Image captionMwanamume awajengea watoto wake barabara ya kilomita 8 kwa sururu India
Mwanamume mmoja katika jimbo lililo mashariki mwa India, amejenga barabara ya umbali wa kilomita 8 akitumia sururu ili kuwawezesha watoto wake kupitia wakitoka shuleni.
Jalandhar Nayak, 45, anaishi umbali wa kilomita 10 kutoka shule ambapo watoto wake watatu wa kiume husoma.
Lakini safari hiyo huchukua saa tatu kwa sababu vijana hao hulazimika kupitia milima mitano kabla ya kufika nyumbani.
Maafisa wa eneo hilo waliiambia BBC kuwa watamalizia kilomita zingine saba zilizosalia.
Kwa miaka miwili iliyopita aliamka kila asubuhi na vifaa vyake na angetumia hadi saa nane kwa siku kuchimba mawe na kuyaondoa.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa alitarajia wanawe kwenda nyumbani hasa wikendi na wakati wa likizo mara kwa mara baada ya barabara hiyo kukamilika.
Barabara hiyo wa kilomita 15 itaunganisha kijiji cha cha Bw. Nayak na mji ambapo shule ipo.
Maafisa wa serikali ambao sasa wamendelea na ujenzi huo walisema kuwa Bw. Nayak pia atalipwa kwa kazi aliyoifanya.
Bw Nayak alisema alikuwa na furaha sana kuwa serikali sasa inaikamilisha barabara hiyo. Pia alisema kuwa aliwaomba kupeleka umeme na maji ya kunywa katika kijiji hicho.
Liverpool tayari wamemsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa dau la £48m lakini wanaweza kulipa kati ya Yuro milioni 15-20 ili kumchukua kabisa.(Bild - in German)
Image captionMkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill
Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill alitarajiwa kukutana na maafisa wa klabu ya Stoke siku ya Jumatano kuhusiana na wadhfa wa mkufunzi ulio wazi huku naibu wake Roy Keane pia akitarajiwa kuondoka iwapo atachukua wadhfa huo. (Irish Independent)
Guangzhou Evergrande wanasema kuwa hawatashindana na klabu pinzani ya ligi ya Super Beijing Guoan kupata hudumu za mchezaji wa Gabon na Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang (ESPN)
Image captionDele Alli ni kiungo wa kati wa klabu ya Tottenham
Tottenham imeanza mazungumzo yasio rasmi na kiungo wa kati Dele Alli. Klabu hiyo inadaiwa kuwa na matumaini ya kutia saini kandarasi mpya na mchezaji huyo wa Uingereza. (Daily Mirror)
Naibu mwenyekiti wa klabu ya Fullham Tony Khan amesema kuwa beki wa kushoto wa klabu hiyo Ryan Sessegnon, 17, hatauzwa licha ya kusakwa na Manchester United na Tottenham Hotspurs. (Daily Telegraph)
Manchester United italazimika kulipa hadi £27m ili kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Leander Dendoncker kutoka Anderlecht mnamo mwezi Januari.(Manchester Evening News)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMshambuliaji wa West ham na Senegal Diafra Sakho
Crystal Palace huenda ikakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho, 28, kutoka West Ham mwishoni mwa wiki . (Daily Mirror)
Huddersfield imekubali kuingia mkataba na winga wa Norwich Alex Pritchard, 24. Raia huyo wa Uingereza aliondoka Tottenham kwa dau la £8m katika dirisha la uhamisho la 2016. (Daily Mail)
West Ham wameambiwa watalazimika kulipa £15m ili kumsajili kiungo wa kati wa Bournemouth na Republic of Ireland Harry Arter, 28. (Daily Mirror)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionKiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ameambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka
Kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ameambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka huku Liverpool ikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21. (Diario Gol - in Spanish)
Hearts wanajiandaa kumsajili beki wa kushoto wa Manchester United Demetri Mitchell kwa mkopo.
Beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20 atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo ya Uskochi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.(Edinburgh Evening News)
Image captionBeki wa Barcelona Gerard Pique ameionya Manchester United kwamba beki mwenza Samuel Umtiti atasalia katika klabu hiyo kwa ''miaka mingi ijayo''
Beki wa Barcelona Gerard Pique ameionya Manchester United kwamba beki mwenza Samuel Umtiti atasalia katika klabu hiyo kwa ''miaka mingi ijayo'' .
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 anaweza kuondoka katika klabu hiyo baada ya Barcelona kulipa kitita cha kumwachilia cha £55m mbali na dau la uhamisho huo(Metro)
Wakati huohuo klabu hiyo ya Catalan inakaribia kumsajili beki wa Palmeiras Yerry Mina. Raia huyo wa Colombia ataweka saini ya kandarasi ya miaka mitano na nusu . (Radio Catalunya - in Spanish)
Image captionJavier Mascherano
Anatarajiwa kuchukua mahala pake beki wa Barca na Argentina ,33, Javier Mascherano ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya ligi ya Superleague nchini China Hebei China Fortune. (Goal)
Kiungo wa kati wa Ujerumani na Juventus Sami Khedira, 30, anasema kuwa hayuko tayari kucheza nchini Marekani na anataka kusalia mjini Turin wakati ambapo kandarasi yake itakamilika 2019(Gazzetta dello Sport)
Millwall imewasiliana na Aston Villa kuhusu kumsajili beki mwenye umri wa miaka 30 Tommy Elphick kwa mkopo kwa kipindi cha msimu kilichosalia.
Image captionSami Khedira
Meneja wa Villa Steve Bruce amekataa kuondoa uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka klabu hiyo mwezi huu. (Birmingham Mail)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anatarajiwa kusisitiza ombi lake kwa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley na mkurugenzi mkuu Lee Charnley kuhakikisha kuwa wachezaji wanasaini kandarasi mpya kabla ya kukamilika kwa muda wa mwisho aliouweka wa tarehe 20 Januari. (Newcastle Chronicle)
Meneja Biashara na Masoko wa Kampuni ya Premium Agro Chem Ltd, Brijesh Barot (kulia), akiangalia upakiaji mbolea uliofanyika katika maghala ya kampuni hiyo, Vingunguti jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mbolea ikipakiwa katika malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Premium Agro Chem Ltd imeendelea kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli kwa kusambaza mbolea kwenda mikoani kwa masaa yote bila ya kujali mapumziko ya Sikukuu ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar inayofanyika leo nchini kote.
Akizungumza na waandishiwa habari wakati akisimamia upakiaji wa mbolea hiyo kwenye maghala ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo, Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Brijesh Barot, alisema kwamba kwa jana wamesambaza mifuko 20,563,000 sawa na tani 1,028 na kuwa mbolea hiyo inasambazwa kupitia kwa mawakala wao.
"Tunaendelea kusambaza mbolea kwa mikoa yote, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe na Katavi, kupitia kwa mawakala pamoja na kuwatumia maafisa wetu walio katika vituo vya matawi yetu huko kwa ajili ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima vijijini," alisema Barot.
Barot alisema kuwa kwa leo watasambaza mifuko 1,200 sawa na tani 600 na hiyo ni kwa mbolea aina ya Urea ambapo alisema usambazaji unaendelea vizuri.
Alisema kampuni yao inafanyakazi kazi hizo kizalendo ndiyo maana wamekubali kuuza kwa bei elekezi mbolea ambayo wao walikuwa wameinunua muda mrefu kabla ya kutolewa kwa maagizo ya kununua kwa mfumo maalum wa serikali, na hili linafanywa kwa kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.
Wasichana katika eneo moja nchini Ghana wamepigwa marufuku kuvuka mto mmoja wanapopata hedhi, na pia kuuvuka mto huo Jumanne.
Marufuku hiyo, ambayo inadaiwa kutolewa na miungu wa mto wa eneo hilo imeshutumiwa sana na wanaharakati watetezi wa haki za watoto. Hii ni kwa sababu wasichana wengi hulazimika kuvuka mto huo kufika shuleni. Hii ina maana kwamba wasichana wa wilaya ya Denkyira ya Juu Mashariki, katika mkoa wa kati, wanakabiliwa na hatari ya kutopata elimu.
Mataifa mengi Afrika kusini mwa jangwa la Sahara yamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanafunzi wa kike wanasalia shuleni wakati wanapopata hedhi. Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi na Elimu, Unesco, linakadiria kwamba asilimia kumi ya wasichana Afrika kusini mwa jangwa la Sahara huwa hawahudhurii masomo shuleni wanapopata hedhi. Ripoti moja ya Benki ya Dunia inasema wanawake 11.5 milioni nchini Ghana hukosa huduma na vifaa vya usafi. Balozi wa usafi wakati wa heshi wa Unicef Shamima Muslim Alhassan ameambia BBC Pidgin kwamba amri hiyo kuhusu sehemu ya Mto Ofin inakiuka haki ya wasichana kupata elimu. "Inaonekana miungu hawa wana nguvu sana, si ni kweli?" alisema. "Wakati mwingine huwa nafikiri tunafaa kuomba uwajibikaji kiasi kutoka kwa miungu hawa wanaoendelea kuzuia mambo mengi yasifanyike, wawajibishwe kuhusu jinsi wanavyotumia mamlaka haya makubwa ambayo tumewapa." Waziri wa mkoa wa kati Kwamena Duncan ametoa ishara kwamba atashirikiana na mwenzake wa mkoa wa Ashanti kutafuta suluhu. Mto wa Ofin ndio mpaka kati ya mikoa ya Ashanti na Kati. Katika jamii nyingi huwa kuna itikadi nyingi na miiko kuhusu hedhi. Nchini Madagascar, baadhi ya wanawake hutakiwa kutooga wanapopata hedhi na Nepal wengine hulazimika kulala katika vyumba maalum mbali na familia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akionyesha fimbo ya kimasai baada ya kupewa cheo cha kiongozi wa kimila Olaigwanani rika ya Korianga akizungumza na wakazi wa akiwa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akisalimiana na wananchi wakati akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Na Mathias Canal, Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu utendaji wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi ya watanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa ziarani Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Kheri alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameamua kusafisha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu yeyote kusalia kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa maslahi ya Taifa.
Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka 2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.
Alisema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua Kali za kisheria dhidi ya yeyote atakayetaka kuvuruga ama kuleta uvunjifu wa amani Siku ya uchaguzi.
"Ndugu zangu wana Mrandarara nataka niwasihi na kuwahakikishia kuwa MTU yeyote atakayeleta masihara na mchezo mchezo Siku ya uchaguzi anapaswa kuchezewa yeye mchezo mpaka ashike adabu" Alikaririwa Kheri
Alisema kuwa Mara baada ya Mbunge kuchaguliwa tu anapaswa kusimamia vyema asilimia 5% za fedha za mfuko wa vijana zinazotolewa na Halmashauri sambamba na asilimia 5% kwa ajili ya wanawake ili kuendeleza chachu na imani ya vijana na wananchi kwa ujumla dhidi ya serikali yao.
Aliongeza kuwa kumchagua mbunge wa CCM itampendeza zaidi Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Magufuli kwani atakuwa amepata msaidizi kwa ngazi ya Jimbo atakayetekeleza vyema ilani ya CCM ambayo imeainisha mambo mengi muhimu na msingi kwa maslahi ya watanzania wote hasa wananchi wa Longido.
Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Longido na majimbo mengine matatu likiwemo Jimbo la Singida Kaskazini na Songea Mjini utafanyika tarehe 13 Januari 2018.
Wakati huo huo akiwa Kijijini Mairowa Kata ya Ngarenaibor Mwenyekiti Kheri amewataka mawakala wa CCM kote nchini kuwa waaminifu katika kusimamia vyema chaguzi mbalimbali kote nchini kwani wameaminiwa na Chama hivyo kutojihusisha na viashiria vya aina yoyote ya rushwa.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.
Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.
Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.
mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Januari 12 ya mwaka huu wa 2018 Wazanzibari pamoja na Watanzania kwa ujumla watakuwa wakiadhimisha miaka 54 tangu kutokea kwa mapinduzi Visiwani Zanzibar mnamo Januari 12, 1964. Mapinduzi ambayo yaliyofanywa na wanamapinduzi wa kiafrika na kupelekea kuung’oa utawala wa kisultani na kiarabu visiwani humo na kuwa na utawala wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pamoja na siku hii kuadhimishwa kila mwaka, bado kuna watu wengi hawafahamu mambo muhimu kuhusu historia ya Zanzibar na yaliyopelekea mpaka mapinduzi kutokea. Kutokana na umuhimu wa siku hii kwa vizazi vilivyopita, vya sasa na vijavyo, Jumia Travel imekukusanyia mambo muhimu ambayo huna budi kuyafahamu.
Ikiwa na historia ndefu ya utawala wa Kiarabu tangu mwaka 1698, Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya nchi ya ng’ambo ya Oman mpaka ilipojitwalia uhuru wake mnamo mwaka 1858 na kuwa chini ya utawala wake wenyewe wa Kisultani.
Wakati wa utawala wa Sultani Ali Ibn Said mnamo mwaka 1890, Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza mpaka mwaka 1963 ilipowapatia wanzibar uhuru wao, ingawa haikuwahi kuwa chini ya utawala rasmi wa moja kwa moja wa dola ya Kiingereza.
Wananchi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa walikuwa ni mchanganyiko kutoka mataifa mbalimbali kama vile Waarabu, Wahindi, Waajemi, Washirazi na Waafrika, ambapo waarabu na wahindi ndio kwa kiasi kikubwa walikuwa wamehodhi ardhi na shughuli kuu na njia za biashara. Kadri muda ulivyozidi kwenda maingiliano baina ya watu wa mataifa hayo yalizidi kuongezeka kitu kilichopelekea utofauti baina yao kuanza kufifia.
Hata hivyo, walowezi wa Kiarabu kama wamiliki wa sehemu kubwa ya ardhi ya visiwani humo ndio walikuwa ni matajiri kuliko waafrika. Suala hilo pamoja na mambo mengine mengi ni miongoni mwa sababu zilizopelekea waafrika kuona sababu ya kufanya mapinduzi ili kuwa na utawala wa haki na usawa visiwani humo.
Kwa upande wa kisiasa, vyama vikuu visiwani Zanzibar vilikuwa vikiendeshwa na kuungwa mkono kulingana na utaifa (ukabila), kama vile Waarabu walikuwa wakitawala kwa sehemu kubwa ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) huku Waafrika ilikuwa ni Afro-Shirazi Party (ASP).
Baada ya Zanzibar kutwaliwa na utawala wa Kisultani wa Oman mnamo mwaka 1698, sehemu ya ardhi yote visiwani humo iligawiwa kwa wanafamilia wa Kifalme wa Oman, ambapo vizazi vyao viliendelea kuimiliki mpaka mwaka 1964.
Ingawa sio Waarabu wote walikuwa ni matajiri kama familia ambazo zilikuwa zikimiliki mashamba ya karafuu na minazi, hasira ambayo waliyokuwa nayo waafrika ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye mashamba hayo ilipelekea kujisikia hali ya kubaguliwa kwenye ardhi yao wenyewe. Hususani kwa kisiwa kidogo kama cha Zanzibar ambapo ilikuwa ni rahisi kuona pengo na utofauti mkubwa kati ya familia tajiri za kiarabu zilizokuwa zinamiliki ardhi na vijakazi wao masikini wa kiafrika.
Harakati za kutaka uhuru Visiwani Zanzibar zilianza kutokana na vuguvugu za shughuli za kisiasa ambapo kwa kiasi kikubwa waafrika hawakuwa wanapata uwakilishi sawa na nafasi bungeni. Kuanzia mwaka 1961 na kuendelea kulianza kufanyika kwa chaguzi za kisiasa za kidemokrasia ambapo vyama vikuu vya ASP na ZNP vilikuwa vikichuana vikali.
Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na waafrika wengi cha ASP kilikuwa kikiendelea kuungwa mkono na kukubalika miongoni mwa waafrika wengi. Katika maeneo mengi kulipokuwa kunafanyika chaguzi kilionekana kuungwa mkono ingawa matokeo ya uchaguzi yalipotoka yalikuwa yanaonyesha kushinda sehemu chache.
Sababu hiyo ambayo ilikuwa ikijirudia mara kwa mara kwenye kila chaguzi ndiyo iliyopelekea waafrika kuona haja ya kufanya mapinduzi. Mnamo Januari 12, 9164 mapinduzi yalifanyika visiwani Zanzibar na kumfanya kiongozi wa chama cha ASP, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais mpya na kiongozi wa nchi.
Mapinduzi hayo yalipelekea ukomo wa utawala wa kiarabu visiwani Zanzibar wa takribani miaka 200, hivyo kuifanya siku hiyo kusherehekewa kwa maadhimisho maalum na kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Godfrey Chongolo (kulia) akimkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kheri James aliyewasiri wilayani humo kfanya kampeni za uchaguzi za mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho.
Dege la kisasa aina ya Boing 787 lenye kupakia zaidi ya abiria 200 lililonunuliwa na Kenya Airway. Dege hilo litakuwa linatoka moja kwa moja Nairobi hadi New York, Marekani kwa kutumia masaa 15.
Madereva Bodaboda wa wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamekula kiapo cha uaminifu cha kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ngono na mimba za utotoni zinazo sababisha kukatisha haki yao ya kuendelezwa.
Kiapo hicho kimeongoza na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Kampeni ya “Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima” iliyozinduliwa tarehe 11 Oktoba, 2017 kwa lengo la kuhamasisha wananchi kupambana na kuzuia matukio ya mimba za utotoni katika jamii zetu.
Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kutokomeza mimba za utotoni hatuna budi kuweka ushirikiano baina ya wazazi, walezi, jamii, Serikali na wadau wengine ili kuwaepusha watoto wa kike kupata vishawishi vya mahusiano ya kingono katika umri mdogo na hatimaye kupata mimba za utotoni.
Ameongeza kuwa lengo la Kampeni ya “Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” imelenga kuunganisha nguvu za pamoja za wanajamii wakiwemo madreva wa Bodaboda kushirikiana na Serikali kuzuia na kutokomeza matukio ya mimba za utotoni katika ngazi ya jamii na shuleni.
“Niseme kampeni hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuunganisha nguvu zetu kama wananchi na sisi Serikali katika kutokomeza vitendo hivi viovu”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amewaasa madereva hao kuondokana na tamaa za kujihususha na mahusiano na kingono na watoto wadogo bali wao kuwa walinzi wao katika kutokomeza suala mimba kwa watoto wetu.
Amewataka kufichua vitendo vyovyote vyenye ushawishi wa mahusiano yanayosababisha mimba kwa watoto wa kike ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuweka mikakati ya kupambana na wanaume na vijana wakware wanaotumia fursa zao kuwa na mahusiano maovu na watoto wa kike katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambao ndio unaoongoza kitaifa kwa kuwa na asilimia 45.
Mmoja wa dereva Boda boda wa Wilaya ya Mpanda Bw. Juma Salum kwa wakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kuandaa Kampeni hiyo itakayowajengea uelewa wananchi kusaidiana katika kuwalinda watoto wa kike kwa kuweka miundo mbinu salama ya kusomea na kujifunzia ili kupunguza kiwango cha mimba za utotoni kwa silimia 50 ifikapo mwak 2021/22.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) alikuwa na ziara ya siku mbili mkoani Katavi kuhamasisha wananchi kupambana na kuzuia mimba za utotoni kupitia “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kiti cha Udiwani katika Kata ya Kimandolu Arusha, baada ya mgombea wake, Gaudence Lyimo kupata kura 8,981 na kumzidi mgombea wa CUF aliyepata kura 1,251.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kiti cha Udiwani katika Kata ya Kurui Wilaya ya Kisarawe, Pwani baada ya mgombea wake, Mussa Kunikuni kupata kura 632 na kumzidi mgombea wa CUF mwenye kura 185.