Quantcast
Channel: Kamanda wa Matukio OnlineTv
Viewing all 21765 articles
Browse latest View live

HATIMAYE MAMA CLINTON KUGOMBEA TENA URAIS 2016

$
0
0


Bibi Hillary Clinton Mke wa Rais wa Marekani wa zamani na Waziri wa nje wa Marekani alimaliza mda wake.
Ametangaza Rasmi anagombea #2016... na amezindua Kampeni yake Jana kupitia chama cha Democratic...Rais wa Marekani Barack Obama alipulizwa jana huko Panama...Anamzungumzaje Bi Hillary Clinton....? Anajibu...... "Namfahamu Kama Mwana mama mshindani wangu 2008...
Namjua Kama Msaidizi Wangu akiwa Secretary of state (Waziri wa mashauri ya Ligeti) Na bado ni Rafiki yangu sana kisha akasema ni mwanamama amayeweza kuiendeleza Amerika...

MRISHO MPOTO AIBIWA VITU VYA NDANI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SABA

$
0
0




Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amejikuta mpweke baada ya kupuliziwa dawa na wezi na kuibiwa vitu vya ndani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7 usiku wa kuamkia leo. Akizungumza na mtandao huu kwa masikitiko, Mpoto 
amesema wezi hao huenda waliwapulizia dawa hali ambayo ilisababisha kutoshtukia mchezo huo.

Sehemu ya TV na radio
“Yaani wamesafisha kila kitu,” amesema Mpoto. “Hapa sebuleni hakuna kitu yaani. Mimi mwenyewe nilikuwepo sema labda ni kwa sababu nyumba kubwa pia tunahisi labda walitumia dawa kwa sababu sio kawada nikalala hivyo bila kusikia kinachoendelea. Nahisi walitupulizia dawa za usingizi. Pesa nyingi sana ni zaidi ya milioni 7, sema tayari suala nimelifikisha polisi na wanaendelea na upelelezi. Wameiba vitu ni vingi, flati screen, maredio yaani ni vingi.”



CHANZO: BONGO 5

FAMILIA YA EDWARD MORINGE SOKOINE WAFANYA MISA YA KUMKUMBUKA BABA YAO

$
0
0

Familia aliye kuwa waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika ibada maalumu ya maadhimisho ya kifo chake  nyumbani kwake monduli juu, siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka
Wake wa  aliye kuwa  waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine  , wakiweka  mashada ya maua kwenye kaburi la  mume wao nyumbani kwake eneo la monduli Juu wilayani monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka.

Watoto wa kiume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Joseph Sokoine,Tumaini Sokoine na Ibrahimu Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.

Watoto wa kike wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Maria Sokoine,Joyce Sokoine ,Mbunge wa Viti Maalum Namelock Sokoine na Seki Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.
 Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akiwa na kaka yake ibrahim Sokoine katika kumbukumbu ya kifo cha baba yao aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
 Mbunge wa Viti Maalum na Mtoto wa  aliye kuwa waziri mkuu  wa zamani   hayati Edward Moringe Sokoine, Namilock Sokoine akiongea na baadhi ya wazee wa kimaasai baada ya misa maalumu ya maadhimisho ya kifo  cha Sokoine amabayo yalifanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Monduli juu wilayani Monduli mkoani Arusha jana.
 Mbunge wa viti maalum, Namelock Sokoine akizungumza na wadau 

BODI YA MANUNUZI NA UGAVI (PSPTB) YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU MBEYA.

$
0
0
1
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Winfrida Igogo akitoa mada katika mafunzo ya wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika Chuo cha TIA Mbeya.
13
Wanafunzi ambao wanasoma masomo ya manunuzi na ugavi wakifuatilia mafunzo yaliyotolewa na Bodi ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu Mbeya.
………………………………………………
Na Mwandishi wetu
BODI ya manunuzi na ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo kwa wanafunzi waosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu(TIA) Mbeya.
Katika mafunzo hayo wito ulitolewa kwa Taasisi binafsi na serikali kuepuka kutoa ajira katika sekta ya manunuzi na ugavi kwa watu ambao hawana taaluma hiyo wala kusajiliwa na Bodi ya PSPTB.
Wito huo ulitolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Manunuzi na ugavi(PSPTB), Winfrida Igogo, alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa Wanafunzi wa taasisi ya Uhasibu kampasi ya Mbeya ambao ni wanachama wa Umoja wa wanataaluma wa manunuzi na Ugavi(PSA-TIA) wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa TIA Mbeya.
Igogo alisema hairuhusiwi kwa mtu yoyote kufanya kazi za manunuzi na ugavi bila kuwa na utalaam pamoja na kusajiriwa na bodi kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria jambo ambalo adhabu inamkumba pia mwajiri.
Alisema lengo la kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na ugavi(procurement & supply)ni kuwajengea uwezo na kuwahamasisha juu ya taratibu wanazopaswa kuzifuata wakiwa kazini kuhusiana na manunuzi na ugavi.
Aliongeza kuwa lengo lingine ni kuwakumbusha wanataaluma hao kujisajili na bodi mara baada ya kuhitimu masomo yao jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa ajira haraka tofauti na wasio sajiliwa ambao hukaa muda mrefu bila ajira kutokana na kukosa kipengere cha uzoefu.
Alisema Bodi ipo kwa mujibu wa sheria ambapo hivi sasa ipo kwenye mchakato wa kupitia kila taasisi kukagua kama walioajiriwa wanasifa za manunuzi na ugavi ikiwa pia kupitia matangazo mbali mbali ya ajira kama vigezo vinavyowekwa vipo kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Mwezeshaji mwingine katika mafunzo hayo, Juvenal Joseph, alisema ni vema wataalamu wa manunuzi na ugavi wakazingatia sheria kwa kuepuka mikataba inayoweza kuwaingiza matatizoni.
Alisema wataalam wa manunuzi na ugavi wanapaswa kujua kuwa kila mikataba ni makubaliano lakini sio kila makubaliano yanaweza kuwa mikataba hivyo wajiepushe kutumbukia katika rushwa kwa kukiuka taratibu za manunuzi na ugavi.
Naye Mlezi wa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya aliyejitambulisha kwa jina moja la Mgaya alisema Wanafunzi wanaosomea masomo ya manunuzi na ugavi wanapaswa kuwa na nidhamu katika masomo yao ili kuepuka kuwa maafisa wav yeti.
Aidha Mwalimu wa Somo la Manunuzi na ugavi chuoni hapo, aliyejitambulisha kwa jina la Gasibila aliishukuru bodi kwa kuendesha mafunzo hayo na kuongeza kuwa jambo hilo litasaidia kuzalisha wahitimu wenye taaluma na kupata watumishi waliotukuka.
 
Aliongeza kuwa waalimu na watumishi katika fani ya manunuzi na ugavi wanategemea maelekezo kutoka miongozo kutoka bodi kwa kuwa wao ndiyo dira ya utumishi mzuri nchini.

KONYAGI YAWASOMESHA WANAFUNZI WA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

$
0
0

 Mratibu wa Mpango wa Somesha mtoto wa Mkulima wa zabibu ulidhaminiwa na Tanzania Distillaries LTD (TDL) Saimon Chibehe akizungumza jambo na wakulima wa zabibu pamoja na wanafunzi wa Kata ya Handari wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
 Mratibu wa Mpango wa Somesha Mtoto wa Mkulima wa zabibu unaodhaminiwa na Kiwanda cha Konyagi cha  Tanzania Distillaries LTD (TDL), Saimon Chibehe akizungumza jambo akizungumza na Wazazi, Walezi ambao ni wakulima wa zabibu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpunguzi iliyopo Manispaa ya Dodoma, MWISHONI MWA WIKI.
 Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Shule ya Sekondari Mvumi, mkoani Dodoma, Nuru Peter akiwa katika shamba la Zabibu la Wazazi Wake wakati alipofika kumuonesha Mratibu wa Mpango wa Somesha mtoto wa Mkulima wa zabibu ulidhaminiwa na Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distillaries LTD (TDL) Saimon Chibehe (hayupo pichani) mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mpunguzi wanaofadhiliwa na Konyagi kwa kulipiwa Ada, Sale za shule na bweni wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kibao cha shule hiyo iliyopo manispaa ya Dodoma.

TAZAMA MATUKIO YA KUSIMIKWA RASMI KWA ASKOFU WA JIMBO KUU LA SHINYANGA LIBERATUS.

$
0
0

Askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akiwekewa mkono kichwani.
Askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akiwekewa kitabu kichwani
Askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akipakwa mafuta.
Askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akikabidhiwa kitabu cha injili.
Askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akikabidhiwa bakora ya kiaskofu
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa akishikana mkono na askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu.
Rais Jakaya Kikwete akifuatilia kwa umakini ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa askofu Liberatus Sangu,kushoto kwake ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga,kulia kwake ni mwenyekiti wa Chama Cham Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Rais Kikwete akitoa salamu zake wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa askofu Liberatus Sangu.
Askofu wa jimbo kuu la Dar es salaam Kadinali Pengo(aliyekaa katikati) akiongoza sala ya Litania huku askofu mpya wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akiwa amejilaza chini wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa rasmi katika kanisa kuu la mama mwenye huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.

BONANZA LA TAASISI 15 LAFANA ARUSHA

$
0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Adollah Mapunda akikagua timu ya netiboli wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Wachezaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakifurahia zawadi ya kuku waliyotwaa baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya kukimbiza kuku wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha


Richard Mwangulube

Timu ya Soka  ya chuo cha ufundi Arusha (ATC) imefnikiwa kubeba kombe  la bonanza  baada ya kuilipua timu ya soka ya Benki Kuu Tawi la Arusha ( BOT mabao 3-0

Ushindi huo wa  timu ya ATC umekuwa faraja kubwa kwa  chuo hicho kutokana na mashindano hayo yaliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa mara ya kwanza

Katika bonanza hilo timu ya soka ya Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA)  ilishika  nafasi ya pili

Kwa upande wa netiboli timu ya RAS  Arusha  ilipata ushindi mnono baada ya  kuwaadhibu ndugu zao timu ya Jiji la Arusha katika mchezo wa fainali

Katika mchezo wa  draft ATC wanaume  imeibuka kidedea tena huku  timu ya  chuo cha uhasibu tawi la arusha ikishika nafasi ya pili

Kwa upande wa wanawake  Halmashauri ya Arusha (Arusha DC)  imefanikiwa kuinyuka  timu ya chuo cha uhasibu

Kuhusu mchezo wa  bao timu yaMamlaka ya Maji Arusha iliibuka na ushindi baada ya kuwacharaja vijana wa  kituo cha mikutano cha kimataifa AICC kwa upande wa wanaume

Katika mchezo w akarata  uhasibu wamepata ushindi  huku nafasi ya pili  ikichukuliwa na AICC upande wa wanaume

Katika mchezo huo wanawake  Jiji Arusha wameshika nafasi ya kwanza  ikifuatiwa na RAS Arusha

Katika kuvuta kamba wanaume  chuo cha uhasibu Arusha kimeshika nafasi ya kwanza  huku mshindi wa pili ikichukuliw ana  chuo cha ufundi Arusha upande wa wanaume

Kwa upande wa wanawake  kuvuta kamba  Timu ya Jiji Arusha  imefanikiw akunyakua nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliw ana  Ras Arusha

Katika mchezo wa kukimbia  na magunia wanaume taasisi ya utafiti TAWIRI ilishika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikinyakuliw ana AICC

Upande wa wanawake kukimbia na magunia  Uhasibu nafasi ya kwanza  huku nafasi ya pili ikichukuliw ana TAWIRI

Kuhusu mbio za  watu wazima  wenye umri  zaidi ya miaka 50 Ofisi ya RAS ilishika nafasi ya kwanza  ikifuatiwa na AICC upande  wa  wanaume

Upande wa wanawake  nafasi ya kwanza ilichukuliwa na TPRI huku nafasi ya pili ikichukuliwa na RAS ili kufanikisha bonanza hilo la kwanza  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felex Ntibenda aliunda timu ya watu 18 kutoka taasisi mbalimbali

Bonanza  la mwaka huku  ambalo ni la kwanza taasisi zipatazo 15   zimeshikiriki  katika mashindano mbalimbali  ukiwemo mchezo wa kufukuza kuku

Aidha washindi wa kwanza na  wa pili walizawadiwa vikombe na medali pamoja na  wengine kubahatika kupata zawadi ya kuku na vyeti
 Bonanza hilo lilifanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Mwisho

HABARI LUKUKI KUTOKA TFF

$
0
0
TAREHE 14 APRILI 2015
KAMATI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI YA BODI YA LIGI
Kocha Jackson Mayanja wa Kagera Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa Sugar kuwa walipewa rushwa.

Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu.

Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.  Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

Nayo Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar. Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.

Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.

Kipa Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


KAMATI YA MASHINDANO TFF
Kamati ya Mashindano ya TFF ilikutana jana kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL) iliyomalizika hivi karibuni.

Katika matukio ya SDL, Kamati imeipiga faini ya sh. 300,000 timu ya JKT Rwamkoma ya Mara kwa kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha kuvurugika. Adhabu hiyo kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya Ligi Daraja la Pili.

Nao makocha wa JKT Rwamkoma, Hassan Makame na Kamara Kadede wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi sita kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi namba moja katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9, 2015.

Wachezaji Shafii Maganga, Saleh Ali, Ismail Salim na Mussa Senyange wa JKT Rwamkoma ambao wanatuhumiwa kwa kushambulia mwamuzi kwenye mechi hiyo suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.

VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili nchini, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.


TTF YAFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI VIJANA
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana 27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa kimataifa baadae.

Vijana hawa mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini, wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.

Mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.

Semina hiyo ya siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe  17 Mei, 2015 inajumuisha vijana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.

Wakufunzi wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


DC KINONDONI AKUTANA NA WANANCHI KAWE MZIMUNI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI

$
0
0
      

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wananchi wa Kawe Mzimuni alipofika kutatua mgogoro wa ardhi kati yao na taasisi moja ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B iliyopo eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia DC Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.
 Mmoja wa wakilishi wa shule hiyo ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B,  Hamad Iddi Almas alimwambia DC Makonda (hayupo pichani), kuwa eneo hilo linamilikiwa na taasisi yao tangu siku nyingi.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, 
Paul Makonda.
Wananchi wa Kawe Mzimuni wakiwa kwenye ukuta walioubomoa kutokana na kujengwa eneo la barabara.
 …………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amezitaka pande mbili zinazogombania ardhi maeneo ya Kawe Mzimuni kufika na vielelezo vya umiliki wa eneo hilo ili kumaliza mgogoro huo.
Mwito huo ameutoa wakati akizingumza na wananchi wa eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi ambao walijichukulia sheria ya kubomoa ukuta uliojengwa na mwananchi mmoja wa eneo hilo kuwa ulijengwa kwenye barabara.
Mbali na kubomoa ukuta huo wananchi hao wanavutana  la taasisi moja ya dini ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B iliyopo eneo hilo kuwa imemega eneo la Shule ya Msingi ya Ukwamani.
“Nimekuja hapa baada ya kusikia mgogoro uliopo wa kugombea ardhi nafikiri ofisa mipango mji wa Manispaa alifika hapa kuzungumza nanyi naomba baada ya siku saba pande zote zinazovutana zije na vielelezo ofidsini kwangu hapo tutajua nani mmiliki wa eneo hilo” alisema Makonda.
Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.
Mmoja wa wakilishi wa shule hiyo ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B Hamad Iddi Almas alimwambia Makonda kuwa eneo hilo linamilikiwa na taasisi yao tangu siku nyingi jambo lililosababisha wananchi kuanza kuzomea wakipinga umiliki huo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

MAGAZETI LEO JUMATANO

Article 14

$
0
0

Obama kuiondoa Cuba kwenye orodha ya ugaidi

  • Saa moja iliyopita
Rais Barack Obama (kulia) na Rais Raul Castro wa Cuba (kushoto)
Rais Barack Obama amesema ataiondoa Cuba kutoka orodha ya Marekani ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani.
Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema hatua hiyo inakuja huku kukiwa na jitihada za kujenga uhusiano kati ya Marekani na Cuba.
Uwepo wa Cuba katika orodha hiyo pamoja na nchi za Syria, Iran na Sudan kilikuwa kigezo cha Cuba katika mazungumzo yake na Marekani ya kufungua ofisi za balozi kati ya nchi hizo.
Seneta wa chama cha Republican Marco Rubio ameishutumu Ikulu ya Marekani kwa uamuzi huo, akisema kuwa Cuba bado ni taifa linalofadhili ugaidi.
"Wanawahifadhi Wamarekani ambao wanakimbia mkono wa sheria, akiwemo mtu aliyemuua afisa wa polisi huko New Jersey zaidi ya miaka 30 iliyopita," amesema Bwana Rubio, Mmarekani mwenye asili ya Cuba ambaye alizindua kampeni yake ya uchaguzi wa rais wa Marekani 2016.
"Ni nchi ambayo pia inaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa."
Bwana Obama alitangaza tukio la kihistoria la kurejesha uhuasiano kati ya Marekani na Cuba mwezi Desemba 2015 lakini vikwazo vya kibiashara vya Marekani dhidi ya Cuba vinabakia, na vinaweza kuondolewa tu na baraza la Congress.

17 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA AL SHABAAB

$
0
0
Wavamizi walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo kabla ya wavamizi kuingia wakiwa wamejihami kwa bunduki
Watu 17 wameripotiwa kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa vibaya wakati wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shaabab waliposhambulia majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia.
Mwandishi wa BBC Mohammed Moalimu,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo
Kulingana na msemaji wa idara ya usalama wa ndani Mohammed Yusuf watu 8 waliuawa na wavamizi hao huku wanajeshi wawili wakipoteza maisha yao.
Askari mmoja ni wa muungano wa majeshi ya umoja wa Afrika.
Msemaji huyo anasema kuwa wavamizi hao walikuwa ni 7 wawili waliojilipua langoni huku wengine watano wakikabiliwa na maafisa wa usalama.
Walioshuhudia wanasema wavamizi hao walitumia bomu lililotegwa ndani ya gari kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab,
amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa
''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara ya elimu''
Mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa polisi.
Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde.
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .
Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo.
hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo .
Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.

Wakimbizi:UNHCR yaahidi kushirikiana na Kenya

$
0
0
Shirika hilo limeitaka serikali ya Kenya kufikiria upya kauli hilo la kuwafurusha wakimbiz
Shirika la umoja wa mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limesema kuwa liko tayari kufanya kazi na serikali ya Kenya ili kuhakikisha kuwa sheria za Kenya zinafuatwa kikamilifu katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab karibu na mpaka wake na Somalia.
Shirika hilo limeitaka serikali ya Kenya kufikiria upya kauli hilo la kuwafurusha wakimbizi na kufunga kambi hiyo katika kipindi cha miezi tatu ijayo.
Serikali ya Kenya ilitoa amri hiyo punde baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab kuwaua wanafunzi wakristu takriban 150 katika chuo kikuu cha Garissa mapema mwezi huu.
Shirika linalosimamia wakimbizi UNHCR liko tayari kushirikiana na Kenya kukomesha utovu wa usalama katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab
Makamu wa Rais William Ruto alitangaza kuwa angetaka wakimbizi hao warejeshwe makwao na kambi hiyo ya Dadaab ifungwe.
Kambi hiyo yenye wakimbizi takriban nusu milioni ndio kubwa zaidi duniani ikiwa na asilimia kubwa ya wakimbizi kutoka Somalia.
Serikali ya Kenya imesema inaushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa asilimia kubwa ya mashambulizi yanayotekelezwa nchini Kenya na kundi la waislamu la Al Shabaab yanapangiwa katika kambi hiyo ya Dadaab.
Haswa ikiashiria shambulizi la maduka ya kifahari ya Westgate ambapo ilidaia washambulizi waliingia nchini kama wakimbizi.
UNHCR inapinga madai hayo.
Kenya imedai kuwa Al Shabaab inapanga mashambulizi katika kambi hizo za wakimbizi
UNHCR inasema kuwa Kenya itakuwa inakiuka wajibu wake wa kuhakikishia wakimbizi usalama wao pindi wapoingia katika mipaka yake.
Serikali ya kenya kwa ushirikiano na UNHCR na serikali ya Somali iliweka mipango ya kurejesha wakimbizi makwao mwaka uliopita lakini mkataba huo ulikuwa utekelezwe kwa hiari.
Idadi ndogo sana ya wakimbizi hao walikubali kurejea makwao.

Mapigano yazuka upya Ukraine

$
0
0
Waasi walikuwa wamekubaliana kuondoa silaha nzito kama vifaru
Ukraine imesema kuwa imewapoteza maafisa wake 6 wa kijeshi katika kipindi cha saa 24 zilizopita kufuatia mashambulizi ya wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi.
Msemaji wa jeshi la Ukraine amesema kuwa kumekuwa na ufyatulianaja wa risasi usiku kucha.
Mapigano yameripotiwa kuendelea viungani mwa mji wa Donetsk.
Mwandishi wa BBC aliyekuwa na waasi wanaounga mkono Urusi pamoja na wakaguzi wa Ulaya karibu na kijiji muhimu cha mji wa Mariupol alisikia milipuko na kuona makombora yakirushwa.
Wachunguzi wa kimataifa wanaohakikisha kufuatiliwa kwa makubaliano ya awali
Mwandishi mmoja wa Urusi aliyekuwa na kundi hilo alijeruhiwa vibaya.
Awali mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain walieelezea wasiwasi uliopo kufuatia kuibuka upya
kwa mapigano mashariki mwa Ukraine hatua iliyokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa mwezi Februari.
Baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya
Waasi Mashariki mwa Urain
silaha ambazo zitaondolewa ni pamoja na vifaru na bunduki nzito nzito zenye uwezo wa uharibifu mkubwa.
Pande hizo mbili zilionekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa ndege wa Donetsk na kijiji cha Shyrokyne nje ya mji wa Mariupol.
Pande hizo pia zimekubaliana kuendelea kubadilishana wafungwa.

Lewis Hamilton ajifagilia

$
0
0
Lewis Hailton
Bingwa wa dunia wa mbio za magari ya langalanga wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton amesema yeye yupo vizuri zaidi kiakili kuliko mchezaji mwenzake wa timu hiyo Nico Rosberg. Hamilton anaamini kuwa kisaikolojia yupo juu ya Rosberg katika mapambano ya mataji ya msimu huu.
Lewis ameyasema hayo baada ya Nico Rosberg raia wa Ujerumani kumtuhumu mchezaji huyo kutumia mbinu za kumdhoofisha yeye ili ashinde. ‘‘Mara zote huwa nasema kwamba yeye ni bora kiakili lakini nafikiri mimi nipo bora zaidi mwaka huu” alisema Hamilton.
Rosberg alidai kuwa Hamilton ambaye ni raia wa Uingereza alipunguza mwendo makusudi wiki iliyopita katika shindano la China Grand Prix na kusababisha yeye kumgonga kutokea nyuma japo mjerumani huyo amesema jambo hilo limeshapita na kufutika.

Article 9

$
0
0

CAF yataja wapinzani wa Twiga - Afrika


Twiga stars viwanjani na shepolopolo ya Zambia
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetaja timu zitakazokwaana na timu ya Twiga Stars ya Tanzania katika fainali za soka za wanawake za Michezo ya Afrika itakayofanyika mwezi Septemba nchini Congo Brazzaville.
Twiga Stars imefanikiwa kucheza fainali hizo baada ya kuitoa timu ya Zambia (Shepolopolo).
Kwa mujibu wa CAF, timu zitakazochuana katika michezo hiyo baada ya kufuzu ni wenyeji Congo (Hosts), Cameroon, Ivory Coast (ambayo imefuzu baada ya Guinea Bissau kujitoa), Ghana, Misri, Nigeria, Afrika ya Kusini na Tanzania
Timu hizo zimefuzu baada ya kupata matokeo yafuatayo:
Nigeria 8-0 Mali (1-1- matokeo ya mechi ya kwanza)
Tanzania 2-3 Zambia (4-2)
Senegal 1-2 Egypt (0-0)
Afrika ya Kusini 5-0 Botswana (0-1)
Cameroon 2-1 Ethiopia (2-1)
Zimbabwe 2-2 Ghana (1-2)

Article 8

$
0
0

Dar Leopards kucheza Mombasa katika raga


Dar Leopards wakichuana na Rhino ya Arusha katika mchezo wa raga.
Timu ya raga ya Dar Leopards inatarajiwa kusafiri kwenda pwani ya Mombasa, Kenya na kucheza na klabu ya Mombasa Jumamosi katika kombe la Mamba (MHC). Dar Leopards ilishinda kombe hilo mwaka jana
Timu hizo zimewahi kupambana mara kadhaa katika miaka ya nyuma. Kwa mujibu wa viongozi wa Dar Leopards, timu hiyo itaondoka Ijumaa kwa usafiri wa basi siku moja kabla ya mechi.
Raga (rugby) ni miongoni mwa michezo isiyo maarufu sana nchini Tanzania na timu ya taifa ya Tanzania (Twigas) imeshiriki mara kadhaa michuano ya Afrika (CAR) na kupambana na nchi kama vile Kenya, Niger.
Dar Leopards ni miongoni mwa timu kubwa nchini Tanzania, mpinzani wake mkubwa ni ni timu ya Arusha Rhinos.

Article 7

$
0
0

Azam kuitoa Yanga,pia itacheza na Mgambo


Kikosi cha Azam
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Jumatano katika viwanja viwili nchini Tanzania, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Azam itakuwa katika jitihada za kujaribu kutetea ubingwa baada ya kutoa droo katika mechi zake mbili zilizopita, hivyo kuipa nafasi Yanga.Azam, ambao ndio mabingwa watetezi, wana pointi 38 huku Yanga wakiongoza ligi kwa pointi 46.
Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.

Article 6

$
0
0

Drogba arejesha alichojaaliwa kwa jamii.


Didie Drogba ana haki ya kutabasamu,amerejesha kwenye jamii yake kile alichojaaliwa.
Mshambuliaji wa timu ya Chelsea F.C. Didier Drogba amezindua hospitali ya kwanza, kubwa na ya aina yake kati ya tano alizo wahi kuahidi kuzijenga kama sehemu ya kujitolea kwa jamii yake .
Hospitali hiyo iko wilaya ya Attécoubé katika mji wa kibiashara wa Abidjan, hospitali hiyo imemgharimu nguli huyo wa kandanda kiasi cha dola milioni moja za kimarekani ili kukamilisha mjengo huo wa afya ;na hospitali hiyo ni maalumu kwa wanawake na watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu .
Hospitali hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba mia nane (800) huduma kadhaa zinapatikana ikiwamo chumba cha uchunguzi, wodi ya wazazi,kitengo cha watoto,jengo la x-ray ,jengo la kisasa la maabara,duka kubwa la dawa,jengo la kulaza wagonjwa na jengo tengefu la wagonjwa.
Inakadiriwa hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu hamsini kwa mwaka na hii ni kwa muujibu wa katibu mkuu wa asasi ya Didier Drogba Foundation , Guy Roland Tanoh ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo.
Hospitali zingine nne zilizo katika ahadi za mwanasoka huyo ziko katika hatua za ujenzi za mwisho mwisho kukamilika ambazo ziko nchini Ivory Coast katika miji ya Yamoussoukro, San Pedro, Man na Korhogo na zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao.
Drogba
Asasi hiyo ya Drogba foundation inaandaa chakula cha hisani mjini London mwezi huu wa April tarehe 18 ili kupata fedha za kukamilisha miradi hiyo.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Chelsea na pia timu ya Elephants anabakia kuwa mchezaji na mfungaji bora na wa mfano wa kuigwa nchini mwake pamoja na kwamba amestaafu kuichezea timu yake ya taifa,ambayo iliutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa mwaka huu nchini Equatorial Guinea mnamo mwezi wa February.
Kazi nzuri Didier Drogba! .

Mikutano ya Majira Kipupwe imeanza rasmi Mjini Washington DC.

$
0
0

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier,  akipata maelezo kutoka kwa Bw. Said Ngosha Magonya, ambaye ni  Kamishina wa Fedha za Nje kuhusu utaratibu uliopangwa na Tanzania katika Mikutano hii ya majira ya kipupwe.
Mikutano ya Majira  Kipupwe imeanza rasmi  Mjini Washington DC.
Mikutano ya majira ya  Kipupwe imeanza rasmi tarehe 14/4/2015 na kuhudhuriwa na nchi mbalimbali wanachama zaidi ya 188. Mikutano hii huudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi kutoka serikalini, waandishi wa habari, Mashirika na Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na kamati za kifedha.Taasisi hizo kwa pamoja zitajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Tanzania ni nchi wanachama katika Mikutano hiyo.Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya  ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile ambaye ni  Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha  Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi na manyunyu ya hapa na pale.

Imetolewa na:
Msemaji wa Wizata ya Fedha
Ingiahedi C. Mduma
14/4/2015
Washington DC.


Viewing all 21765 articles
Browse latest View live