamid eneo la Shah Alam, karibu na Kuala Lumpur.
Maafisa nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege hiyo kutoweka.
Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, au goodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
Juhudi za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.
CHANZO: PICHA DAILYMAIL / HABARI BBC SWAHILI

FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ARNOLD KAMBONAPANI NKHOMA YAENDESHA MISA MAALUM YA SHUKRANI JIJINI DAR

$
0
0


DSC_0496
Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai, akiendesha Ibada bya Misa maalum ya Shukrani kufuatia kifo cha Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma (100), aliyeaga dunia Ijumaa ya tarehe 17 January,2014 katika hospitali ya Mount Ukombozi na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 19 January, 2014 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
DSC_0486
Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikishiriki misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika mwishoni mwa Juma jijni Dar.
DSC_0491

DSC_0551
Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai akimrithisha kiti alichopenda kukaa marehemu wakati wa ibada za Jumapili kanisani hapo mmoja wa watoto wa Mzee Arnold Nkhoma Bw. Amos Nkhoma.
DSC_0554
Baadhi ya wajukuu na vitukuu wa Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma, wakiwa kwenye misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika jijini Dar.
DSC_0562
Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikitoka kanisani mara baada ya misa maalum.
DSC_0595
Babu wakiwa na mmoja wa vitukuu wa Marehemu Mzee Arnold Nkhoma.
DSC_0607
Michael Nkhoma, ndiyo mtoto mkubwa wa marehemu, akiongea na mdogo wake Amos Nkhoma. Kulia ni Aidan Nkhoma.
DSC_0626
Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na baba yake mkubwa Michael Nkhoma,(kushoto) na Mzee Aidan Nkhoma.
DSC_0608
Mama na Mwana wakijichukua taswira.
DSC_0642
Familia ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma wakiwasha mishumaa kwenye kaburi la Mzee Arnold Nkhoma mara baada ya misa maalum ya shukrani iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
DSC_0664
Mmoja wa vitukuu wa Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma akiweka shada la maua kwenye kaburi la babu yake.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.AMEN.
DSC_0679
Ndugu, jamaa na marafiki walipojumuika nyumbani kwa nyumbani kwa Profesa Alice Nkhoma Wamunza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya chakula cha mchana.
DSC_0750
Profesa Alice Nkhoma Wamunza, akiongoza ndugu, jamaa na marafiki kwenye chakula mchana baada ya misa ya shukrani ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma. Kwa picha zaidi ingiahapa

Article 11


MTWARA KUJIVUNIA HOSPITALI YA RUFAA

$
0
0

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake. Kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia).
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa akisisitiza jambo wakati wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa (Wapili kulia, aliyenyanyua mikono) akiwaonesha eneo litakapokuwepo Hospitali mpya ya rufaa mkoani humo wakati wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika kujionea maendeleo ya maandalizi ya awali ya ujenzi wa hospitali hiyo.
 Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdallah Komba (aliyeinama) akiwaelekeza namna ya hospitali ya rufaa ya mkoa huo itakavyokuwa wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea mradi huo.
Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza wakati timu yake ilipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya awali ya ujenzi wa hospitali hiyo.
=======  =======  =========
MTWARA KUJIVUNIA HOSPITALI YA RUFAA
Na Saidi Mkabakuli
Wakazi wa mikoa ya kusini ikiwemo Mtwara, Lindi, na Ruvuma inatarajiwa kupata hospitali ya kisasa ya rufaa itakayojengwa katika eneo la Mikindani, nje kidogo ya mkoa wa Mtwara katika lengo la kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unakuwa shirikishi na kuendelea kuboresha huduma za jamii hususan na afya katika mikoa hiyo.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya katika mkoa huo.
“Mradi wa hospitali ya Rufaa ya Mtwara umelenga kutoa huduma za rufaa kwa kanda ya kusini hususan mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma, hospitali hii itakapokamilika inategemewa kuchukua wagonjwa wa nje na ndani watakaohudumiwa kwenye vitengo mbalimbali vinavyojitosheleza kwa vifaa na wataalamu, “ alisema Dkt. Maarifa. Kwa mujibu wa taarifa za awali mradi ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2012/13 kwa fedha za Serikali zinazotolewa kupitia ngazi ya wizara ambapo mpaka sasa ujenzi wa uzio kuzunguka eneo hilo umekamilika.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa suala la afya kwa wakazi wa mikoa ya kusini, na akatoa wito kwa uongozi wa mkoa kuzingatia na kusimamia matumizi sahihi ya fedha za serikali katika mradi huo.
“Madhumuni ya mradi ni mazuri hivyo mkoa kupitia wizara kuweka msukumo kwa kuhakikisha mradi unakamilika na kutelezwa kwani utachangia kuboresha huduma za afya katika maeneo ya kusini na kupunguzia wananchi mzigo wa gharama kwa kufuata hospitali zilizo mbali na mikoa yao,” alisema Bibi Mwanri ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Huduma za Jamii na Maendeleo ya Idadi ya Watu.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) eneo la afya ni kipaumbele cha nne cha mkakati kwa lengo la kuongeza maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi ambapo Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu hasa katika elimu ya juu na vyuo vya huduma za afya na uongezaji ubora na upatikanaji wa huduma hizo katika kujenga nguvu kazi itakayoleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Article 9

$
0
0

OLE SENDEKA, LEKULE LAIZA WAMFAGILIA RIDHIWANI KIKWETE CHALINZE,WAWATAKA WANACHALINZE WAMCHAGUE RIDHIWANI

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa katika Mkutano na Wazee wa Kimasai walipokuwa wakijadilina juu ya swala la Wafugaji wa Chalinze na Pwani kwa Ujumla,jana Machi 17,2014 kwenye Ukumbi wa Masai,Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka akiwaomba Wananchi wa Lugoba,Jimbo la Chalinze kutofanya makosa kwenye Uchaguzi Mdogo ndani ya Jimbo lao na Wampigie Kura Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete. Sendeka aliyasema hayo jana Machi 17,2014 katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoni wakati alipopita kuwasalimia WanaChalinze
Mbunge wa Jimbo la Longido,Mh. Lekule Laiza akiwasalimia Wana Chalinze
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya Kadi mbili za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto) na Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha Msata,Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi
 Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana   
 Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa Lugoba,Chalinze



  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa amekabidhiwa fimbo ikiwa ni ishara ya kusimikwa na kuwa Laigwanani wa Kimasai na Laigwanan Ole Masinga,jana .Picha na Othman Michuzi

NGOME YA CHADEMA YAKUMBWA NA MSISIMKO JIMBO LA CHALINZE,WAFUASI WAKE WAANZA KURUDISHA KADI KWA RIDHIWANI KIKWETE

$
0
0

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto) na Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha Msata,Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa Lugoba,Chalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akiambatana na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chalinze (CCM),Saleh Mpwimbwi (kushoto) pamoja na Msafara wake wakielekea kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakishiriki kwenye dua ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kisomo cha kumuombea Marehemu ambaye ni Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman (alieketi nyuma ya mgombe) mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MSAMA AIPONGEZA BASATA KWA KUANZISHA MAFUNZO YA SANAA KWA WATOTO

$
0
0

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama  akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Boma mara baada ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto 200 wa shule za msingi tano za wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam jana. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), na kufadhiliwa na kampuni ya Msama Promotions. 
 Baadhi ya watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Ilala wakionesha vipaji vya kucheza ngoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),na kufadhiliwa na Kampuni ya Msama Promotions . Jumla ya watoto 200 wamenufaika na mafunzo hayo.
  Mmoja wa wanafunzi akionesha mitindo ya mavazi.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buguruni Visiwi wakionesha mitindo mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Mtoto Mariam Yusuf akisimulia hadithi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto wa shule za msiongi kutoka Manispaa ya Ilala. 
 Mtoto Mariam akionesha kipaji chake.
 Watoto wakicheza maigizo.
 Baadhi ya watoto wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana wakiwa katika hafla hio.
 Msama akiagana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana.
DAR ES SALAAM, Tanzania

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama amepongeza hatua ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuanzisha mafunzo maalumu kwa watoto wa shule za msingi.
 
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo maalumu
yanayolenga kuwajenga watoto katika fani ya sanaa na kushirikisha watoto wapatao 200 kutoka shule tano za wilaya ya Ilala, Msama alisema ni jambo zuri kuandaa vipaji vya kesho.
 
“Mafunzo haya yataweza kuwajenga watoto wetu ambao ndio taifa la kesho, pia kupunguza tatizo la watoto kujiingiza katika mambo mabaya kama matumizi ya bangi, dawa za ulevya, hivyo kuwa mzigo na janga kwa taifa,” alisema Msama.
 
Shule zilizonufaika na mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Msama kupitia
kampuni yake ya Msama Promotions, waratibu wa Matamasha ya Pasaka na Krismas, ni Buguruni Moto, Buguruni Visiwi, Ilala Boma, Uhuru Wasichana na Msimbazi.
 
Aidha, Msama alihimiza umuhimu wa somo la sanaa shuleni akitaka lipewe msisitizo mkubwa katika kuandaa vijana bora ambao hata kama wakifeli masomo mengine, wanaweza kuwa wasanii bora. “Somo hili la sanaa mashuleni lipewe uzito unaostaili kama masomo mengine kwa sababu, mtoto akifeli masomo mengine, fani ya sanaa yaweza kuwa msaada kwake,” alisema.
 
Msama aliwashauri pia Basata kuyapeleka mafunzo hayo hadi mikoani na
kupendekeza kwa hatua ya awali waanzie katika mikoa ya Pwani na Morogoro, akiamini kuna vipaji vingi vya sanaa.
 
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema mafunzo hayo yaliyoanza Machi 1, wanafunzi walikuwa wakifanya mazoezi ya sanaa katika fani utambaji, hadithi, ngoma za asili na maigizo katika maeneo ya shule zao chini ya usimamizi wa walimu wao na waratibu kutoka Basata.

Mngereza alimshukuru mgeni rasmi Msama kwa kudhamini mafunzo hayo
akisema amefanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu ya sanaa katika maisha ya kila siku.
 
“Msama ameonesha wazi kuwa yeye ni mdau na mfurukutwa wa sanaa,
aliyepania kuendeleza sekta ya utamaduni hasa sanaa kwa kuibua vipaji vya
watoto,” alisema.

Higher Education in Science & Technology Critical for Africa?s Future !

$
0
0


             
         
       REPUBLIC OF RWANDA
     



Higher Education in Science & Technology Critical for Africa’s Future, say Rwanda's President Kagame, WB's Makhtar Diop

KIGALI, March 17, 2014 – At a high-level forum in the Rwandan capital, H.E. President Kagame, President of Rwanda and World Bank Vice President for Africa Makhtar Diop highlighted Africa’s urgent need for larger numbers of scientists, engineers, and technicians who can meet the growing market demand for such expertise and contribute to development and shared prosperity in their countries.

Themed “Accelerating Africa’s Aspirations,” the forum on Higher Education for Science, Technology and Innovation was co-hosted by the Government of Rwanda, a champion of science and technology, and the World Bank, one of Africa’s largest development partners in higher education. The forum aimed to boost science, technology, and engineering capability as a key driver of economic growth and job creation.

The governments represented at the forum (Ethiopia, Mozambique, Rwanda, Senegal and Uganda), private sector participants and development partners issued a communiqué to the effect that they would invest strategically in science, technology, and engineering education to accelerate Africa’s progress into a developed, knowledge-based society within a generation.
  
H.E. President Paul Kagame said: "I welcome the commitment to strengthen and mobilise resources for building capacity in science and technology, in our pursuit of Africa’s socio-economic transformation. Our collective commitment must be followed by concrete action to drive innovation for the development of our people and our continent."

Makhtar Diop, the World Bank’s Vice President for Africa, who delivered the keynote address, said:
“To be more competitive, expand trade, and remove barriers to entering new markets, Africa must expand knowledge and expertise in science and technology. Let us set some bold targets: that we will see a doubling of the share of university students graduating from African universities with degrees in mathematics, science and technology by 2025. The time has never been more auspicious to focus on higher education, particularly in science, technology and mathematics.”

In the concluding communiqué, countries present committed to collaborate with development partners and the private sector to support Africa’s socioeconomic transformation with strategic actions to reform tertiary education systems; increase the share of students in science, technology and engineering; and improve the quality of learning and research. 

They also committed to use growing foreign direct investment flows to build greater technological capability, to enroll more women in science and technology disciplines, and to strengthen science and mathematics education at all levels.

The forum highlighted the importance of setting up regional centers of excellence in various disciplines such as agriculture, biotechnology, health, water and sanitation, and ICTs. 

“Regional partnerships help universities to pool their resources, achieve economies of scale, set up joint facilities and standards, and most importantly, share knowledge and expertise,” Diop noted, “Beyond the borders of the continent, we need to tap the vast experience of Brazil, China, India, and Korea.”  

MANCHESTER UNITED YAPOTEZA MASHABIKI 450,000 KATIKA UKURASA WAO WA FACEBOOK.

$
0
0
man
Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza, hakuna kitu kizuri kama kushabikia mpira hasa inapotokea timu unayoipenda ikiwa inafanya vizuri kwa kuzikabili na kuzifunga timu pinzani, lakini hugeuka kuwa shubiri endapo timu hiyo ikianza kuwa shamba la bibi ama si jamvi la wageni kwa kufungwa mechi za nyumbani na nje na kuwapa nafasi wapinzani kuteleza kwa ganda la ndizi.
Hayo ndiyo yaliyokikuta kikosi cha mashetani wekundu, Manchester United baada ya kupokea vibano mfululizo kutoka kwa timu pinzani, hali iliyosababisha mashabiki wake wapatao 450,000 kujiondoa(Unlike) katika page ya timu hiyo kwenye mtandao wa Facebook baada ya kukatishwa tamaa  kwa kukubali kufungwa dimbani kwao ‘Old Trafford’  jumla ya mabao 0 -3 dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita.

NAZIZ AKANUSHA KUBANJUKA NA PRODUCER KHERI SAPPY WA TANZANIA, PICHA WALIZOPIGA ZAZUA UTATA.

$
0
0

Nazizi-1-602x360
Queen wa rap kutoka Kenya, Naziz, ameruka kimanga habari zilizozagaa mitandaoni kuwa kwa sasa anatoka na producer mtanzania Kheri Sappy ikiwa ni kipindi kifupi kupita  tangu aachane na aliyekuwa mume wake raia wa Tanzania, sambamba na kuzagaa kwa picha za kimahaba alizopiga na mtengeneza beat huyo zilizovuja katika mtandao wa Instagram.
“Nina marafiki wengi zaidi ambao ni wa kiume,tunapiga picha kila mahali, hivyo ndivyo ninavyohusiana na marafiki zangu”. Naziz aliuambia mtandao wa Nairobi news.
Aliongezea kuwa picha hizo zilizozagaa kwenye blogs nyingi zilipatikana kwenye akaunti ya Instagram anayotumia Sappy na mojawapo ya gazeti tando(Blog) lilikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba producer huyo alikiri kuwepo kwa uhusiano baina yao na yuko kwenye mipango ya kumchumbia, ingawa Naziz bado ameendelea kushikilia msimamo wake wa kuwa jeshi la mtu mmoja(Single Lady).
”Kwa kweli, sitashangazwa kwa picha zaidi zikiendelea kusambazwa, kama nilivyosema , siangalii mtu, nina marafiki wengi wa kiume  na ambao nipo nao karibu” aliongezea rapa huyo wa kike.
Nazizi-2-603x360
Nazizi-5-598x360
Nazizi-4-621x360

MAHABA NIUE : RIHANNA AMFUATA DRAKE HADI CHOONI.

$
0
0
Ama kweli penzi ni kiti cha basi, ukishuka wanakaa wengine, aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Chris Brown, Bad Girl Riri ‘Rihanna, amepigwa biti la nguvu na mpenzi wake mpya, handsome boy anayeipa rekodi lebo ya Cash Money ugali wa kila siku , Drake, kwa kutokuwa na ukaribu wa aina yoyote ule na zilipendwa wake Chris.
Ishu hiyo inakuja kufuatia mastaa hao kumwaga mchele kwenye kuku wengi na kuamua kujiachia hadharani kama wafanyavyo wapendanao wengine na hivyo kuanza kuwekeana mipaka mapema itakayosaidia kuimarisha penzi lao hilo  walilokuwa wakiliiba kwa siri kubwa tangu enzi hizo.
Pichani  ni Drake na Rihanna wakipata Dinner kwenye mgahawa mmoja huko majuu.
Katika kuonyesha hakuna tena siri, Drizzy na mwanadada Rihanna walikwenda pamoja kupata chakula cha jioni kwenye mgahawa mmoja , hali iliyopelekea kunaswa kwa picha na video ikimuonyesha Rihanna akimfuata Drake kwenye vyoo vya kiume.
Tazama hapa, Hatari lakini salama.

TYGA NA FAMILIA YAKE MITAA YA MALIBU MAMTONI.

$
0
0

Blac Chyna has a lunch at Mr Chow with her fiance Tyga in Malibu, CA
Mmiliki wa  Clothing Line ya  ‘Last King’ na mwanafamilia kutoka Young Money, Michael Ray Nguyen-Stevenson(24) ‘TYGA’ aliwashtua mapaparazi kwa staili ya aina yake baada ya kutokelezea ghafla mitaa ya Malibu akiwa ameongozana na baby mama ake, Blac Chyna na mtoto wao ‘Cairo’  walipokuwa wakielekea kupata msosi wa mchana kwenye mgahawa maarufu wa Mr.Chow uliopo katika mji wa California.
Hivyo kuwapa nafasi watu wenye fani zao kuweza kuwafaidi kwa kuwafotoa picha za kutosha hasa mke wa rapa huyo anayesifika kwa kuwa na umbo la kichokozi kama alilokuwa nalo Agness Masogange.
Watazame mwenyewe..
Blac Chyna has a lunch at Mr Chow with her fiance Tyga in Malibu, CA
Like Father! Like Son! Pichani ni Rapa Tyga akiwa na mtoto wake wa kiume, Cairo aliyezaa na mnenguaji ‘Blac Chyna.
Blac Chyna has a lunch at Mr Chow with her fiance Tyga in Malibu, CA
Hapo sasa, katika picha aliyevalia suruali nyeupe ndiye ‘Blac Chyna mwenyewe.
Blac Chyna has a lunch at Mr Chow with her fiance Tyga in Malibu, CA
Blac Chyna wakuache.
Blac Chyna has a lunch at Mr Chow with her fiance Tyga in Malibu, CA
Mwanamke shepu, sura hata Mbuzi anayo.

TAZAMA VIDEO ZA MAGOLI UONE JINSI LIVERPOOL ILIVYOIADHIBU MANCHESTER UNITED BAO 3 – 0 DIMBANI KWAO OLD TRAFFORD.

$
0
0

Kikosi cha mashetani wekundu,  Manchester United,  kimeendelea kushikilia kaluli mbiu yao ya ukibonde mbele ya mabingwa mara 19 klabu ya Liverpool kwa kukubali mvua ya magoli 3 kwa nunge katika dimba la nyumbani, Old Trafford na hivyo kuipa Liver ubingwa wa bure na kuifanya ivunje historia ya miaka 5 ya kutokushinda uwanjani hapo
 Man Utd: De Gea, Da Silva, Jones, Vidic, Evra, Fellaini, Carrick, Mata, Rooney, Januzaj, van Persie.
Subs: Ferdinand, Lindegaard, Young, Welbeck, Cleverley, Valencia, Kagawa.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Agger, Flanagan, Henderson, Gerrard, Allen, Sterling, Sturridge, Suarez.
Subs: Brad Jones, Aspas, Coutinho, Moses, Sakho, Cissokho, Lucas.
Wafungaji : Gerrard pen 34, pen 46, Suarez 84
Referee: Mark Clattenburg (Tyne & Wear).
Magoli yapo hapa chini..

MILEY CYRUS AUMIZA KINYWA CHAKE KWA TATTOO MPYA ALIYOCHORA KWENYE LIPSI.

$
0
0
Duh! Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi, Dunia inaelekea mrama kutokana na vihoja vinavyoendelea kutokea kila kukicha hiyo inakuja kufuatia  Mwanamuziki wa kibao cha ‘Wrecking Ball’ mwendawazimu ‘Miley Cyrus’ kuja na kioja cha aina yake baada ya kuamua kuumiza lipsi zake na kujichora tattoo ya rangi kwa kimombo ‘colorful tattoo’   na kisha kutupia picha hiyo mtandaoni iliyoambatana  na ujumbe uliosomeka   “#sadkitty #f–kyeahtulsa,” Cyrus, 21”..
Miley Cyrus tattoo
Pichani ni Miley Cyrus akionyesha Tattoo yake mpya aliyoichora kwenye Lipsi zake iliyo na picha ya mtoto wa paka ‘Kitty’
Tangu kuanza kwa ziara yake ya muziki iliyopewa jina la BANGERZ, , Miley amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wake   hasa kutokana na mfululizo wa vituko anavyokuwa akivifanya pindi anapokuwa jukwaani,  mojawapo ya tukio lililovuta vichwa vingi vya habari na kuandikwa sana  mitandaoni  ni kitendo chake cha  kukutanisha ndimi na mwanamuziki ‘Katty Perry’ alipokuwa akiperform katika ukumbi wa Staples Center Los Angels mwezi uliopita.

ATCL yaanza safari za kwenda Mbeya

$
0
0

 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania, Juma Boma (wa pili kulia) akipanda ndege mpya aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe. Shirika hilo limeanza safari zake kwenda Mbeya ambapo itaruka mara nne kwa wiki.
 Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma akipokea maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 iliyotumika  kuzindua safari za kati ya Dar es Salaam na Songwe. Nyuma yake ni kaimu mkurugenzi wa ufundi, Patrick Itule. Shirika hilo litakuwa linaruka mara nne kwa wiki kwenda Mbeya. 
 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma, akibadilishana mawazo na Kaimu mkurugenzi wa ufundi wa shirika hilo, Patrick Itule, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 inayotumika katika uzinduzi wa safiri kati ya Dar es S alaam na Mbeya. Shirika hilo litakuwa likifanya safari zake mara nne kwa wiki kwenda Mbeya, safari ya lisaa limoja tu.
 Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL), Shabani Mtambalike (kulia), akimkaribisha Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa ATCL, Juma Boma (wa pili kulia) na kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe Jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.
 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma (wa pili kulia, Kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule (wa tatu kulia) na Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika hilo Shabani Mtambalike (kulia) wakishangilia, pamoja na wageni wengine, kuwasili kwa ndege ya ATC katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe  jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.
 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania Juma Boma akikata keki kama ishara ya kuzindua safari za ndege ya ATCL kati ya Dar Es Salaam na Mbeya, hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Songwe siku ya Jumatatu mchana. Shirika hilo la ndege lilitumia ndegeyake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki
 Abiria wakiwa ndani ya ndege mpya ya Air Tanzania aina ya CRJ-200 muda mfipi kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa  Songwe wakitokea Dar es Salaam. 
Abiria wakipanda ndege ya Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe wakielekea Dar es Salaa. Safari hizi zitafanyika mara nne ndani ya wiki.
========  ========    =========
ATCL yaanza safari za kwenda Mbeya  

Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Jumatatu hii lilizindua safari zake za kwenda Mbeya kupitia uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Songwe likitumia ndege yake mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ya Canada aina ya CRJ – 200.

Safari hiyo inayochukua kadri ya saa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya itakayofanyika siku nne kwa wiki; Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili, ililakiwa na abiria na wafanyabiashara wanaosafiria kutoka Mbeya kwenda katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa kihistoria uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara/Masoko wa shirika hilo Bw. Juma Boma alisema Air Tanzania imerudi kwa kishindo katika mji ambao ni kitovu cha biashara kwa mikoa ya nyanda za juu kusini na inayotumika kama njia ya kuiunganisha Tanzania na nchi za Kusini mwa  Afrika, ili kupunguza adha ya usafirina kuiunganisha sehemu ya Kusini mwa Tanzania na mikoa mingine.

“Safari ya Air Tanzania kwenda Mbeya iliyosubiriwa kwa muda mrefu imeanza rasmi leo hii. Kwa kutumia ndege yetu mpya, tunatoa usafiri wa haraka na salama, tukiiunganisha Mbeya na mikoa mingine. Kwa saa moja tu, abiria wetu wanauhakika wa kutua uwanja wa ndege wa Songwe kutokea Dar es Salaam.

“Tumezingatia masuala yote ya kiuchumi ili kupanga nauli tuliyoanza nayo ambayo ni kiasi cha shilingi 150,000 kwa tiketi ya kwenda na shilingi 260,000 kwa tiketi ya kwenda na kurudi,” alisema,” Bw. Boma.

Alisema uzinduzi wa njia ya Mbeya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati madhubuti wa upanuzi wa shirika, ambao umelenga katika kuzirejesha safari zote za ndani na za kimataifa na kufungua njia nyingine mpya.

Boma alisema kuwa kutokana na mkakati wao ujulikanao kama go-green utalipelekea shirika hilo la ndege la taifa kuongeza toleo jipya ya ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 78 mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, shirika hilo litaongeza idadi ya safari zake katika njia zake kuu na kuongeza safari za kimataifa.

“Kupitia upanuzi wa safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondokea Dar ukiwa ni saa 11 jioni na kutokea Mwanza  ni saa moja usiku. Tutakuwa tukienda mwanza mara nne kwa wiki.

 Tutakuwa pia tukisafiri kwenda Moroni nchini Comoro katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Vile vile tunatarajia kufungua njia ya Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.

Alibainisha kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria wanaoshindwa kutokea wakati wa safari na wale wanaobadilisha ratiba ya safari zao, na kusema kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana na dharura mbali mbali kabla ya safari.

Mmoja kati ya abiria aliyesafiria katika ndege hiyo kwenda Mbeya, Deogratius Nyanshile aliipongeza Air Tanzania kwa maamuzi yake na kutoa wito kwa watanzania kuliunga mkono shirika kwa kusafiria na Air Tanzania.

“Nawaasa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kanda ya kusini kwa ujumla, kuitumia fursa hii kikamilifu iliyotolewa na shirika la Ndege la Air Tanzania,” alisema Nyanshile. Ndege hiyo ya taifa, ambayo ilisimamisha huduma zake katika mkoa huo kwa sababu ya ubovu wa uwanja wa ndege wa zamani wa Mbeya, imerejesha safari hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.

Ikitumia ndege yake aina ya  Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa shirika hilo linasafiri katika zaidi ya sehemu naneTanzania ikiwa ni pamoja na Mtwara, Mwanza,  Tabora,Kigoma, Dar es Salaam, Bujumbura, Mbeya na kwendaMoroni nchini Comoro.
Viewing all 21901 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>