Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21765 articles
Browse latest View live

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0
Waziri mkuu Kassim Majaliwa asema halmashauri za wilaya, miji na majiji zitakazoshindwa kukusanya mapato kwa asilimia 80 zitafutwa.https://youtu.be/LGpSrwo9ksc
Jeshi la wananchi watanzania JWTZ kwa kushirikiana na umoja wa mataifa limesema litafanya uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaodaiwa kufanya vitendo vya unyanyasaji nchini Congo. https://youtu.be/kndyFLxcAVE
Mahakama ya Kisutu ya jijini Dar es salaam yawanyima dhamana kamishina mkuu wa TRA wa zamani pamoja na wenzake 2 ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mshitaka 4 ikiwemo utakatishaji fedha. https://youtu.be/2aQoBHWWJDo
Polisi kanda maalum ya Dar es salaam yawakata watuhumiwa 63 wa ujambazi na silaha 6. https://youtu.be/cM2nxpweQF4
Serikali imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa sekta ya usafiri wa reli na anga katika juhudi za kukuza uchumi wa nchi. https://youtu.be/_3LKRnzdAos
Waziri wa nishati na madini Prof. Muhongo atoa agizo kwaa wafanyakazi wote wa wizara ya nishati na madini walio na vitalu vya madini kuchagua moja kati  ya kuendelea kuajiriwa na kuacha vitalu vya madini au waache kazi waendelee na vitalu vya madini.https://youtu.be/vWLL61BECXY
Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na vitendo yasema itaendelea kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kufungua maduka ya dawa katika kila makao makuu ya mkoa ili kurahisha upatikanaji wa dawa kwa wananchi katika hospitali mbalimbali.https://youtu.be/qRfuWiwHGKI

Moto mkubwa wateketeza mabweni ya shule ya sekondari Soni Day wilayani Lushoto na kusababisha hasara ya takribani milioni 167.https://youtu.be/26_sGAvrZXo
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam yawatia mbaroni watuhumiwa 63 wa ujambazi huku pia likikamata silaha 6 katika msako maalum. https://youtu.be/6GbQSYE_Tgs
Waziri mkuu Kassim Majaliwa azitaka jumiya za serikali za mitaa nchini ALAT kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kupambana na rushwa na uvujaji wa mapato. https://youtu.be/K_g7rz1YacY

Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ, laeza kushitushwa na taarifa za kulituhumu jeshi hilo juu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi wa Congo huku liki ahidi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kali. https://youtu.be/tC8hmY2qW_0

Nyumba zaidi ya 12 zimeanguka kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora na kusababisha kaya kadhaa kukosa makazi.https://youtu.be/kqql6EYVt3c
Serikali yasema bajeti ya dawa kwa mwaka ujao wa fedha 2016/2017 itakuwa ni zaidi ya mara 3 ya bajeti ya mwaka uliopita ili kuondoa tatizo la dawa na vifaa tiba katika hospitali, vituo vya afya na zahanati nchini. https://youtu.be/Dn--9A4BWXQ

Hatimae ofisi ya madini ya mkoa wa Geita yaufungua mgodi wa Mgusu baada kufungwa hapo awali kwa takribani mwezi 1 kufuatia vifo vya watu 5. https://youtu.be/apX7zOr80PI


DONDOO ZA MAGAZETI

HOSPITALI YAKABILIWA NA UHABA WA VYUMBA VYA KUHUDUMIA WAGONJWA

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza na Wagonjwa katika Hospitali ya Ngarenaro iliyoko jijini Arusha ,hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na gari la wagonjwa
Na Woinde Shizza,Arusha.
Hospitali ya Ngarenaro inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na kukosekana kwa miundombinu imara ya maji katika chumba cha upasuaji hivyo kuhitaji upanuzi pamoja na ukarabati wa hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000 wa kata ya Ngarenaro jijini Arusha.
Akizungumzia changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo Josephat Kivuyo katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa hospitali hiyo inahitaji upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha huduma za afya ambazo zinahitajika na wananchi wengi.

Daktari huyo Mfawidhi alisema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la zamani na haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wananchi na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya ukarabati ambao tayari umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa wananchi na wahudumu wa afya.

Pia Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa na kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya ambayo inahudumia watanzania wengi.Alisema Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na tayari hivyo nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika kuhakikisha kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma za afya.

VITUO VYA POLISI VYAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UCHAKAVU

$
0
0


Na Woinde Shizza,Arusha.
Vituo vingi vya polisi hasa vile vilivyopo pembezoni mwa miji vimekua vikikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo,uhaba wa majengo pamoja na vitendea kazi suala ambalo linapunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake Liberatus Sabas amesema kuwa uhaba wa majengo na vituo katika maeneo ya vijiji umekua ukipunguza ufanisi wa kazi ya polisi katika kulinda raia na mali zao hivyo ameitaka serikali kukarabati vituo hivyo pamoja na kuweka vitendea kazi vya kutosha.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo kipya cha polisi cha Tengeru kilichozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa hatua ya kuboresha vituo vya polisi itasaidia kutatua kero za kiusalama zinazokabili maeneo mengi mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua baadhi ya polisi ambao huwabambikia wananchi na kujihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo huwaumiza wananchi wengi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza kila mara

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA WATAFITI TOKA WASHINGTON DC-MAREKANI.

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Bwana Tye Ferrell kutoka Shirika la Utafiti la Tetra Technology lililopo nchini Washington DC Marekani, pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala (katikati) wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 08 Aprili, 2016.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimweleza jambo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala (katikati) wakati wa mazungumzo katika ofisi ya Mhe. Spika jijini Dar es Salaam leo 08 Aprili, 2016.
Mtafiti toka Shirika la Utafiti la Tetra Technology lililopo nchini Washington DC Marekani Bwana Tye Ferrell akimweleza jambo Mhe. Spika Job Ndugai (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo katika ofisi ya Mhe. Spika jijini Dar es Salaam leo 08 Aprili, 2016.
Watafiti kutoka Shirika la Utafiti lililopo Washington DC-Marekani Bwana Patrick McGoven (kushoto) pamoja na Bwana Tye Ferrell wakimsikiliza Mhe. Spika Job Ndugai (hayupo pichani) wakati akiongea, wakati walipomtembelea ofisini kwake leo 08 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 09.04.2016

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AMBAYE NI BALOZI WA KAMPUNI YA STARTIMES ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI YA MAJI MATITU MBAGALA JIJINI DAR

$
0
0

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (wa pili kushoto), akitoka kusaini  kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi ya Majimatitu baada ya kufika shuleni hapo leo asubuhi kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanao soma kwenye shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi. Wengine ni walinzi wake.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi, akimkaribisha mchezaji huyo shuleni hapo. Kutoka kulia ni Mwalimu Shabani Msabaha wa shule hiyo, Mchezaji Kanu na Makamu Rais wa Kampuni ya StarTimes, Zuhura Hanif.
Mchezaji Kanu akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Hapa Kanu akimkabidhi msaada wa sabuni ya unga Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi.
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wazazi wa watoto wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kanu akitoa msaada wa magodoro.
Kanu akitoa msaada wa vyombo vya jikoni kwa wanafunzi hao.
Hapa Kanu akikabidhi unga wanafunzi hao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto hao, Rehema Lemway na kulia kwake ni Mlezi wa watoto hao, Somoe Said Omary.
Kanu akiwakabidhi wanafunzi hao Luninga.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Kanu akishiriki kucheza na watoto hao wakati wakitoa burudani.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto hao.
Hapa Kanu akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya

$
0
0


Waziri Ummy Mwalimu azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya
0f5c4672-9fd5-4bcf-87cc-9862e000a1c2
Na Rabi Hume, Modewjiblog

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.

“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa, “Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.

Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
0f5c4672-9fd5-4bcf-87cc-9862e000a1c2
Mh.Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e
2ff7c78a-1555-486b-93f6-19118e784a78
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo
7a1d5446-ae11-4b37-946b-337d47d8e85c
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya
18f8ebf2-a48e-4f8d-ae8a-99ce5c23f6ac
Duka la Dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Kanda ya Mbeya ambalo litahudumia mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
e38d5120-d82d-496e-85f2-e82f53d9dcbb
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.


HABARI MPASUKOO!!!!!! MWANAMUZIKI NDANDA KOSOVO AMEFARIKI DUNIA

$
0
0
Mwanamuziki wa Kikongo, Ndanda Kosovo, amefariki leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwanamuziki mwenzie  Dodoo, amesema kuwa  Kosovo ambaye awali alilazwa  Hospitali ya Mwananyamala amepatwa baada ya kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Kosovo 'Kichaa', amweahi vuma na bendi za FM, Stono Musica aka Wajelajela Agwaa.

Blogu hii itaendelea kuwapatia taarifa za msiba huo kadri tutakavyokuwa  tunazipata.

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina

TRA YAENDELEZA ZOEZI LA KUBOMOA MTANDAO WA WAFANYA BIASHARA YA MAGENDO UKANDA WA KUSINI MWA PWANI

$
0
0


Na Mwandishi Wetu-Kilwa.

Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST)  wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh.

Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu.

Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko762Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135,Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49,Betri aina ya tigger katoni 223,Amira katoni 135,Sabuni za kufulia katoni 48

Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari.Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya Kilombero,TPC na Mtibwa Sugar.
Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India  2000
Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari36,000
mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo25 kiasi cha 1150
Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609
Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Nyumba hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo hutumika kuweka bidhaa kabla ya kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.
sehemu ya kuweka sukari na kupima.
Nyumba inayotumika kuweka sukari
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayomboakionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.
Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA 
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni
Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.
Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta
Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda.

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI ZA MKOA WA MBEYA

$
0
0

8e796dee-b674-43f7-97f8-3bad1046087d
Na Catherine Sungura, Mbeya
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika hospitali zilizopo Mbeya na kuzitaka hospitali zinazotumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa kieletroniki wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.
Rai hiyo imetolewa na aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya mjini Mbeya.
Ummy alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa, vifaa na vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi.
“Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote, tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa,” alisema.
Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma, hivyo wameishauri Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa dawa kwa haraka.
Waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa.
“Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka ya dawa binafsi, hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka mahakamani”
Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini, Waziri wa afya alisema, nchi ina upungufu wa asilimia 52, hivyo serikali inatarajia kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni.
Katika hospitali ya uzazi ya Meta, waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na watoto njiti.
Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi Milioni mia tano na pia inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu milioni mbili.
46e02c3a-bc41-4fed-9ff6-a180f42fa264
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mbeya.
afc64d2e-46a1-49a8-be9b-59340b6d8a8a
Waziri Ummy akimsalimia mtoto Jenifer Joel (9) mkazi wa Chunya aliyelazwa hospitalini hapo.
5f7ab771-5109-4c0c-95e6-83931c8ec108
Waziri wa afya akimjulia hali mtoto Baraka Jekonia (1) mkazi wa Chunya aliyelazwa wodi ya watoto, Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kuwachaji pesa wagonjwa wote wanaofika hospitali ya rufaa moja kwa moja bila kupatiwa rufaa kutoka vituo vya afya vilivyopo jirani na wananchi ili kupunguza msongamano kwenye hospitali za rufaa nchini.
8e796dee-b674-43f7-97f8-3bad1046087d
Katika hospitali ya uzazi ya Meta, Waziri Ummy Mwalimu alimsalimia Binti Kanisia Komba aliyejifungua mtoto wa kike katika hospitali hiyo mama wajawazito wote wanatibiwa kwa kadi ya bima ya afya inayodhaminiwa mpango wa kusaidia akina mama wajawazito wa KFW toka Banki ya Ujerumani.
9518e21d-3e1e-43ad-a96a-c9b85ce91018
Hospitali ya Meta tayari imetekeleza maagizo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ya kutoa kipaumbele kwa wazee wote nchini wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma.
974627cc-137b-436b-996a-f364952f7580
Waziri Ummy akiwasalimia wazazi waliolazwa kwenye moja ya wodi Hospitali ya Meta kutokana na ufinyu wa wodi inawalazimu akinamama wengine kulala chini hospitali hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo jipya ambalo litaondoa msongamano wa wazazi hospitalini hapo.
5b44d003-a727-495c-bde5-dea332ef407f
Waziri wa Afya akiwasalimia wagonjwa waliofika Hospitali ya Uzazi ya Meta kupata matibabu.

MUOGELEAJI NYOTA WA TANZANIA SONIA TUMIOTTO AWASILI

$
0
0

01Katibu Mkuu wa klabu ya Dar Swim Club (DSC), Inviolata Itatiro (kushoto) akikabidhi shada la maua kwa muogeleaji aliyeshinda medali tatu mjini Dubai, Tumiotto (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jana. Kati kati ni katibu mkuu wa chama cha kuogelea (TSA), Ramadhan Namkoveka.
02Muogeleaji nyota wa Tanzania, Sonia Tumioto akizungumza huku akifuatiwa kwa umakini mkubwa na kocha wake, Michael Livingstone
03Kocha wa Sonia, Michael Livingstone akizungumza mara baada ya Sonia kuwasili huku Sonia akifuatilia.
04Katibu Mkuu wa chama cha kuogea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka akizunguza huku Sonia akisikiliza.
05Meneja wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Leena Kapadia akizungumza mara baada ya kuwasili huku sokia (kulia) na kocha wake, Michae Livingstone akifuatilia.
06Picha ya pamoja baada ya Sonia kuwasili.
Picha na mpiga picha wetu.

BREAKING NEWS: Dkt Shein atangaza baraza lake la mawaziri

$
0
0


Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza jipya Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.
Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo la Mapinduzi kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7 na taasisi za wizara alizozivunja amezihamishia ambapo  katika baadhi ya wizara za sasa.
mawaziri hao watawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
      Mhe. Issa Haji Ussi Gavu.

2). Wizara nchi Afisi ya Rais Katiba  Sheria Utumishi wa Umma na utawala bora – 
     Mhe. Haroun Ali Sleiman.
    Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Katiba .Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora 
      Mhe. Khamis Juma Maalim.  

3). Wizara ya nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ 
      Mhe. Haji Omari Kheir.

4). Wizara ya nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa  Rais 
      Mhe. Mohammaed  Aboud. Mohammed

5). Waziri wa Fedha na Mipango 
      Mhe. Dk. Khalid Salum Mohd.

6). Wizara ya Afya
      Mhe Mahmoud Thabit Kombo.
Naibu Wizaya ya Afya .
      Mhe.Harusi Said Suleiman.

7). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
      Mhe.Riziki Pembe Juma 
Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali.
      Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri.

8). Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
      Mhe. Balozi Amina Salum Ali.

9). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji
     Mhe Balozi Ali Karume 
Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji 
Mhe.Mohamed Ahmed Salum.

10). Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo 
         Mhe.Rashid Ali Juma 
Naibu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo.
          Mhe.Chumu Kombo Khamis.

11).Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi
        Mhe.Hamad Rashid Mohd 
Naibu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi.
   Mhe.Lulu Msham Juma.

12).Wizara ya  Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
        Mhe.Mauldine Castiko.

13). Wizara ya Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
       Mhe.Salama Aboud Talib.
 Niabu Waziri Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
       Mhe.Juma Makungu Juma.

YANGA, WAARABU NGOMA DROO

$
0
0
YANGA SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo, Yanga italazimika kwenda kushinda ugenini ili kutimiza ndoto za kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yao baada ya mwaka 1998.
Katika mchezo wa leo, mabao yote yalipataka kipindi cha kwanza, Ahly wakitangulia kufunga kupitia kwa mshambuliaji wake mjanja, Amr Gamal, kabla ya Yanga kusawazisha la ‘ngekewa’ la Issoufou Boubacar.






VIDEO YA BAO LA SAMATTA JANA UBELGIJI

$
0
0


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao katika ushindi wa 4-0 wa klabu yake, KRC Genk dhidi ya KV Oostende katika Ligi Kuu ya Ubelgiji. Tazama video chini;

ENZI ZA DIAMOND PLATINUMZ

JWTZ YAKANA UZUSHI KUHUSU UNYANYASAJI HUKO DR-CONGO

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 10.04.2016

MWALIMU: KIPINDUPINDU HAKIENEZWI KWA KUROGWA

$
0
0

indexnn
Na.catherine Sungura,Kyela 
Wananchi wa wilaya ya kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoletwa kwa imani ya kishirikina
Hayo yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto  Ummy Mwalimu,wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea na watendaji wa halmashauri.
Mh.Ummy alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha unyakyusa kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio wanaoneza ugonjwa huo.
Naye mkuu wa wilaya ya kyela dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya malawi anatafutwa.
Matukio hayo yametokea mwezi februari na machi mwaka huu.
Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu
Hali ya kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini,takribani mikoa yote tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi agosti mwaka jana,isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa wowote hadi Sasa
Ripoti ya wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya tarehe 4 machi mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na kati ya hao 320 wamepoteza maisha.
Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA UJENZI WA FLOW METER.

$
0
0

KIV
Meneja wa mradi wa Ujenzi wa Flow Meter ya Kigamboni Eng. Mary Mhayaya akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi huo.
KIV1
Muonekano wa Flow Meter mpya ya Kigamboni katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
KIV4
Muonekano wa Daraja la Kigamboni mara baada ya ujenzi wake kukamilika.
KIV3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni (kushoto) na Nahodha wa kivuko hicho (kulia) wakati alipokikagua.
KIV5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelekezo kwa Mkurugenzi Msaidizi Barabara za Mijini Eng. Hussein Mativila (kushoto) alipokagua Daraja la Kigamboni.
………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mtambo mpya wa kisasa wa kupima mafuta yanayoingia nchini flow meter unaojengwa Kigamboni jijini Dar es salaam uko katika hatua za mwisho za kukamilika kwake na utaanza kazi rasmi mapema mwezi ujao.
Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokagua mtambo huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na kuhimiza waendeshaji wa mtambo huo wawe watu wenye uadilifu wa hali ya juu na elimu ya kutosha ili kuulinda na kuwezesha kufanyakazi inavyostahili.
“Hakikisheni mnawasiliana na Wakala wa Vipimo nchini (WMA), ili wahakikishe mtambo huu unaviwango vinavyotakiwa vitakavyowawezesha wafanyabiashara wa mafuta kuridhika na ufanyakazi wa mtambo huu ili kuondoa malalamiko”, amesema Prof. Mbarawa.
Zaidi ya shilingi bilioni 12 zimetumika katika ujenzi wa mtambo huo ambao utawezesha Serikali kupata mapato stahiki na wafanyabishara kupata mafuta sahihi kwa mujibu wa mahitaji yao.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni na kuwataka wananchi kuhakikisha wanalitumia daraja hilo kwa usahihi na kuepuka vitendo vyote vya hujuma.
Amesema daraja hilo lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 214 linatarajiwa kufunguliwa rasmi Aprili 16 na litakuwa na njia sita za magari na mbili za watembea kwa miguu.
“Nawataka wananchi na watumiaji wote wa daraja hili kuhakikisha kuwa miundombinu ya daraja haihujumiwi na watu wenye nia mbaya kwani vitendo vya aina hiyo licha ya kuharibu daraja vitahatarisha usalama wa watumiaji”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Naye Msimamizi wa Daraja hilo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. Karim Mataka amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni umekamilika katika hatua zote na kinachosubitriwa na ufunguzi na kuanza kutumika.
Amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya daraja hilo kwa madereva na watembea kwa miguu ili kuepuka usumbufu siku za mwanzoni.
Daraja hilo litakalofunguliwa rasmi Aprili 16 litapunguza msongamano wa usafiri kwa wakazi wa kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam.
Viewing all 21765 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>